Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 899
- 999
Baada ya DC Hapi wa Kinondoni kuagiza kakamatwa kwa Mbunge wa Kawe Halima Mdee asubuhi ya leo kwa kosa la uchochezi na kumdhihaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli hapo jana Makao ya Chadema;
Jioni hii Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameagiza kamati ya Kinga na Madaraka ya Bunge ikutane kumjadili kwa kulifedhehesha Bunge kwa maneno yake mbele ya waandishi wa habari hapo jana.
Jioni hii Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameagiza kamati ya Kinga na Madaraka ya Bunge ikutane kumjadili kwa kulifedhehesha Bunge kwa maneno yake mbele ya waandishi wa habari hapo jana.
"Mheshimiwa Kabudi wakati anahitimisha hoja yake hapa alitoa somo kuhusu ukaidi kuhusu ujeuri na akawa ametuasa kama mtu mzima jinsi ya kwenda. Kwa wale mlioangalia Mitandao na kadhalika, mtakuwa mumeona Mbunge mwenzetu Halima Mdee, ameendeleza huo ujeuri na huo ukaidi kwa maneno mabaya ya kuendelea kumdhalilisha Spika, na mimi nipo tayari kwa Shughuli hiyo.
Kwa hiyo kwa mara nyingine kama mnavyojua, mtu hata kama akiwa Magereza kama amefanya makosa huko huko Magereza basi anapelekwa Mahakamani akiwa huko huko Magereza.
Kwahiyo naelekeza kamati yetu ya Maadili kwa wakati unaofaa mtamuita Mheshimiwa Halima Mdee popote pale atakapokuwa kama ikibidi aletwe kwa Pingu mtaniletea hati nitaisaini, atakuja hapo kwenye kamati na wakati mwafaka atarudi tena hapa. Na tutafika mahali tutaelewana tu kiswahili".
Amesema Spika Ndugai