Mbunge Wilfred Lwakatare afutiwa kesi ya kutaka kuteka na kumdhuru Denis Msaki

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Mahakama imefuta kesi ya kula njama ya kudhuru iliyokuwa imebaki kisutu ikimkabili mbunge wa Bukoba Mjini (CHADEMA) Wilfred Lwakatare.

Serikali imesema haina nia ya kuendelea na kesi hiyo.
lwa.jpg

Kutoka kushoto: Frank Lwakatare, Wakili dr. Julius Lugaziya, Wlfred Lwakatare na Wakili Zebron. Leo 21/09/2017

Hapo awali Jan 25, 2012, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema,) Wilfred Lwakatale na Ludovick Walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka manne.

Wakili Rweyongeza alililata kosa la kwanza ambalo linawakabili washitakiwa wote kuwa ni la kula njama kutenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , na kwamba mnamo Desemba 28 mwaka jana, huko Kimara King'ong'o Stopover, wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia sumu kwa lengo la kumdhuru Denis Msaki ambaye alikuwa ni Mwanahabari wa Gazeti la Mwananchi ambalo ni kinyume na kifungu cha 227 cha sheria hiyo.

Wakili Rweyongeza alilitaja kosa la pili kuwa ni la kula njama ambalo pia ni kwaajili ya washitakiwa wote ambalo ni kinyume na kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka Msaki kinyume na kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

Aidha alilitaja kosa la tatu kuwa ni kutenda kufanya mkutano wa kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.

Wakili Rweyongeza alilitaja shitaka la nne ambalo linamkabili Lwakatare peke yake ni aliwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28 mwaka jana, Lwakatale akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka King’ong’o kwa makusudi aliliruhusu kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick cha kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msaki.

Walikuja kufutiwa haya Mashitaka na kukamatwa tena kwa Mashitaka ya kutaka Kumdhuru Denis Msaki ambalo ndo leo Wamefutiwa pia na kuachiwa huru.

Habari zaidi soma;.

Lwakatare aachiwa huru kisha kukamatwa hapo hapo kwa kosa lingine
Lwakatare, Ludovick wafikishwa mahakamani Kisutu

Hatimae Lwakatare huru kwa mashitaka ya Ugaidi
 
Leo September 21, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ‘DPP’ kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi dhidi yake ya kula njama ili kutenda kosa.
 
DPP amekuwa kama hajui chakufanya ila jicho la tatu linasema tunafukia ili mtuone wema kumbe mungu anajua roho zetu zimejaa nini
 
Hiii ndo lunga mpya ya "ma-DPP kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi dhidi yake"
Wanakusotesha ndani kwa miezi kadhaa baadae wanasema hana nia ya kuendelea na shtaka hilo. Tunajua ndo maangizo kutoka juuu kuwa piga tarehe kesi zao tunaweaken na kuwaharibu akili zao, wakishanyooka mnawaachia huru. Hii ndo falsafa ya serikali ya awamu hiii, uraiani wakomeshe kwa kutumia polisi, mahakama na jeshi. Wakiwa bungeni wafukuze wasiongee wala kuonekana msimu mzima wa bunge. Hakuna demokrasia, hakuna uhuru wa kuongea, hakuna kukosoa serikali, are you an ANGEL????? Pandeni mpandancho maana mtavuna kwa wakati asema Bwana.
 
Kesi ya kubambikiwa na Mwigulu.

Leo September 21, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ‘DPP’ kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi dhidi yake ya kula njama ili kutenda kosa.
 
Mwisho wa mwaka tuwe tunaletewa marejesho ya kesi anazofungua Jamhuri....

Anashindwa ngapi anashinda ngapi.
 
Back
Top Bottom