Breaches of Fundamental Freedoms and rights to Free, Fair and Credible election

S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
851
1,000
Wanabodi, kama heading inavyosomeka:

TLS- Tanganyika law society na wanasheria wengine, tuleteeni Test case dhidi ya NEC jinsi walivyooendesha uchaguzi huu chonde chonde.

Tunafahamu kwamba, katika katiba yetu hii ya 1977, "the legitimacy of presidential elections results cannot be questioned in any court of law regardless of the irregularities, illegality or fraud". This means civil disobedience is the only way to reject flawed poll results.

Lakini kabla ya kwenda huko kwenye civil disobediences:

1. Ni kwa nini TLS- Tanganyika law society (pro bono) na wanasheria wengine wasiende kuhoji mahakamani kwamba hiki kipengere ni unconstitutional maana kina breach fundamental rights and Freedoms guaranteed under our constitution and laws therein na kwamba ni NEC ndio wame breach hizo fundamental freedoms and rights na hivi wamefanya kitu ambacho hakiendani na rights, freedoms na credibilities za uchaguzi...

2. The breaches to the right to free, fair and credible election. Kwenda mahakamani ni kuomba muongozo wa hii breach of fundamental rights and freedom sio ku-question legitimacy of presidential elections results. Kwa maana nyingine kama kuna breaches yeyote ya hiyo fundamental freedoms by NEC, athari yake ni kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi bila mkwaruzo...

3. Cha kutakiwa ni kwenda tu mahakamani kusema kwamba NEC wame- breach fundamental rights and freedoms zinazohusiana na uchaguzi juu ya free, fair and credible election na sio mambo mengineyo ( Mfano wa breaches hizo ni kura kupigwa kabla ya wakati, mawakala kuzuiliwa, haya hayahusiani na irregularties au fraud, but ni wizi ambao hautakiwi kisheria)... na tuone mahakama itasimamia upande gani kama inakubaliana na breaches hizo za fundamental rights and freedom za uchaguzi...Wanasheria, amkeni na changamkeni...hata UN sec council iliwahi kubwagwa na mahakama ya ulaya- someni Kadi case 1-2- summary yake ni hii hapa: Kadi Case – Constitutional Core Values and International Law – Finding the Balance?

4. Mwisho, kwa NEC kuegemea sana upande mmoja maana yake- wali- exceed scope of their authority - acted ultra vires... hii ni hoja Nyingine ya Kuwatoa kwenye mstari

Kadi Case – Constitutional Core Values and International Law – Finding the Balance?

Povu ruksa
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,006
2,000
Wapinzani wamekataa matokeo yote ya Udiwani, Ubunge na Urais. Kwahiyo, iwapo kweli wana ushahidi wa kuchezewa rafu, waende mahakamani kushitaki Ubunge na Udiwani. Iwapo zaidi ya nusu ya majimbo ya Ubunge yatatenguliwa, itakuwa rahisi kutetea hoja kuwa matokeo ya Urais yanahitaji mjadala.

Kwa sasa Mbowe na wenzake hawana hoja zenye mashiko zaidi ya hisia za uchungu wa kupoteza ajira.
 
S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
851
1,000
Wapinzani wamekataa matokeo yote ya Udiwani, Ubunge na Urais. Kwahiyo, iwapo kweli wana ushahidi wa kuchezewa rafu, waende mahakamani kushitaki Ubunge na Udiwani...
Hata kama wameyakataa, haiwazuii kwenda huko kuishtaki NEC kwa hizo breaches za fundamental freedoms, mahakama ikisema kwamba haki zimekiukwa maana yake ni kwamba NEC hawana uwezo wa kusema kwamba uchaguzi ulikuwa free na Fair na maana ya pili ni kwamba uchaguzi utakuwa void ab nitio, haina hata haja ya kujadili zoezi zima.

Ni hicho tu kipendegere cha breach ndio hicho kitacho watoa hao wapinzani na sio hii ya nataka sitaki, maandamano etc, yawapasa wasome jinsi gani na njia gani yule askofu wa malawi alipitia.
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,101
2,000
Mahakama tanzania zenyewe zimeshalawitiwa na mtakatifu.

Ilifunguliwa kesi ya kuwapinga "WAKURUGENZI" kusimamia uchaguzi kwasababu ni wateule wa rais (wanakuwa biased), High Court ilikubalina na hoja hio. Wanasheria wa mtakatifu wakakata rufaa na mahakama ya rufaa ikapiga chini hukumu ya High Court, mtakatifu akashinda kesi.

Hio keso unayosema kufunguliwa si itakua kazi bure mkuu.

Nchi hii inatakiwa "KATIBA" na "SHERIA NYINGI" zifumuliwe fumuliwe kisawasawa, maana katiba na sheria nyigi zimekua designed kuwapa madaraka ya maisha CCM na kuwaweka juu ya sheria.
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,006
2,000
hata kama wameyakataa, haiwazuii kwenda huko kuishtaki NEC kwa hizo breaches za fundamental freedoms, mahakama ikisema kwamba haki zimekiukwa maana yake ni kwamba NEC hawana uwezo wa kusema kwamba uchaguzi ulikuwa free na Fair... na maana ya pili ni kwamba uchaguzi utakuwa void ab nitio... haina hata haja ya kujadili zoezi zima.. ni hicho tu kipendegere cha breach ndio=cho kitacho watoa hao wapinzani na sio hii ya nataka sitaki, maandamano...etc... yawapasa wasome jinsi gani na njia gani yule askofu wa malawi alipitia.
Wapinzani wa Tanzania hawaamini Tume, hawaamini Polisi, hawaamini Usalama wa Taifa, hawaamini Mahakama, hawaamini Jeshi la Wananchi.

Watu wa namna hii, hata kunapokuwa na njia za amani zinazoweza kuwapa mafanikio, hawawezi kuziangalia.

Maandamano yao yamelenga kupata political relevance tu ili waendelee kuwa kwenye midomo ya watu. Hayajalenga kutafuta utatuzi wa chochote.
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,006
2,000
Mahakama tanzania zenyewe zimeshalawitiwa na mtakatifu.

Ilifunguliwa kesi ya kuwapinga "WAKURUGENZI" kusimamia uchaguzi kwasababu ni wateule wa rais (wanakuwa biased), High Court ilikubalina na hoja hio. Wanasheria wa mtakatifu wakakata rufaa na mahakama ya rufaa ikapiga chini hukumu ya High Court, mtakatifu akashinda kesi.

Hio keso unayosema kufunguliwa si itakua kazi bure mkuu.
Sasa kama hawaamini Mahakama, wanategemea chombo gani kiwape haki? Au wanataka kupindua serikali?
 
S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
851
1,000
Wapinzani wa Tanzania hawaamini Tume, hawaamini Polisi, hawaamini Usalama wa Taifa, hawaamini Mahakama, hawaamini Jeshi la Wananchi.

Watu wa namna hii, hata kunapokuwa na njia za amani zinazoweza kuwapa mafanikio, hawawezi kuziangalia.

Maandamano yao yamelenga kupata political relevance tu ili waendelee kuwa kwenye midomo ya watu. Hayajalenga kutafuta utatuzi wa chochote.
Nakubaliana na wewe mara 100, lakini pia labda public interest defenders kama hao TLS Labda nao wataamka toka huko walipo lala.
 
jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
4,772
2,000
Ni maandamano tu yatakayoleta haki, hakuna taasisi ya umma iliyo huru kwa sasa.
 
S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
851
1,000
ni maandamano tu yatakayoleta haki, hakuna taasisi ya umma iliyo huru kwa sasa.
Kabla ya kwenda huko na jazba za kushindwa, yafaa kuangalia all remedies ikiwemo mahakamani hata kama hawaikubali kwa ule usemi wa kesi ya ngeredere.
 
Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
4,054
2,000
Nakubaliana na wewe mara 100... lakini pia labda public interest defenders kama hao TLS Labda nao wataamka toka huko walipo lala
Rejea kilichomkuta yule mwanasheria aliyeanza "kusumbua" kuhusiana na mambo ya uchaguzi. Hakuna wakumfunga paka kengele.
 
S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
851
1,000
Rejea kilichomkuta yule mwanasheria aliyeanza "kusumbua" kuhusiana na mambo ya uchaguzi. Hakuna wakumfunga paka kengele.
Kwa hiyo wasijalibu hata kwenda huko mahakamani, yaani kwa maana nyingine tukubali kwamba mwizi akituibia, basi tukae kimya tu na tujisemeze kwamba lilikuwa kosa letu na sio la mwizi au unashauri nini mkuu, maana inajulikana kwamba wizi ulifanyika, njia ni ipi inayofaa? sio hii ya kuwapa taabu polisi ili wachague wapi pa kufyatulia risasi.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,988
2,000
Duh, haya ni maswali ya mambo makubwa!. Sijui kama yatachangiwa na wengi humu!, maana wana jf wa kisasa, wamezoea mambo madogo madogo tuu ya issues nyepesi nyepesi.
P
 
Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
4,054
2,000
Kwa hiyo wasijalibu hata kwenda huko mahakamani... yaani kwa maana nyingine tukubali kwamba mwizi akituibia, basi tukae kimya tu na tujisemeze kwamba lilikuwa kosa letu na sio la mwizi...au unashauri nini mkuu, maana inajulikana kwamba wizi ulifanyika... njia ni ipi inayofaa? sio hii ya kuwapa taabu polisi ili wachague wapi pa kufyatulia risasi...
Hakuna njia bora kuliko nyingine, cha msingi kwa kuwa kilichotokea hakijawahi kufanyika kwa namna hii basi ili kukabiliana nacho inabidi kifanyike kitu ambacho hakijawahi kufanywa kwa namna mpya
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,244
2,000
Wapinzani wamekataa matokeo yote ya Udiwani, Ubunge na Urais. Kwahiyo, iwapo kweli wana ushahidi wa kuchezewa rafu, waende mahakamani kushitaki Ubunge na Udiwani. Iwapo zaidi ya nusu ya majimbo ya Ubunge yatatenguliwa, itakuwa rahisi kutetea hoja kuwa matokeo ya Urais yanahitaji mjadala.

Kwa sasa Mbowe na wenzake hawana hoja zenye mashiko zaidi ya hisia za uchungu wa kupoteza ajira.
Kuna mahakama au kuna tawi la CCM?
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,244
2,000
Hakuna njia bora kuliko nyingine, cha msingi kwa kuwa kilichotokea hakijawahi kufanyika kwa namna hii basi ili kukabiliana nacho inabidi kifanyike kitu ambacho hakijawahi kufanywa kwa namna mpya
Naunga mkono hoja kabisa
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,244
2,000
Kwa hiyo wasijalibu hata kwenda huko mahakamani, yaani kwa maana nyingine tukubali kwamba mwizi akituibia, basi tukae kimya tu na tujisemeze kwamba lilikuwa kosa letu na sio la mwizi au unashauri nini mkuu, maana inajulikana kwamba wizi ulifanyika, njia ni ipi inayofaa? sio hii ya kuwapa taabu polisi ili wachague wapi pa kufyatulia risasi.
Bora kinuke ilitupate solution ya kudum, hatuna mahakama wala nini ni shina la CCM.
 
S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
851
1,000
Duh, haya ni maswali ya mambo makubwa!. Sijui kama yatachangiwa na wengi humu!, maana tumezoea madogo madogo tuu!
P
Walalamikaji wasije sema au kusingizia kwamba hawakuambiwa... kutokwenda mahakamani Kwa kisingizio chochote kile ni ku- second guess maamuzi ya mahakama ambayo hatujui itaamua nini hii test kesi ikifunguliwa...
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,567
2,000
TLS nayo imeshageuzwa kikundi cha kijani, usitegemee jipya lolote toka kwao.

Taasisi zote kama bunge, mahakama na polisi nazo zinamuogopa jiwe, zinatenda kwa kadri ya mapenzi yake.

The only solution ni maandamano, hayo ndio yangewafanya wenye mamlaka waamke usingizini, wajue kumbe wananchi ndio wenye nguvu na mamlaka zaidi yao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom