Brazil yaihurumia Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Brazil yaihurumia Tanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jul 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Rais Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake rais wa Brazil Lula Da Silva akiwapungia baadhi ya watanzania mkono

  RAIS wa Brazil, Lula da Silva amesema serikali yake inafikiria kuisamehe Tanzania mkopo wa dola za Marekani 240 milioni (zaidi ya Sh336bilioni) ambazo zilitumika katika ujenzi wa barabara ya Morogoro - Dodoma miaka ya 80.
  Awali mkopo huo ulikuwa dola 49 milioni lakini uliongezeka kwa sababu ya riba hadi kufikia dola 240 milioni ambazo serikali ya Tanzania imeshindwa kuilipa.


  Akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya Maonyesho ya 34 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Silva alisema serikali yake itakaa na kujadili suala hilo baada ya serikali ya Tanzania kusema haina uwezo wa kulipa deni hilo.


  Alisema serikali ya Brazil ilitoa dola 49 milioni za Marekani kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo lakini, hadi sasa halijarudishwa jambo ambalo limewafanya wajadiliane juu ya utaratibu unaofuata kabla ya kuwasamehe.


  “Tunafikiria kuisamehe Tanzania deni letu la dola 240 milioni ambazo tuliwakopesha kwa ajili ya ujenzi wa barabara na hadi sasa wameshindwa kurudisha. Nitazungumza na Waziri wangu wa Fedha juu ya utaratibu unaofuata,” alisema Silva.


  Rais huyo wa Brazil alieleza pia kuwa nchi yake imepanga kujikita katika masuala ya uwekezaji ili kuhakikisha kuwa uchumi wa Tanzania unakuwa na kupunguza umaskini.


  Alisema katika kufanikisha jambo hilo, Brazil itatoa watalaamu wa fani mbalimbali ikiwemo mazingira, kwa ajili ya kutoa elimu ya uboreshaji wa mazingira na uzalishaji wa nishati mbadala kwa ajili ya kuzalisha mafuta.


  Kwa mujibu wa Silva, nchi za Afrika sio maskini, kwa sababu zina rasilimali nyingi ambazo zikitumiwa vizuri, zinaweza kupunguza umaskini.


  Aliishauri Tanzania kutoa elimu kwa wananchi wake ili waanze kununua bidhaa zinazozalishwa nchini mwao ili kuchangia ukuaji wa uchumi na ajira.


  Rais Silva alibainisha kwamba, kama wananchi watapenda bidhaa zinazozalishwa nchi za nje, watarudisha nyuma maendeleo na kuharibu uchumi wa ndani ya nchi, hivyo kuwataka Watanzania kujenge tabia ya kununua bidhaa zao ili wachangie kukuza uchumi wao.


  Kwa mujibu wa Silva, Brazil ilikuwa miongoni mwa nchi maskini duniani lakini baada ya kuwahamasisha watu wake kununua bidhaa za ndani, iliweza kupita katika kipindi kigumu cha mtikisiko wa uchumi wa dunia bila madhara makubwa.


  “Nilishirikiana na media (vyombo vya habari) kuhakikisha kuwa tunatoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa bidhaa za ndani kwa sababu kampuni zliyopo zimechangia kutoa ajira kwa vijana na kukuza uchumi, hivyo basi hatukuhitaji bidhaa za nje wakati za ndani zipo,” alisema na kuongeza:


  “Nimefungua milango ya uwekezaji, Wabrazil watakuja hapa kwa ajili ya kuwekeza maeneo mbalimbali, ili kuhakikisha kuwa tunashirikiana kukuza uchumi wa Tanzania”.
  Brazil yaihurumia Tanzania

  Tunadaiwa Madeni na Wafadhili wetu mpaka wanaamuwa kutusamehe kasheshe kweli Tanzania yetu. Je tutakwenda Brazil kuomba tena msaada?
   
 2. doup

  doup JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  aibu tupu; timekuwa wazurumaji brasil walikuwa maskini kama sisi tukashindwa kuwalipa; alafu bado tunaendelea kuwalea mafisadi na kuendekeza safari za nje, chai/vitafunwa asubuhi serikalini bajet ni bilioni kadhaa.

  Mpaka mgeni aje ndio atushauri tupende vya kwetu!!!!!?????? Hapo utasikia watakavyokurupuka na kuja na kamati za uhamasishaji==kula pesa
   
 3. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Tangu lini nchi ikaihurumia nchi nyingine? Hizi ni lugha za siasa tu ambazo hutumika katika kutoa misaada inayotufanya tuendelee kuwa maskini. Hivi ngoja niulize, ni nchi gani iliyowahi kuendelea kwa kupewa misaada, na si kuzalisha?

  Kinachofanyika hapa, Brasil wameona opportunity nyingi za kuchuma toka kwetu, na kusema kutusamehe deni ni lugha ya kisiasa tu kujiweka karibu na ulaji. Ndivyo ilivyo kwa mataifa mengine kama India, China n.k., kila mtu anakuja kuchuma.

  Siku zote, mali ya mjinga huliwa na mwerevu!
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hii imeingia shkio la kushoto na kutokea shkio la kulia.

  Kinachotakiwa sio serikali kuelimisha tu, bali ku-enforce kwa kutumia sheria na kuzifuatilia, kwamba bidhaa fulani zinazozalishwa nchini zisiingizwe nchi, na atakayekiuka apewe kifungo na faini juu. Wakati inafanya hivo inahakikisha inapanua uzalishaji kukidhi soko la ndani.

  Lakini haya yatawezekana wapi wakati kazi tumewapa watu wasio na maono??
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Je, inawezekana hii inamaanisha hata watoa kazi hawana maono?
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Brazil wanatuhurumia, lakini sisi wenyewe hatujihurumii!!! Basi viongozi wasiokuwa na maono tunawafahamu, sasa situwatoe Oktoba 2010?!!
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Umesoma ile thread ingine inayosema CCM haina mpango wa kung'oka iwe kwa heri au shari?? Which is quiet true, mbinu ya kwanza inayotumika ni ku-confine mawazo ya wadanganyika kwenye uchaguzi only, wakati wameshaandaa surprise package kitaaaambo..(ndio maana ya JK kuwaambia wafanyakzi kuwa go and f^%% urself, sihitaji kura zenu)

  (I mean this is for starters)
   
 8. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2010
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tanzania zaidi ya uijuavyo..... and you can hear the politicians boasting around kwamba wamesamehewa madeni kutokana na mahusiano mazuri waliojenga na nchi za nje....WTF!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...