Brazil 'kuchafuka' punde

kuna tetesi kuwa ile mechi tulikuwa tunachezeshewa play station, kuna mchina alihack tv broadcast zote, hivyo fifa watafanya press conference leo kuipa dunia matokeo sahihi ya mechi.

Hahahahahaha
 
Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva ametangaza siku tatu za maombolezo na kuamuru bendera ya nchi hiyo ipandishwe nusu mlingoti kufuatia kichapo ilichokipata timu ya taifa ya Brazil cha 7-1 toka Ujeruman.

Akitangaza taarifa hiyo kwa vyombo vya habari mjini Brasil msemaji wa ikulu ya Brazil Costantino Bald amesema rais da silva ameuzunishwa na kipigo hicho na kukifananisha na janga la taifa. amesema Rais hakupata hata chembe ya usingizi usiku wa tarehe 8 kuamkia tarehe 9 ambapo mchezo huo ulichezwa.

"Ndugu zangu rais hajapata usingizi kabisa na anaamini hali hiyo ndiyo waliokua nao wabrazil wengi" na kuongeza.

"Wajerumani hawana huruma kabisa, hata hivyo nawasihi raia wote wa Brazil kushikamana na kuwa watulivu katka kipindi hiki kigumu inachokipitia nchi yao".

Timu ya taifa ya Brazil imekutana na dhahama ya kufungwa 7-1 na timu ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali wa kwanza wa fainali za kombe la dunia zinazofanyika nchini Brazil.
 
Angewapa japo mwezi mmoja yaani ilikipigo ilikuwa na kwaajili ya paka dowezi kwa jirani.
 
kuna tetesi kuwa ile mechi tulikuwa tunachezeshewa play station, kuna mchina alihack tv broadcast zote, hivyo fifa watafanya press conference leo kuipa dunia matokeo sahihi ya mechi.

hii kitu nimeiona kwenye moja ya magroup ya sport kule facebuk
 
Mwambieni huyo Rais, tubadilishane timu..... yake ije Tanzania na yetu Taifa Stars iende Brazil...
 
Rais wa Brazil kwa sasa ni mwanamama Dilma Rouseff; sio Lula da Silva, mwanamama huyo amewaomba radhi wananchi wake basi na wala sio kushusha bendera, wacha upotoshaji, unawaharibia wenzio wasio na vyanzo mahsusi vya habari!! No research no right to speak....read (no right to post anything on this forum)
 
Mmmmh;
Ya kweli hayo jamani
au ndo mnatufanyisha sikukuu ya wajinga tena leo?
 
moderator tunaomba muondoe huu uchafu hauna hadhi ya kuwepo hapa.
 
Huyu anafaa kula ban ya mwaka mzima.
 
Lula sio Rais wa Brazil kwa sasa, usitudanganye
 
Ile ni aibu ya dunia tangu ilipoanza

Kwi kwi kwi kwi...Jana wachezaji wote wa Brazil walikuwa kama wamewehuka uwanjani....Niliwaonea huruma sana..

Tuombe Munguargentina wasipatwe na majanga kama ya Ndugu zao Brazil..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…