Braza Mtikila, visa na vituko hadi lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Braza Mtikila, visa na vituko hadi lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiranja Mkuu, Jul 30, 2010.

 1. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Atakiwa kumhudumia Mtikila kifungoni

  MLALAMIKAJI katika kesi ya madai dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila, ametakiwa kumhudumia Mwenyekiti huyo wa DP wakati akitumikia kifungo chake cha miezi sita jela.

  Amri hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Ilala, Joyce Minde, baada ya kumhukumu Mtikila kutokana na kupatikana na hatia ya kushindwa kulipa deni la Sh milioni 9.8 mali ya Paschazia Matete.

  Hukumu hiyo ikitekelezwa itakuwa ni mara ya pili maishani mwake, Mtikila kufungwa jela mara ya kwanza ikiwa ni katika Gereza la Ukonga, Dar es Salaam Desemba 14, 1999 kwa hatia ya uchochezi na kutumikia kifungo cha mwaka
  mmoja.

  Mwaka huo Mtikila alipatikana na hatia ya kutoa kauli chafu na za uchochezi dhidi ya viongozi wa CCM na Serikali yake juu ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Horace Kolimba.

  Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kinondoni, Gabriel Mirumbe, akamkuta na hatia ya kutoa maneno kwamba viongozi wa CCM na Serikali walimuua Kolimba na ni mashetani.

  Kuhusu hukumu ya jana, Minde, alifikia uamuzi huo baada ya Mahakama kukubali ombi la upande wa Mashitaka la kumfunga Mtikila akishindwa kulipa deni.

  Mahakama hiyo ilihukumu bila yeye kuwa mahakamani hapo na pia bila taarifa. Minde alisema Mtikila ataanza kutumikia kifungo baada ya mdai, Matete, kutoa fedha hizo za matumizi ya Mchungaji huyo.

  “Mshitakiwa atakamatwa na ataanza kutumikia kifungo baada ya Matete kuleta Sh 100,000 kila mwezi, kwa ajili ya matumizi ya Mtikila kwa kipindi ambacho atatumikia kifungo chake,”alisema.

  Aliongeza kuwa endapo Matete hataridhika na uamuzi huo atakamata mali yoyote ya Mtikila itakayoshikiliwa na Mahakama hadi atakapolipwa deni lake.

  Awali upande wa Mashitaka, uliiomba Mahakama hiyo kumfunga kifungo cha madai endapo atashindwa kulipa deni hilo, baada ya Mahakama kushikilia nyumba yake lakini Mtikila akadai kuwa hana nyumba kwani aliyokuwa nayo alishaiuza.

  Hata hivyo, Mahakama ilimtaka Mtikila kutaja siku ya kulipa fedha hizo, lakini hakuonekana na kutoa sababu mbalimbali za kutofika.

  Ilidaiwa kuwa Mtikila akiwa na mwenzake aitwaye Mariam Issa, walifikishwa mahakamani hapo mwaka juzi wakikabiliwa na mashitaka ya madai ya Sh milioni 9.8 likiwa ni deni kutoka kwa Matete.
   
 2. s

  schulstrasse Senior Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: May 31, 2010
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo ndo kesi ya Madai bwana...both sides benefits....ila hukumu kiboko siajwahi ona
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Jul 30, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Du!
   
Loading...