Bravo JK: Jin Ping and Obama in Dar , all done in one stride!!

Bravo JK: Jin Ping and Obama in Dar , all done in one stride!!

....Na hapo ndo nampa heko JK kwa kucgeza karata na kulamba dume, kwa kuwaleta madingi hawa.

Ukarimu ulioje Wachina na Wamerekani watafanya kazi usiku na mchana, wakatwe kodi ili misaada itolewe kuleta maendeleo kwa Watanzania?! Kabla ya kutoa pongezi, kama unashughulisha akili yako hata kwa kiwango kidogo tu lazima ujiulize; Kati ya hawa wageni, Je kuna hata mmoja ambaye ujio wake kweli ilikuwa ziara ya matembezi au mapumziko ya kuja kukwea bembea kama wafanyavyo viongozi wetu? Kama kuna mikataba ya miradi ya kiuchumi imefanyika, je ni rasilimali za nani zimefunganishwa kwenye hiyo mikataba, Je, kuna rasilimali hata moja ambayo ni mali binafsi ya Ndugu Kikwete, Salma na wanawe; ambayo si ya wananchi wa Tanzania? Au je, rasilimali hiyo haikuwepo kabla katika ardhi ya Tanganyika kaileta Rais Kikwete? Ni vema kujua kwa nini watangulizi wake, akiwemo wa zama za hivi karibuni ambaye naye alikuwa mlafi hakufikia kiwewe cha sasa katika kuzifungua na kuziwekea fungani rasilimali zetu kwa pupa kubwa kama hii. Huwezi kupata neno bora zaidi ya uwendawazimu kwa mtu anayeshika hili na kabla hajakamilisha anaanzisha lile na kuacha hili likiwa bado halijapata muelekeo. Serikali ya Kikwete imekuwa kama vile imeambiwa baada ya 2015, vizazi vijavyo vitaletewa Tanzania nyingine yenye rasilimali tele, na kama haiwezi kuzimaliza sasa basi zitachacha! Kwa hiyo jukumu la serikali ya awamu yao ni kutapanya na kugawa kila kilichopo sasa. Kiwewe hiki ndicho kinafanya swali la nini kipaumbele cha maendeleo kwa uchumi wa Tanzania kuwa gumu kwa watunga sera wetu. Wakilala leo na MADINI, kesho wataamka na KILIMO KWANZA, keshokutwa watakuja na ELIMU KWANZA na mtondo watasahau watakuambia NISHATI KWANZA kabla hawajaota mchana na kusema AFYA KWANZA na mtondogoo wakakueleza MIUNDOMBINU KWANZA! Kwanza inatumika katika kila jambo jipya mpaka mwishowe kimantiki inasimama kumaanisha MWISHO-KWANZA.

I liked that part highlighted in purple!
Source: Nitatoa pongezi kwa Rais Kikwete nikijua undani wa Mikataba ya Marais Xi na Obama - wavuti.com
 
Nafikiri itakuwa makosa kumlaumu JK and the like minds kama Membe,

hawa ni watanzania wamekulia hapa, kwahiyo wamebeba tabia, taratibu, tamaduni na vipaumbele kulingana na mtazamo wa jamii yetu,

Watanzania tulio wengi tunafuatilia mambo ya watu maarufu tukiamini yanatija, kwahiyo mmoja wetu akiwa kiongozi atafanya hayo hayo katika ngazi ya juu zaidi, hawezi kuishia kuwasoma katika magazeti ya sani na ijumaa.

Mtanzania mwenzangu kama wewe una "mental model" tofauti na sisi wengine kwa maana kwamba wakati mwingi unafikiria fursa za biashara, unafikiria namna ya kupata faida, fursa za uwekezaji, unafikiria namna taifa linavyoweza kuondokana na umaskini, unafikiria namna ya kuboresha elimu, afya, ulinzi n.k basi nikupe pole.

nikupe pole kwasababu maisha yako yote hapa Tanzania yatakuwa yakuumia, sisi wengine hatuna mtazamo kama huo wa kifikra, na kwa bahati mbaya kuna wengi wenye mtazamo wetu kuliko wenu kwenye meza ya maamuzi

POLENI ZENU MNAODHANI kutembelewa na wakubwa na kuwatembelea wakubwa hakuna Tija
 
Mkuu hao wanaangalia TV ina maana wameishashiba hao,,, pia naona hapo taa inawaka. Hao watoto wa huku umewaona jinsi utapiamlo ulivyowatafuna?? Unajua nyie watu wa Darisalama mna_overlook sana hii nchi. Sisi huku vijijini ndio tunaoucheza muziki wa maisha magumu na shida za kidunia, mlo mmoja kwa siku. Sio Bush au Jin Ping anayeweza kumfanya jirani yangu Mr Mgonapawene akapata milo miwili, bali kubadili sera zenu za ufisadi kuwa sera za haki sawa na kugawana keki ya taifa. Haiingii akilini wakati Riziwani ni Trilionea baba yake anaomba msaada wa NETI kwa Obama, kwa nini asiombe kwa mwanaye tu...

mbona mnasahau na haya , ambayo ni muhimu kwa maendeleo wasiache kutuletea

Army-captain-Michael-Poto-006.jpg

Army captain Michael Potoczniak marries Todd Saunders at San Francisco's City Hall. Photograph: Marcio Jose Sanchez/AP
 
Sio Jin Ping wala Obama watakaokusaidia kuondoa hizi aibu....
View attachment 100528
View attachment 100529

African problems needs African solutions....
matatizo ya Mi ccm ni kwamba wamefikia ukomo wa kufikiria..nini wafanye ili watoke walipo .sasa jambo la kusikitisha ni kwamba wabunge wote wanalalamika ooh wananchi hawana maji hawana umeme bila kujali professional zao wapo madakitari wazamifu. wa fani mbali mfano maprof,mainjinia.baadala ya wao kuibana serikalli ili serikali iweze kuwajibika kwa wananchi wake,unasikia wanafanya kazi za mawaziri kujibu hoja,au kutetea hoja za moto kwao .utasikia wanalalamika mwisho wa naunga hoja 100% this implies udaifu ambao tunauona katika serekali ..my comment kumsaidia rais ni kuonyesha udhaifu wa sehemu mbalimbali penye mianya kama ya rushwa na mengine.hususani kaitka kipindi hiki allocations of cash ya wizara mbalimbali zinapewa hela, kiundwe kikundi kazi cha kufuatilia matumizi na mapato ktk sehemu mbali-mbali kama T.r.a...........Bandari.na sehemu mbali mbali zenye vyanzovya vipato kama kwenye majeshi yetu, kuna miradi mingi km vile suma jkt na magereza..wakifanyia hivi watatusaidia nakuacha kutoa ngonjera za kila cku..or kilimo kwanza,kasi mpya,tumeweza..sasa naona tena slogan zinazidi mpaka za kithungu.power africa sasa sipati picha what next kesho..
 
Mkuu naona unajiexpose kwa mambo ambayo huya jui kabisa.
Waleta siasa kwenye mambo ambayo kwako ni sawa na mbingu.

Swala la umeme ni watu wa uelewa wa chekechea kama ulivyo ndio wanaolielezea so simply.
Najua kwako ni lazima darasa ni mgogoro.

Sasa hebu tukupe elimu ya awali katika suala uliloliongelea la umeme.
Umeme kabla ya kumfikia mlaji(consumer) una sehemu kuu tatu.
Sehemu ya kwanza ni production-kinu cha kufua umeme iwe ni maji, jenereta au hata wa jua
Sehemu ya pili ni usafirishaji umeme huo, kwa msongo mkubwa(High tension)
Sehemu ya tatu ndio distribution unayoiona wewe Bramo mlalahoi na wenzagu wengi tu.Na hapa ndio tuna umeme mdogo wa majumbani(Low tension)

Sehemu ambayo Bramo anailalamikia huko Tanesco hi hiyo ya tatu, bila kujua hizo sehemu kuu mbili zinaendeleaje.

Hao wawekezaji wa China na Marekani wanakuja kutatua tatizo la kuongeza uzalishaji kwenye vinu mbadala, na hapo ndo watanzania kama Bramo ni lazima walielewe hilo.

Huwezi Kufananisha uelewa wako na wangu katika Eneo la Electrical Power.

Ok, Ngoja Nikupe Darasa la Ki Handisi Zaid.

Production

So Far Main Sources ni Maji (Hydro Electric Power) Hivi Jiulize Tuna Vyanzo Vingapi Vipya tumeshajenga Tokea Mkoloni

Transimmision

Hapa ni Miundo Mbinu Kutoka Production Plants Kwenda Sehemu Mbali Mbali kwenye Substations.
Jiulize tokea Mkoloni Hadi Leo, Serikali imeshatengeneza Transimission Lines Ngapi Mpya??????????????????

Access

Hapa Ndipo Watu wengi wana pa feel.
Hapa ni Mteja anapounganishwa na Network ya Tanesco, Hapa Kuna Urasimu wa Kipumbavu sana
Hii inafana na Kipindi kile cha TTCL Peke yake, ukitaka kufungiwa Simu Mpaka ukalambe watu Miguu Tanesco.
Hebu Jiulize nani anawafuata tena TTCL Kwa Sasa
Next time usithubutu Kuhoji uelewa wangu katika Suala lolote Coz ku fananisha uwezo wangu na wako wa Ku elewa Mambo ni sawa na Kufananisha Tembo na Sisimizi
 
Hivi kwa nini watu mnaona kama vile ni mafanikio kutembelewa na hao marais?

I just don't get it.
Nyani Ngabu, kama unakumbuka kwenye 2010 General Election CCM, waliweka sign boards karibu nchi nzima, wakimwonyesha Kikwete na viongozi mbali mbali wa Marekani waliotembelea Tanzania mfano George W. Bush...hivyo ujue hiyo ni ASSET ya CCM kwenye 2015 General Election, tutaona mengi mkuu!!
 
he he he he he he mi napita tu aisee....he he he eh he he he he he
 
Nina haki ya kufanya hivyo na sina sababu ya kusubiri hadi 2015 kutoa maoni yangu. Jamaa aliingia madarakani akiitwa chaguo la Mungu, Mkombozi wa Watanzania sasa anaondoka madarakani akiwa na majina yenye negative connotation kama DHAIFU, VASCO DA GAMA, MSANII n.k. na hayo yote hayakutungwa na BAK kama hizo fursa zingekuwa zinapatikana kwa Watanzania basi kule Mtwara na maeneo mengine nchini yenye rasilimali chungu nzima kusingetokea machafuko yaliyosababisha mali kuchomwa moto, wengine kupigwa na kutiwa vilema vya maisha na wengine wengi kupoteza maisha. FUNGUA MACHO Ndugu uone jinsi Serikali hii ilivyo dhalimu usikubali tu uongo wao wanaoueneza kila siku huku hali za Watanzania wengi kimaisha zikizidi kudidimia.

BAK mbona UNABWEKA mno!
Unashauriwa kuwaondoa hao waliosaini mikatanba unayoisema kwa kura yako ifikapo 2015.
Na ikiwezekana kwa vile una usongo gombea kabisa uwakwide kule bungeni ili kieleweke.

Wakati huo huo bado wewe kama BAK angalia mfukoni kwako kama kumenona na ujue jinsi ya kuchukua fursa zilizopo kujiendeleza kiuchumi.
 
Mleta maada ... Elewa kua Obama na huyo jing china hawajaleta msaada. Wamesign mkataba na tunaelezwa tu kua tutanufaika japo wanaoleta hizi fedha hatuelezwi watanufaikaje maana huu ni mkataba. Hatujawahi kuwa na win-win mkataba na hawa watu wa nje...may b mleta maada hakai Tz. Wake up people!!!
 
mbona mnasahau na haya , ambayo ni muhimu kwa maendeleo wasiache kutuletea

Army-captain-Michael-Poto-006.jpg

Army captain Michael Potoczniak marries Todd Saunders at San Francisco's City Hall. Photograph: Marcio Jose Sanchez/AP
Mkuu wakati watu wanawania fursa za uwekezaji toka Marekani wewe wawazia uliberali?

Kama umejikita huko huna haja ya kwenda mbali, ni hapo Mchambawima tu.
 
Huwezi Kufananisha uelewa wako na wangu katika Eneo la Electrical Power.

Ok, Ngoja Nikupe Darasa la Ki Handisi Zaid.

Production

So Far Main Sources ni Maji (Hydro Electric Power) Hivi Jiulize Tuna Vyanzo Vingapi Vipya tumeshajenga Tokea Mkoloni

Transimmision

Hapa ni Miundo Mbinu Kutoka Production Plants Kwenda Sehemu Mbali Mbali kwenye Substations.
Jiulize tokea Mkoloni Hadi Leo, Serikali imeshatengeneza Transimission Lines Ngapi Mpya??????????????????

Access

Hapa Ndipo Watu wengi wana pa feel.
Hapa ni Mteja anapounganishwa na Network ya Tanesco, Hapa Kuna Urasimu wa Kipumbavu sana
Hii inafana na Kipindi kile cha TTCL Peke yake, ukitaka kufungiwa Simu Mpaka ukalambe watu Miguu Tanesco.
Hebu Jiulize nani anawafuata tena TTCL Kwa Sasa
Next time usithubutu Kuhoji uelewa wangu katika Suala lolote Coz ku fananisha uwezo wangu na wako wa Ku elewa Mambo ni sawa na Kufananisha Tembo na Sisimizi

Nakupongeza kwa kufanya juhudi ya ku google info na kujielewesha katika masuala ya power production/transmission/distribution, vijana mna akili lmpo wengi ila hamzitumii kujinuafaisha.

Mngekuwa mnajituma kutafuta kipato kama mnavogoogle basi tungepata middle class yenye uelewa.
Tatizo wote mnafikiri siasa ni kipato.

Sasa hebu endelea kugoogle ili ujue main production power plants (Kidatu ,Mtera,Nyumba ya Mungu)na zilijengwa wakati gani na si mkoloni kama ambavyo vyama vyenu vya kitoto vinawaaminisha
 
JK asiuze nchi tu atuuze na sisi tuliomo, maana akiuza nchi peke yake sisi tutaenda wapi?
 
Kikolo, kuna kitu kama watanzania tunashindwa kuelewa, sometimes back hao economic giants walikuwa wanaenda saan tiger countries, kisa ni opportunities, cha kuzingatia hapa we should make sure we stick on a win - win situation, otherwise tutakuwa looses1 Afu nkamu, DRC Hawana madini kama Tanzania, hujajua vitu vingi saana ndugu, ask the germans watakujuvya, Sisi ni nchi inayoongoza kwa madini Africa! Everything is here pal, hujajua tuu!

Kikolo , angalia vizuri mada yangu na msisitizo wake.
Watu wengi ni wavivu, hata wa kufikiri.
Msisitizo wangu ulikuwa mtu kunufaika binafsi na uwekezaji huo.
Ingekuwa mtihani karibu woote wangetupwa nje, maana wako off point.

Uchumi unaanzia kukua kutokana na kipato cha mtu binafsi, uwekezaji wa nchi ni kuchochea tu fursa za uwekezaji wa wananchi. Tatizo kubwa ni mental orientation ya watu wengi kufikiri serikali iko pale kuwajaza mapesa.

Mnaowachagua wanajijaza mapesa kwanza mifukoni mwao na hata wakiondolewa hilo halikujazi mwananchi maendeleo na mapesa bila wewe mwenyewe kujibidiisha.
 
Hivi kwa nini watu mnaona kama vile ni mafanikio kutembelewa na hao marais?

I just don't get it.

Kuna case ya kusema kwamba "nyumba ianayopata wageni ni nyumba yenye baraka". Na watu wanaotaka Tanzania iwe influential wataona kutembelewa na jumbe kubwa hizi ni kuipaisha nchi kimataifa. Kama kungekuwa na ranking za ushawishi wa nchi/ viongozi kama zile rankings za mpira za FIFA, basi Tanzania mwaka huu ingepanda kwa kuweza kupata ugeni kutoka mataifa makubwa.

Kuna watu watasema ni mafanikio kwa sababu badala ya Kikwete kwenda cap in hand Marekani, Wamarekani wamekuja kutafuta deals (arguably really kutoa misaada) Tanzania.

Kwa hiyo siwezi ku dismiss outright kwamba jumbe hizi hazina maana. Kuna wafanyabiashara wame sign deals, kuna mradi wa umeme unapata dola bilioni saba, kuna exposure ya nchi tu (kuna watu wamesikia Obama alitaka kwenda safari Mikumi huko, watataka kwenda na wao, good publicity) etc.

Nisichopenda ni hii over emphasis ya kuona kwamba matatizo yetu yatatatuliwa na watu wa nje. Kumfanya Obama kama mfanya miujiza fulani hivi. Nimeangalia hii attitude hata rais Kikwete anayo, halafu anai embrace openly, bila aibu wala any presidential dignity. Hata masikini anatakiwa kuwa na dignity fulani, Nyerere agreed. Kikwete anashadadia misaada kama chickenhead asiye na confidence in her abilities anavyoshabikia voucher, inatia aibu. Hata Obama naona alikuwa embarassed na attitude hii ya Kikwete ambayo inaweka question mark kwenye hii rhetoric nzima ya "trade not aid". Inaonekana kuwa rais Kikwete alianza kuongea kwa kushabikia misaada sana, kabla ya kuweka context kwamba misaada hii itasaidia ku propel development kwa kuunganisha "the food basket" regions of Tanzania. Naona hata yeye mwenyewe alijishtukia kwamba amekuwa giddy like a chickenhead taken expensive shoppin unexpectedly.
 
Naona mkuu dhana nzima ya maendeleo hauijui. Serikali yako imeshindwa kuweka infrastructure za maendeleo, huku vijijini kupeleka mazao sokoni mjini Ni ndoto tunangojea walanguzi waje kutunyonya. Elimu mnayotupa ndio hiyo ya shule za kata, mtambo WA ziro. Unategemea zero utanipa mbinu za kupata Milo mitatu? Unategemea vitabu alivyoomba JK kwa Obama Jana, tena bila aibu, huku akidanganya takwimu ndio viondoe umaskini WA mtanzania wa kujijini? JK aache uvivu akusanye kodi, mfano mdogo Tu ukienda pale Mlimani City duka la Game unapewa risiti za EFD then pembeni yake kwa rafiki ya JK Home Shopping Center hata risiti hawatoi, ukidai wanakupa za vitabuni kukwepa kodi, badala ya kuwabana hawa mpate hela za vitabu mnaomba kwa Obama, aibu at its best

Mheshimiwa unatia aibu kwa uwezo mdogo wa kujiamini.
Hebu tuchambue mawazo yako........

Serikali yako imeshindwa kuweka infrastructure za maendeleo,

Infrastructure zinazojengwa sasakwa maana ya barabara naona bado hujaziona....

huku vijijini kupeleka mazao sokoni mjini ,Ni ndoto tunangojea walanguzi waje kutunyonya.

Sasa hizi ndio fursa zinazoongelewa, hata kununua fuso au pikipiki ya gurudumu tatu imekuwa nongwa?.....

Elimu mnayotupa ndio hiyo ya shule za kata, mtambo WA ziro. Unategemea zero utanipa mbinu za kupata Milo mitatu?

Mkuu wewe ukiwa msomi inabidi uelewe kuwa kwa leo usizae watoto wengi ambayo utashindwa kuwalea na kuwasomesha.Usitegemee kodi ya mtu ikutunze we kazi yako kuzaa tu. Sitegemei mkulima alielewe hili lakini sio wewe

Unategemea vitabu alivyoomba JK kwa Obama Jana, tena bila aibu, huku akidanganya takwimu ndio viondoe umaskini WA mtanzania wa kujijini?

Halafu unalalamika kuwa shule za kata ni ziro, ukoje wewe?

JK aache uvivu akusanye kodi, mfano mdogo Tu ukienda pale Mlimani City duka la Game unapewa risiti za EFD then pembeni yake kwa rafiki ya JK Home Shopping Center hata risiti hawatoi, ukidai wanakupa za vitabuni kukwepa kodi, badala ya kuwabana hawa mpate hela za vitabu mnaomba kwa Obama, aibu at its best

Hapa ndio nasema wewe kweli ni kama kijana wa mtaani tu asiyesoma, ukidai risiti na duka likashindwa kukupa unaweza kuwashitaki hata wewe je unajua hilo?
Tatizo ni uvivu wa kujisaidia na hata kufikiri, na kuwekeza matumaini katika kuomboleza na kulalama daima dumu.
 
Hivi kweli Tanzania Tumeshindwa Kabisa Katika Suala la Umeme hadi Obama aje kutoka Marekani kuja Kusambza Umeme hadi Vijijini??????
Hivi umeshawahi kwenda Tanesco Kuomba Kuunganishwa kwenye Network ya Umeme wa Tanesco ukaona jinsi unavyopigwa Dana Dana na Kuombwa utoe Rushwa ya Nguzo??????
Haya yote Serikali imeshindwa kuya Handle Mpaka kuwangoja China na Marekani ndo waje Kututatulia Haya.
Nashuku Kichwa cha Mleta Mada kimejawa na Ushabiki wa Kimbeya pamoja na Matope

pia pamoja na rasilimali tulizonazo bado hata kuwafanyia tohara wananchi tunasubiri msaada kutoka kwa watu wa marekani
 
Kuna case ya kusema kwamba "nyumba ianayopata wageni ni nyumba yenye baraka". Na watu wanaotaka Tanzania iwe influential wataona kutembelewa na jumbe kubwa hizi ni kuipaisha nchi kimataifa. Kama kungekuwa na ranking za ushawishi wa nchi/ viongozi kama zile rankings za mpira za FIFA, basi Tanzania mwaka huu ingepanda kwa kuweza kupata ugeni kutoka mataifa makubwa.

Kutembelewa na wageni ni jambo zuri. Ni jambo linaloonyesha kwamba una mahusiano mazuri na watu - ambacho siyo kitu kibaya hata kidogo. Kinachonikera mimi ni ile hali ya kuchukulia kutembelewa huko (hususan na marais wa Marekani) kama neema au mafanikio fulani hivi. Kuanzia raia wa kawaida hadi rais wao ni kama wote wamepatwa na kiwewe. Inasikitisha.

Kuna watu watasema ni mafanikio kwa sababu badala ya Kikwete kwenda cap in hand Marekani, Wamarekani wamekuja kutafuta deals (arguably really kutoa misaada) Tanzania.

Kwangu yatakuwa ni mafanikio kama nitabahatika kuyaona matokeo yake yenye manufaa kwa wananchi wa kawaida kama wale waliokuwa wanakimbilia mabarabarani kwenda kulitia machoni Beast la POTUS.

Kwa hiyo siwezi ku dismiss outright kwamba jumbe hizi hazina maana.

Yawezekana kweli hizi visits zina maana lakini mimi kwa kweli mpaka sasa sijaona visit yoyote ile, iwe ya Clinton ama Bush, kwa mfano, iliyoleta mabadiliko ya kweli mashinani. Wanakuja na mbwembwe zao halafu hao wanarudi kwao na kutuachia gumzo tu.

Kuna wafanyabiashara wame sign deals, kuna mradi wa umeme unapata dola bilioni saba, kuna exposure ya nchi tu (kuna watu wamesikia Obama alitaka kwenda safari Mikumi huko, watataka kwenda na wao, good publicity) etc.

Sawa, hayo yote ni mazuri. Tusubiri matokeo yake sasa. Ila, hiyo ya dola bilioni 7 ni kwa Tanzania tu au ni kwa nchi kadhaa?

Nisichopenda ni hii over emphasis ya kuona kwamba matatizo yetu yatatatuliwa na watu wa nje. Kumfanya Obama kama mfanya miujiza fulani hivi. Nimeangalia hii attitude hata rais Kikwete anayo, halafu anai embrace openly, bila aibu wala any presidential dignity. Hata masikini anatakiwa kuwa na dignity fulani, Nyerere agreed. Kikwete anashadadia misaada kama chickenhead asiye na confidence in her abilities anavyoshabikia voucher, inatia aibu. Hata Obama naona alikuwa embarassed na attitude hii ya Kikwete ambayo inaweka question mark kwenye hii rhetoric nzima ya "trade not aid". Inaonekana kuwa rais Kikwete alianza kuongea kwa kushabikia misaada sana, kabla ya kuweka context kwamba misaada hii itasaidia ku propel development kwa kuunganisha "the food basket" regions of Tanzania. Naona hata yeye mwenyewe alijishtukia kwamba amekuwa giddy like a chickenhead taken expensive shoppin unexpectedly.

Kuna mwandishi mmoja aliuliza swali kama misaada inayotolewa na Marekani inatosha. Kama sikosei aliulizwa Obama na Kikwete naye akalijibu akasema kwamba kama akisema inatosha basi Rais Obama hatamsikiliza tena kuhusu maombi yake mengine. Nadhani ndicho hicho unachokizungumzia wewe. Ni aibu. Yaani ni kama vile anaamini (yeye rais pamoja na watu wengine) kwamba bila misaada hatuwezi kupiga hatua ya kwenda mbele kiuchumi. Jambo ambalo sikubaliani nalo kabisa.
 
Right on the money, that was the question I was talking about.

Kikwete pamoja na Mkapa kumsaidia kumpiga msasa kumuweka MOFA miaka kumi na urais miaka nane sasa, na kabla ya hapo miaka nenda rudi kama waziri na naibu waziri, bado hajui kujibu maswali with presidential dignity?

Kama watu wanataka kuturarua ki-Dambisa Moyo si kashawapa bonge la ammunition kwa statement hiyo inayoonyesha thinking yake off the cuff?

Yani mara nyingine unatamani hata usimuangalie mpuuzi huyu kwa sababu he is such an embarassment.

dead-aid-cover-or8.png
 
Back
Top Bottom