Brain drain in Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Brain drain in Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vancomycin, Feb 5, 2011.

 1. V

  Vancomycin Senior Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tatizo la nchi kupoteza wataalamu wake wa kada mbalimbali hasa kwa kuondoka na kwenda kufanya kazi katika nchi nyingine.Hili ni tatizo ambalo lipo duniani kote lakini tatizo hili limekuwa likiziathiri nchi nyingi hasa zilizoko kusini mwa jangwa la sahara hivyo kupelekea nchi hizo kushindwa kupiga hatua katika kujikomboa kiuchumi na kupoteza pesa nyingi katika kuandaa wataalamu wengi ambao watalitumikia taifa.

  Tatizo kwa wengine linaweza lisiwe sawa letu kwa kutegemea mikakati,sera na uzalendo na mengineyo.Hapa kwetu Tanzania tatizo hili ni kubwa na limekuwa likikwamisha maendeleo ya nchi.Licha ya wataalamu wengi kuondoka na kwenda nje ya nchi taifa limekuwa likipoteza wataalamu kwa aina nyingine pia ambapo wataalamu muhimu kama madaktari,walimu na wahandisi wamekuwa wakimezwa na siasa(internal brain drain).Sababu ya kupoteza wataalamu ziko wazi ambapo baadhi yake ni kutafuta maslahi mazuri(green pastures),mazingira ambayo si rafiki yakufanyia kazi,taaluma zingine kutopewa kipaumbele mfano mwalimu wangu Prof(jina limehifadhiwa) ambaye miaka ya 70 aliondoka kwa kukosa sehemu ambapo angetumia taaluma yake ya upasuaji wa moyo na serikali kutokuwa tayari kuanzisha kitengo hicho pale Muhimbili na sababu zinginezo.Pamoja na haya yote tungetarajia watu hawa wanaoishi nje(in the diaspora) wangekuwa basi wanaliingizia taifa fedha za kigeni lakini hali ni tofauti.
  Leo hii serikari inapiga kelele za wataalamu walimu hawaonekani wanaenda kwenye fani nyingine,madaktari wamelundikiwa mzigo kwani uwiano wa daktari na mgonjwa hapa kwetu ni mkubwa tofauti na nch za magharibi ambao ni 1 kwa 500 ambapo kwa takwimu za hapo kabla ya 2008 kwa dar uwiano ulikuwa daktari 1 kwa wagonjwa 50322,bado tunaendelea kuleta wataalamu wa kigeni kwa kushindwa kuwabakiza wataalamu wetu.Tunasafirisha watu kwenda kutibiwa nje ambapo tungeboresha hospitali zetu na kubakiza wataalamu wetu zingehudumia watu wengi.
  Je taifa kuendelea kupoteza wataalamu,fedha za kuwasomesha na za kigeni ambayo inapelekea taifa kushindwa kupiga hatua je ni watanzania kupoteza uzalendo au serikali ina sera mbovu katika kujenga taifa lake?tujadili kwa upana wake pengine zaidi ya swali hili.NAWAKILISHA
   
Loading...