Boys to Men

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,566
814
Huwa napenda sana kuuliza maswali ambayo yana dadavua na kuchambua si historia ya nchi yetu tu bali hata viongozi wetu. Ni vizuri kufahamu ni wapi viongozi wetu walipo toka ili tujue kwa nini wapo walipo sasa na kwa nini wana misimamo waliyo nayo sasa. Kwa nchi za wenzetu mtu ukisha kuwa kiongozi wa kitaifa kuna material nyingi juu ya historia yako kuanzia essay ulizo andika ukiwa chuoni mpaka miswada uliyo pigia kura. Pia wananchi wanakua tayari wana fahamu ni nani rafiki zako wa karibu na wana changiaje kwenye maamuzi yako.

Hivyo basi leo hii ningependa kuuliza kuhusu kikundi cha wanasiasa vijana lililo kuwa liki fahamika kama Boys to Men. Kwa ufahamu wangu mdogo kwenye kundi hili alikuepo raisi Jakaya Kikweter na aliye kuwa waziri mkuu bwana Edward Lowasa (yawezekana wapo na wengine). Kingine ninacho fahamu ni kuwa jina hilo walipewa mwaka 1995 baada ya kuwa wagombea wadogo zaidi kwenye kinyanganyiro cha kumrithi Mwinyi. Naweza nikawa nime kosea ila ndicho ninacho fahamu kwa sasa.

Swali langu ni je uhusiano wa kisiasa wa Kikwete na Lowasa umeanzia 1995 au kabla ya hapo? Je ni wakina nani wengine walio kuwa nyuma ya hiki kikundi? Kwa maana kwenye kila kikundi kuna wale visible personalities na wale nyuma ya pazia. Je kikundi cha Boys to Men ndicho kilicho kuja kuzaa "Mtandao"?

Kama kijana mdogo ningependa sana kuelewa swala hili ili kuelewa zaidi kwa nini tupo hapa tulipo iwe kwa uzuri au ubaya.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Top Bottom