Boyfriend wangu ni mchafu sana

Boyfriend wangu ni mchafu sana

mwanaume na mwanamke ni ngumu sana kubadilishwa tabia na mzaziwake au mtu yeyote isipokuwa ni kwa mpenzi tu anayempenda tu.kama kweli anakupenda wewe ndio una nafasi kubwa ya kumbadilisha
Mapenzi ya suku hizi bora huyo ni bora kwa huyo kasoro zinazobadilika kuliko ukutane na tabia zisizovumilika
 
Najua mtanitukana na kunisema eti ni kazi ya mwanamke kumuweka mwanaume sawa lakini hapa nimenyanyua mikono, isiwe kesi bora tuachane tu.
Nimekua katika haya mahusiano mwezi wa 8 sasa, mwanzoni nilikua sijamuelewa sana huyu jamaa na tabia yake lakini yamenifika kooni.
I'm not the cleanest person lakini huyu mwanaume ni mchafu jaman. Akioga usiku kabla ya kulala asubuhi haogi. Hata kama nikimsema yani analala na mwanamke usiku asubuhi anaenda kazini hivyo hivyo. Chumba chake ndo kichafu usiseme. Kuna wakati nilisafiri nikaenda mkoa mwingine kama mwezi hivi kurudi chumba hakitamaniki. Nikaona isiwe shida nikamsafishia. Ikawa kila weekend nikienda nasafisha. Nilipata ugeni sikuweza kwenda kwake kwa takribani wiki mbili, mungu wangu siku nilioenda ni kama pamepigwa bomu! Sahani aliolia chakula siku kama 3 zilizopita zipo humo, machupa ya maji, maganda ya ndizi. Hapo kitandani ndo usiseme. Ana jiko na sebule lakini viombo vimejaa chumbani. Yani nikaona hii ni tabia yake.

I can't do this anymore. I'm like his house girl.hata mama hamlei mtoto wake hivi.Mwanaume haambiliki. Nikishauri ajitahidi usafi anasema nampanda kichwani( Male ego).
Sijaenda kwake wiki sasa I know nikienda huko huo uchafu ntakaokutana nao sina hamu.
He's a good guy lakini hii tabia yake imenishinda. Bora yaishe tu.

Kina dada mnaishije na hawa viumbe?. Huyu kanishinda
Sasa kama haogi si atakuwa ananuka sana kama beberu? Wanawake mna kazi sana.
 
Mnataka nini sasa mbona wangu alienda nitangaza kuwa ni msafi kupitiliza?_
 
Hahahahahahaahahahaha umenchekesha..

Eti chumba kama kimepigwa na bomu... hahahaha

We mdada unavituko

Usafi ni tabia inayotengenezwa, wazazi tunajukumu la kukuza watoto. Usimlaumu sana huyo jamaa.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 uwanja wa vita
 
Back
Top Bottom