Boyfriend anataka wanunue kiwanja cha pamoja

angelita

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2013
Posts
3,017
Reaction score
2,445
Habari wapendwa....!

Nina rafiki yangu wa kike, ana boyfriend wake anampenda sana na kaahidiwa ndoa, wiki mbili zilizopita bwana akamwambia bidada, wanunue kiwanja kila mmoja atoe hela nusu ya inayotakiwa, bidada akakubali.

Jana ndo ilikuwa siku waliyokubaliana kwenda kununua hicho kiwanja, akaja kuniomba ushauri, nikamuuliza hiko kiwanja kinaandikaa jina la nani, akajibu la mwanaume, nikamwambia usithubutu mngekuwa wanandoa sawa, lakini wapenzi hapana, Je, mkiachana itakuwaje? Bidada anahaha bwana anampenda hataki kumuuzi wala kumpoteza, anawaza atamfikishiaje bwana habari kwamba hayuko tayari akamwelewa?
 
Mkataba waandike.majina yote wakishaoana wataanza mchakato wa hati kwa majina yote!!!!!!

Ila hiyo share awe tayari kuendelea nayo mpaka mwisho yaani kama nyumba ni 80M basi aandae hiyo 40M kabisa siyo kudai mwanzo halafu kwenye ujenzi ajidai yeye atashughulikia mambo ya nyumbani!!!!!
 
Na wasipooana itakuwaje?
 
Atali kilio cha mbwa mwizi huyo hajuagi kuachwaaa

habari wapendwa....!

Nina rafiki yangu wa kike, ana boyfriend wake anampenda sana na kaahidiwa ndoa, wiki mbili zilizopita bwana akamwambia bidada, wanunue kiwanja kila mmoja atoe hela nusu ya inayotakiwa, bidada akakubali.

Jana ndo ilikuwa siku waliyokubaliana kwenda kununua hicho kiwanja, akaja kuniomba ushauri, nikamuuliza hiko kiwanja kinaandikaa jina la nani, akajibu la mwanaume, nikamwambia usithubutu mngekuwa wanandoa sawa, lakini wapenzi hapana, je, mkiachana itakuwaje? Bidada anahaha bwana anampenda hataki kumuuzi wala kumpoteza, anawaza atamfikishiaje bwana habari kwamba hayuko tayari akamwelewa?
 
Asara tupu,yani kumwambia kua sina hela ua siwezi kununua kiwanja sababu wewe sio mumewangu pia inakua ngumu?
Hajiamini au? watu wengine jamani mie shosti achilia mbali mchumba hata mume namwambia bila kificho,asinitie BP isokua yalazima siku akisema basi............
 
ninao ushahidi kwa waliwahi kulizwa kwa style hiyo
sio lazima amwambie kuwa amegairi kuna mbinu nyingi tu za kufanya mojawapo ni pamoja na kutengeneza safari ya gafla then akisharudi kutoka hiyo safari yake amwambie juu ya dharula iliyojitokeza na kwamba hela yote imeishia huko then mapenzi yao yataendelea kama kawaida
ukizingatia hajwahi mdanganya boyfriend wake bila shaka atamwamini tu
 
Honestly, asitoe hiyo pesa. Atakuja kulia kikwao bure. pesa mtoe pamoja, jina aandikwe kidume, mbona majanga! kwa nini asiandikwe bidada? kama bf hamwamini gf wake, kwa nini yeye aaminiwe?

kuna bidada alijipendekeza hivyo hivyo wakiwa wachumba. wakanunua kiwanja kwa jina la mshikaji. baadaye jamaa akaanza kujenga nyumba bila binti kujua. alipokuja shtuka, jamaa ana gf mwingine with serious relationship. the monster monopolised the pieace of land na dada hakuwa na ushahidi wa kudai haki yake!
 
Asara tupu,yani kumwambia kua sina hela ua siwezi kununua kiwanja sababu wewe sio mumewangu pia inakua ngumu?
Hajiamini au? watu wengine jamani mie shosti achilia mbali mchumba hata mume namwambia bila kificho,asinitie BP isokua yalazima siku akisema basi............

Anaogopa kuachwa, kumwambia ukweli bwana atanuna
 
ninao ushahidi kwa waliwahi kulizwa kwa style hiyo
sio lazima amwambie kuwa amegairi kuna mbinu nyingi tu za kufanya mojawapo ni pamoja na kutengeneza safari ya gafla then akisharudi kutoka hiyo safari yake amwambie juu ya dharula iliyojitokeza na kwamba hela yote imeishia huko then mapenzi yao yataendelea kama kawaida
ukizingatia hajwahi mdanganya boyfriend wake bila shaka atamwamini tu

Nimemwambia amwambie alikotegemea kupata hiyo ela imeshindikana, mana kumwambia ukweli hawezi.
 
makubaliano yao tu,wao ndio wanaojua jua jinsi wanavyoshibana na malengo yao.tatizo wadada wa humu jf na wakaka(sio wote ila wengi wao)wamekaa kiwizi wizi tu.muda wote mtu anafikiria kuiba au kuibiwa.ndoa haitokei kama ajali,watu hukaa,huishi,huzungumza na kuelewana ndipo humalizia na ndoa.pengine mkaka wa watu ana uwezo wa kutosha sana kununua viwanja kama hivyo kumi,lakini ameamua kumshirikisha mwenzake ili kila mmoja a feel uzito wa mali wanazotafuta?acheni ushetani
 
Akili kichwani kwake, ushauri nimempa akijifanya kichwa maji atalia na Mungu wake

Good, maadam wewe ushampa ushauri akili kichwani mwake, kweli.

Ila anakamata kaa la moto.

Si mbaya ku share lkn maandikiano ni lazima kwa kila hatua.

Sasa km yeye anafkiri maisha ni mapenzi tu atakuja kuji carry
 
makubaliano yao tu,wao ndio wanaojua jua jinsi wanavyoshibana na malengo yao.tatizo wadada wa humu jf na wakaka(sio wote ila wengi wao)wamekaa kiwizi wizi tu.muda wote mtu anafikiria kuiba au kuibiwa.ndoa haitokei kama ajali,watu hukaa,huishi,huzungumza na kuelewana ndipo humalizia na ndoa.pengine mkaka wa watu ana uwezo wa kutosha sana kununua viwanja kama hivyo kumi,lakini ameamua kumshirikisha mwenzake ili kila mmoja a feel uzito wa mali wanazotafuta?acheni ushetani

Kozooooo....we ndio 'kaka' niniiiii?haaaahaaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom