Mkuu kuna wakati ni busara kukaa kimya.
- Wewe unajua fedha mbovu au zilizo chakaa kiasi gani zimerudishwa BOT?
- Unajua pesa kiasi gani zilifichwa na watu wenyewe wakafa au wapo jela, au zikaharibika, au zilizo ungua kwenye ajali za moto, zilizo zama kwenye mafuriko ajali za meli na vivuko?
- Unajua serikali ina mpango gani wa kuzikusanya fedha hizo za zamani taratibu kwa kuziondoa kwenye mzunguko?
- Unajua inachukua siku ngapi kufanya mabadiliko , kuchapisha fedha na kuzisafirisha toka nje zinako tengenezwa kwenda BOT kisha kwenye mabenki yetu ya kibiashara, maana muda alio andika yule mtu na leo fedha mpya ipo kwenye mzunguko ni muda mfupi sana.
Hizo zote namba 1 na 2 hazipo kwenye mizunguko tena, na anaye fuatilia pesa zilizo kwenye mzunguko ni BOT.
Kuna mengi ya kukufumbua akili lakini kwa sasa niishie hapo.
Ni akili ya ajabu sana kuamini watu wote serikalini, wizara ya fedha, BOT na baraza la mawaziri ni wajinga na wewe ndio pekee una akili nyingi sana.