BoT yakanusha uvumi kuhusu mwisho wa matumizi ya noti ya Sh.500

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
15538411_693315030839365_5166049211237531648_n.jpg


Benki kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa,habari inayoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano haitatumika tena kuanzia Desemba 31,2016.

Sio taarifa ya kweli na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa.

Ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi.

Tafadhali mpuuze taarifa hizo sio za ukweli.

Marcian Kobello.
Mkurugenzi wa Huduma za kibenki- BoT .
 
Chadema wanatutia aibu sana,
Kimekuwa chama cha kutunga uzushi na uongo kila siku.

Na ndio maana walipinga sana sheria ya mtandao kumbe walijua mbeleeni chadema itakuwa chama la kutetea mafisadi na kusambaza uongo kila siku
 
Sasa kama Hawa release noti Mpya za 500, huku Wakina release Sarafu pekee tafsiri Nyepesi unayoipata ni ipi?

Sio Kila Jambo ni lazima likanushwe ama Kutangazwa Hadharani na Idara za "Makunusho" JIONGOZE KUELEWA UHALISIA.
 
Back
Top Bottom