BoT: Watanzania waoga wa Mikopo

BALAGASHIA

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
392
383
Hivi BoT wanajua kweli magumu yaliyopo kwenye kupata mikopo?

MIKOPO.png
 
Bot wana mishahara minono watajuaje kapuku huku ana matatizo ...hawa ni sawa na ccm tu ..
Yaaan hawajui uchumi ukoje sasa hivi ni bora syria kuliko Bongo
 
Utakopaje kama biashara zote zimedolola..utafanya biashara gan itakayoweza kurejesha kila mwezi
 
wapuuzi sana hao wanashindwa kupunguza riba za mikopo kwa mabenki then unasema watanzania waoga kwa mikopo, ndo wasomi wa tanzania hao. wakati kenya riba ni chini ya 10% tanzania mpka 25%
 
Riba 24% . Faida kwenye biashara 10% ukikopa utarudisha vipi? Wanaokopa wanajua hawarudishi washajiandaa, tunaotaka kukopa na kurudisha tukipiga hesabu mkopo haulipiki hatuji!
 
Watu wengi hawajuwi jinsi ya kuandika mpango kazi wa biashara ulio endelevu. Huwezi kwenda benki na Business plan mbovu ukategemea kupewa mkopo. Utafiti ni muhimu.
 
Washushe riba...we....mpaka.. 12..percent...utaona watu watakopa..lakn sasahiv...noma...18 to 24...shida unazeeka kwa kulipa mikopo ya bank.....
 
Watu wengi hawajuwi jinsi ya kuandika mpango kazi wa biashara ulio endelevu. Huwezi kwenda benki na Business plan mbovu ukategemea kupewa mkopo. Utafiti ni muhimu.
Mkuu kwa kuandika hizo wabongo ni mabingwa. Ila kuandika na kufanya biashara ni vitu viwili tofauti ndio wengi hawawezi kurejesha mikopo!
 
Mafisadi hawajui maisha ya mtaani yalivyo, wao wanagawana pesa kwenye magunia na kujikopesha kwa riba nafuu ndio maana wanaongea kirahisi sana.
 
Back
Top Bottom