Benki Kuu ya Tanzania: Hatuuzi dhahabu kufadhili miradi ya Serikali

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,481
Reaction score
14,858
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa ina mpango wa kuuza sehemu ya hifadhi yake ya dhahabu kwa ajili ya kufadhili miradi ya kimkakati ya serikali.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema madai hayo si ya kweli.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa ina mpango w.jpg
Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo.

Kwa mujibu wa Akaro, bodi ya BoT imeidhinisha benki hiyo kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi dola za Marekani bilioni mbili, wakati thamani ya sasa imefikia dola bilioni 3.24, hivyo kutokana na tofauti hiyo, benki inapanga kuuza kiasi kilichozidi kiwango kilichowekwa.

Amefafanua kuwa fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo hayo zitawekezwa katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa lengo la kuongeza mapato ya uwekezaji, na si kwa ajili ya kufadhili miradi ya serikali.

Akaro amesisitiza kuwa BoT ni chombo huru, na uamuzi wowote wa kutumia uwekezaji wake kufadhili miradi ya serikali unahitaji idhini ya Bunge.

Hadi jana Januari 29, 2026, BoT ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni yenye thamani ya dola bilioni 6.52, na kati ya hizo, dhahabu inakadiriwa kuwa dola bilioni 1.2, dola za Marekani bilioni 3.8, na sarafu ya China (yuan) dola milioni 735.

Pia Soma
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa ina mpango wa kuuza sehemu ya hifadhi yake ya dhahabu kwa ajili ya kufadhili miradi ya kimkakati ya serikali.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema madai hayo si ya kweli.

Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo.

Kwa mujibu wa Akaro, bodi ya BoT imeidhinisha benki hiyo kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi dola za Marekani bilioni mbili, wakati thamani ya sasa imefikia dola bilioni 3.24, hivyo kutokana na tofauti hiyo, benki inapanga kuuza kiasi kilichozidi kiwango kilichowekwa.

Pia Soma Tanzania yapanga kuuza sehemu ya Hazina yake ya Dhahabu kusaidia kufadhili miradi ya miundombinu

Wawe wanatoa taarifa kamili kabla wahuni hawajaongeza chumvi zao.

Hata hivyo Kuna sehemu wanasema dhahabu watakayouza pesa zitawekezwa kwenye masoko ya Kimataifa,Kwa nini wasiwekeze kwenye soko letu la ndani?

Pia lengo la kuwekeza hizo pesa linakuwa ni lipi mwisho wa siku?

Mwisho Wizara ya fedha ipeleke mswaada Bungeni kuongeza ceiling ya Hazina ya dhahabu badala ya Kuuza Ili kupata forex
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa ina mpango wa kuuza sehemu ya hifadhi yake ya dhahabu kwa ajili ya kufadhili miradi ya kimkakati ya serikali.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema madai hayo si ya kweli.

Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo.

Kwa mujibu wa Akaro, bodi ya BoT imeidhinisha benki hiyo kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi dola za Marekani bilioni mbili, wakati thamani ya sasa imefikia dola bilioni 3.24, hivyo kutokana na tofauti hiyo, benki inapanga kuuza kiasi kilichozidi kiwango kilichowekwa.

Pia Soma Tanzania yapanga kuuza sehemu ya Hazina yake ya Dhahabu kusaidia kufadhili miradi ya miundombinu

Amefafanua kuwa fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo hayo zitawekezwa katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa lengo la kuongeza mapato ya uwekezaji, na si kwa ajili ya kufadhili miradi ya serikali.

Akaro amesisitiza kuwa BoT ni chombo huru, na uamuzi wowote wa kutumia uwekezaji wake kufadhili miradi ya serikali unahitaji idhini ya Bunge.

Hadi jana Januari 29, 2026, BoT ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni yenye thamani ya dola bilioni 6.52, na kati ya hizo, dhahabu inakadiriwa kuwa dola bilioni 1.2, dola za Marekani bilioni 3.8, na sarafu ya China (yuan) dola milioni 735.
Ndugu ofisa Wadanganye Wajinga wenzio
 
BOT wanaanza siasa

TOKA MAKTABA:

Nov 27, 2025
Gavana Tutuba - Hifadhi ya Dhahabu imehifadhiwa nje ya nchi, na yote ipo huko katika Bank of England Uingereza

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amesema kuwa hadi sasa Benki Kuu imenunua jumla ya tani 15.37 kupitia mpango wake wa ununuzi wa madini hayo, ikiwa ni hatua muhimu ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni na kuimarisha thamani ya shilingi.. na kuwa dhahabu ya BoT imesafirishwa na kuhifadhiwa ktk benki kuu ya Uingereza yaani Bank of England

View: https://m.youtube.com/watch?v=ql7hRR5sA08
Source : Bank of Tanzania
 
Hiyo sheria inataja thamani ya hiyo dhahabu au kiwango cha uzito?

Na ni busara gani hiyo imetumika kuuza dhahabu ambayo thamani yake bado inapanda kwa kasi ili kwenda kuwekeza katika maeneo ambayo yana faida ndogo zaidi na ambayo yana risk kubwa zaidi?

Hawa watu wamesikiliza hotuba ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu wa Canada kule Davos kwenye World Economic Summit?
 
TOKA MAKTABA:

Nov 27, 2025
Gavana Tutuba - Hifadhi ya Dhahabu imehifadhiwa nje ya nchi, na yote ipo huko katika Bank of England Uingereza

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amesema kuwa hadi sasa Benki Kuu imenunua jumla ya tani 15.37 kupitia mpango wake wa ununuzi wa madini hayo, ikiwa ni hatua muhimu ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni na kuimarisha thamani ya shilingi.. na kuwa dhahabu ya BoT imesafirishwa na kuhifadhiwa ktk benki kuu ya Uingereza yaani Bank of England

View: https://m.youtube.com/watch?v=ql7hRR5sA08
Source : Bank of Tanzania

Huyo Gavana vipi tena, anaiita dhahabu ni fedha za kigeni?
 
Back
Top Bottom