Boss mpya, mgao wa maji mara moja kwa mwezi sasa basi?

Boss mpya, mgao wa maji mara moja kwa mwezi sasa basi?

Jahom

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2008
Posts
351
Reaction score
33
Kwa muda mrefu nimekuwa nikisali sana atokee mkombozi wa huduma za maji hapa Dar es Salaam. Inawezekana wakati ni sasa. Sitaki kuamini huyu aliyekuja kuwa Mkuu wa Dawasco hajui maeneo yenye uhaba sugu wa maji na uhaba wenyewe ni wa bandia. Haiwezekani mgao usio na ratiba ndiyo kinachowezekana, wakati mwingine mara moja kwa mwezi wakati mwingine mpaka sikukuu, yaani hata kuweka fomyula ya vigezo vya mgao haiwezekani, labda aje Aristostle. Walau tupe maji lisaa moja kila siku tutashukuru kama vile tumekaribia mbingu.

Badala yake, inaonekana kama kuna makubaliano ya wauza maji wenye magari na visima vyao ili biashara zao ziende. Kwa watumiaji, hata kama una uwezo wa kuhifadhi maji kiasi gani, haiwezekani ukatunza maji hayo bila kujua mgao unaofuata ni lini. Bahati mbaya sana, wahitaji wa maji ni wananchi wa kipato cha chini ambao hawana uwezo hata wa kununua chombo cha hifadhi ya maji cha kubeba lita 100, na ndiyo wanaopewa mgao sikukuu kwa sikukuu. Hapo lazima magonjwa ya matumbo yawepo bila kukoma.

Boss Mpya, inawezekana wewe ndiye tuliokuwa tunakusubiri hasa wakaazi wa Tabata, Kimara, Ubungo, na wengine ambao sijawataja. Umeanza na maji yanayopotea, kuzuia wezi wa maji, n.k. Sasa kumbuka pia kushughulikia wahujumu uchumi ndani ya DAWASCO ambao wanatusababishia shida za bandia kwa kushirikiana na walafi wachache.
 
Huyo Boss mpya ni bomu linalosubiri kupasuka..akimaliza mwaka hapo Dar sijui
 
Jamani naona kuna ushirika kati ya wenye magari ya kuuza maji na DAWASCO.Wauza maji wako bize kila siku lakini maji kwenye mabomba yetu hayatoki.Kulikoni ndugu zangu ?Naomba tujuzane.
 
Back
Top Bottom