Hela ni roho, sasa fahamu roho zina sifa zipi, moja huishi milele, husikia na kukaa na mtu au watu na pia humtoka mtu ....
Hofu yako ndo itakuletea uhalisia wa unachokihofia na ujasiri wako hukuletea na unachokiamini, kumbuka imani ina nguvu kuliko matendo.
Kwa hali ya kawaida tuu, isemeshe hiyo hela ikiwa hapo mezani na iamrishe ikutumikie wewe na isahau maagizo yote iliyopewa toka huko ilikotoka na kuwa kuanzia hapo wewe ndo mmiliki wake maana ni mshahara na uko kwa matamshi ya jina lako. Kisha hapo waweza ichukua kwa kujiamini na kuitumia kwa maarifa na akili. Itume na isemeshe hela ikutumikie sio wewe uitumikie.
Sio ndumba wala kichumio, ndio maana sadaka kule madhabahuni huwa inaombewa na kubarikiwa maana inatolewa kma sadaka lakini imetoka kwa watu wengi mbalimbali.