Boss kazini nyumban mke mwema

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Wakati dunia nzima inaungana kuhakikisha mwanamke anapata haki zote na kupewa kipau mbele katika masuala ya msingi ya maendeleo wapo wanawake wachache ambao huchanganya mambo kwenye ndoa zao.

Ni dhahiri na ni ukweli kwamba wanawake leo katika dunia ya tatu sasa wana elimu, wana kazi zao, na fedha zao na taaluma kitu ambacho ni kizuri na jambo la msingi sana kwa familia yoyote kuwa na mke na mume ambao wote wanachangia pato la familia.

Hata hivyo kwa upande mwingine suala la mahusiano baada ya mke na mume wote kufanya kazi na kuwa na taaluma yake data zinaonesha suala la mahusiano katika ndoa linazidi kuwa gumu na linapelekea ndoa nyingi kwenye ICU au kufa kabisa.

Ni kama vile kutatua tatizo la wanawake kupewa uwezo na haki zao kumetengeneza tatizo jipya kabisa la mahusiano kwa maana kwamba baadhi ya wanawake (siyo wote) anataka akiwa boss kazini basi akirudi nyumbani anataka awe boss pia.

Ndiyo maana baadhi ya wanaume ambao hawajiamini bado hupendelea kuoa mwanamke ambaye elimu yake au kipato chake ni kidogo kuliko wao na huwa wanaamini kwamba wanawake wenye fedha na elimu hupendelea kukalia wanaume zao.

Ukichunguza kwa undani sababu za baadhi ya wanawake ambao wana uwezo kitaaluma na kifedha kuliko waume zao, mwanaume kukaliwa ni suala la mtazamo (attitude). Kwa kuwa kazini ni boss na ana mshahara mkubwa na elimu kubwa kumzidi mume basi huyo mwanamke huamini na nyumbani anatakiwa kuwa juu ya mumewe.

Wanaume hukiri kwamba zamani wanawake walidumu katika ndoa kwa sababu walimtegemea mume kwa kila kitu na baada ya sasa kupewa uwezo wanawake wanabadilika.

“Nina elimu, taaluma na fedha, kwa nini mwanaume anibabaishe”, wapo wanawake wanaoamini hivyo. Ndiyo maana kuachana na idadi ya single moms inaongezeka kila kukicha na inaonekana ni kitu cha kawaida.

Hata hivyo kutokana na tamaduni zetu za kiafrika haijalishi mwanamke una kazi nzuri kiasi gain au fedha nyingi kiasi gain unaotakiwa kumtii na kumpa mume respect anayostahili ili mahusiano yadumu.
Mumeo ni mumeo na nyumba haiwezi kuwa na wanaume wawili.

Uwe boss kazini na uwe mke mwema nyumbani!

 
Mawasiliano ni muhimu sana katika mahusiano, wakikaa na kuongea nini wanapenda na nini wanachukia, kila mtu atafurahia mahusiano kwa nafasi yake
 
Sara alimtii Ibrahimu hata akamwita BWANA, akina mama zingatieni tafadhali kwa uhai wa ndoa zenu.
 
Sara alimtii Ibrahimu hata akamwita BWANA, akina mama zingatieni tafadhali kwa uhai wa ndoa zenu.
waanze kutuita bwana?heshima iwepo kwa wote c kwa mwanamke tu hata wanaume vivyo hivyo,hakuna asiependa kuheshimiwa,sema ni wanawake wachache wanaokuwa na status flani na bado wanakuwa na nidhamu kwa waume zao
 
True.....,
Respect Goes Both Ways..., You Have to Give It to Receive it...

Ingawa kina dada wengine huwa wanakosa nidhamu lakini sometimes kina kaka huwa wanakuwa na Inferiority Complex, wakiambiwa kitu wanadhani wanaambiwa sababu ya dharau au sababu mtu kawazidi....
 
Ongezeni michango tuweze kusoma tuwaelewe vizuri nyie akina mama! Mpooooo humu ndani? Je mnawadharau waume zenu? au mwawapa heshima zenu. Mi wangu ananiheshimu nafikiri kwa sababu maisha yetu si ya juu wala chini.
"Hata misaafu inatuelekeza kuwa wa kiasi"
 
Back
Top Bottom