Habari wadau,
Kuna boss wangu ambaye amekua kama mshauri wangu pia hapa kazini kwetu, yeye ananizidi kama miaka 4 hivi, tumekua karibu sana kwa muda mrefu tukiheshimiana kama kaka na dada, si bosi wangu moja kwa moja bali mmoja wa line managers hapa kwetu
Wakati mama yangu aliponiletea mke kutoka kijjjini kwetu, mshauri wangu mkubwa kwenye sakata hilo alikuwa ni huyu dada, ambapo alinisihi sana nisimkatae huyo binti, nami nimeendelea kukaa na huyu msichana hadi sasa.
Kwa zaidi ya wiki mbili sasa katika mazingira ambayo ni accidental tumejikuta tumeanzisha uhusiano wa kirafiki na huyu dada wa kazini, ameniita kwake mara kadhaa, amenipikia chakula kizuri, na tukapumzikia hapo hapo kwake mara kadhaa, sasa ameniomba nihamie kwake tufanye maisha pamoja, kwa kweli yupo vizuri sana kiuchumi, aliachiwa nyumba kubwa wakati wa kugawana mali na mumewe na alipata mali nyingi, juzi tu aliniomba nipitie hesabu kwenye moja ya biashara zake, karibu 3 million.
Ana watoto wawili na ni mzuri kwa kweli, ningekuwa nimeshahamia kwa huyu boss wangu lakini shida huyu mwanamke wangu ambae mama alimleta amegoma kuondoka kwangu na kudai haendi kokote eti mimi ni mumewe, sijui majirani wamemshika masikio au, sielewi, juzi nilimdanganya aende nyumbani kwa ajili ya pasaka akashtuka akagoma.
Sasa wadau mlikua mnanishaurije katika suala hili?
Au nihamie tu kule kwingine nimuache tu yule pale nyumbani kodi ya nyumba ikiisha ataondoka mwenyewe, maana mama yangu hataki kusikia namrudisha, nikianzisha mada hiyo tunakua hatuelewani kabisa.
Yule bosi wangu ana mavumba, naweza kutokea hapo, na ananipenda kwa dhati.
Help please