Nini hiki mbona sielewi??Shost ameolewa na watoto wanne, anafanya kazi katika mradi wa mmoja wa jamii mjini. Story iko hivi yeye ni among seniors kwenye mradi, head wake ni professor lakini yule baba amepata mental health issues.
Kazi hawezi kufanya tena, haongei na mtu, haongei hata neno moja, yeye hukaa na kalamu na daftari, sasa kuna anayoandika kwenye daftari kutwa nzima akikaa. Madaktari wanaomtibu walitaka wajue anaandikaga nini. Cha ajabu huwa anarudia kuandika jina la shost tena la kimila ambalo hata mume wake halifahamu.
Hali hii inamkosesha shost raha sana, ananiambia walizoeana kama colleagues, na lile jina aliliona kwenye document za shost kiofisi. Jamani yaani huyu baba ndiyo amelishika hilo jina.
labda wa mwisho kukutana nae kabla hajapata huo ugonjwa alikuwa shosti yako imebaki kwenye memory card yake hapo shosti analo tena jina la nyumbani eeeehhh marefu hapo
Ni hali ngumu fikiria na mke wa professor atakuwa anafikiria nini sasa? Lakini wamefocuss kuuguza.
Mmmmm mbaya hiyo,boss wangu alikosea kumuita jina mkewe akamuita jina langu kimakosa mbona mke alikuja kunitafuta
kazini eti nimweleze why mumewe kaniita jina langu,alinitukana mpaka alipo maliza akaondoka,sikumjibu manake mumewe nilikua namuheshimu sana na pia nilikua nakwenda kusoma sasa sikutaka kisirani cha kitu kizima, so mwambie shosti wako wala asijitie BP hutokea...
Mpe tahadhari asijaribu kwenda kutafuta solution kwa kina MANYAUNYAU,KAMCHAPE,KALUMANZIRA NA KINA BABU WENGINE WASHIRIKINA sababu itakula NGUONI KWAKE,HALAFU ASALI YOOOTE KWISHNEY.Shost ni msoma masomo J2. Atatuchanganya, yaani hii ni kali kuliko.