Bosco Ntaganda aanza kula baada ya kugoma wiki mbili ICC

Bosco Ntaganda aanza kula baada ya kugoma wiki mbili ICC

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,086
Reaction score
34,883
_91323785_d06a631f-8e0e-4af6-9655-1282633203c6.jpg

Kiongozi wa zamani wa waasi DRC anakabiliwa na mashtaka 18
Aliyekuwa kiongozi wa waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda ameanza kula baada ya kugoma kwa takriban wiki mbili katika kizuizi chake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhaini huko Hague, Shirika la AFP linaripoti..

Anakakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita.

Amepewa jina la utani "The Terminator" kutokana na shughuli zake Congo, Ntaganda aligoma kula kulalamika dhidi ya hali inayomkabili kizuizini, ikiwemo kuhusu suala la kutembelewa na familia yake.

AFP imemnukuu wakili wake Stephane Bourgon aliyesema kwamba ameanza tena kula.

Ameongeza:

''Iwapo kila kitu kitakwenda sawa, mkewe atafika The Hague kuanzia Alhamisi na ataweza kumuona bwana Ntaganda kwa kiwango fulani cha faragha, kitakachokidhi matarajio yake."

Mwaka jana, Ntaganda alikana mashtaka 18 yanayomkabili - ikiwemo mauaji, kuwasijili watoto katika jeshi na kuwatumia wanawake kama watumwa wa ngono.
chanzo.BBC
 
Alikua analiombea taifa la Congo kwa njia ya kufunga na kuomba. Hakuwa amegoma kula
 
huyu jamaa kwel terminator yan kagoma wiki mbilo kula hadi jamaa wamesalim amr...huyu ndo mwanaume sio yule jamaa wetu wa pale arusha alietaka kukata roho baada ya kususa kula kwa siku moja tuu....hahahahaha
 
Kuna Nyumbu siku zote wanadhani ICC ipo kwa ajili ya Viongozi wa kiserikali hata Wapinzani inawezekana kutupwa ICC.
Bosco Ntaganda alikuwa Ndie Mbowe wa DRC lakini yupo Lupango ICC na Joseph Kabila anakula Kima tu Kinshasa!
 
Ah ah ah ah ah
 
Hahahhahahahahaaahahahahahahahahhaha...!.Daah! Nasikia harufu ya uChama hapa.
 
Kuna Nyumbu siku zote wanadhani ICC ipo kwa ajili ya Viongozi wa kiserikali hata Wapinzani inawezekana kutupwa ICC.
Bosco Ntaganda alikuwa Ndie Mbowe wa DRC lakini yupo Lupango ICC na Joseph Kabila anakula Kima tu Kinshasa!
naona chadema inakuwasha dada
 
Back
Top Bottom