Grader
JF-Expert Member
- Feb 23, 2009
- 445
- 65
Nipo dar group tangu saa sita mchana, nilibahatika kuonana na daktar majira ya saa saba hivi ndipo alipomwambia mtoto Wangu akachukuliwe vipimo vya damu,mkonjo na ultra sound. Hapo Maabara nimekuta umati wa watu wakisubiri kuhudumiwa na malaboratory technician wapo ndani walichokuwa wanafanya sijui, nimesubiri sana hadi ambapo dada mmoja alipokwenda kulalamika ndipo wakaanza kazi. Sasa kasheshe huku ultra sound foleni ni ndefu na muhudumu amekimbia eti kisingizio Umeme hakuna hali ambapo majengo yote upo. Tukamfuata daktari mmoja akampigia simu akamjibu ameondoka nyumbani ya kuwa amechoka. Hili picha nimefuatilia kwani mwanangu siku moja alisema ukiwa mgonjwa serious hospital ya dar group utakufa kwenye foleni. Walengwa hamtaki kufanya kazi, au ndiyo tabia za watanzania wanataka hela ila kazi ni kuzurura ili mud a ufike.