Bora Shoes - what happened?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,447
39,857
Hivi kuna mtu anakumbuka what happened to kiwanda hiki. Kiliweza kurudi kwenye uzalishaji tena?
 
Mkuu sasa hivi ni godown la huyo mwekezaji kwa mali zake anazoagiza !
 
Kilichokuwa 'Kiwanda cha Viatu (BORA)' kilibinafsishwa mid 90's. Wahindi waliokinunua kwa bei ya kutupa hawajawahi kutengeneza viatu toka enzi hizo, in fact mashine zote za kutengenezea viatu ziliuzwa kama scrap.
Hata hivyo, line za kutengeneza kandambili na tairi na tyubu za baisikeli ziliendelea kufanya kazi na bila shaka ziliimarishwa kwa kuwa uzalishaji uliongezeka na mauzo yanafanyika mpaka nchi za jirani (source: TRA).
 
aisee nakimbuka zile raba zao za akinamama... zilikuwa za kijani!!! nikuwa ndogo sana mm ila nakumbuka sana mavitu yao!!!!!

sasa hivi wanatengeneza viatu vya ngozi vizivyo na finishing nzuri sio kama zamani!! SI amesema tunasonga nyuma!!!

hapa tanga kuna duka la viatu vya Bora!!! limefunguliwa karibuni... inaonakana uzalishaji unendelea!!
 
Nyway sio jibu la hoja,lakini hapa mkuu umenikumbusha moro shoe,walikuja vizuri na bidhaa bora kuliko za bora shoe..nao sijui walifia wapi?
 
BORA..
Kila kitu kiliuzwa kwa bei ya kutupa kwa wahindi japo ilikua pesa kubwa kwa waliokua wafanyakazi kwa kua ilitakiwa kulipa kwa mkupuo.
Jamani Bora...
Nimekumbuka mengi hadi najisikia kulia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom