Bora nitawale mimi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bora nitawale mimi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Think, Aug 7, 2012.

 1. Think

  Think Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je wewe hupendi kuwa kiongozi? je wewe hupendi kuwa mzalendo?

  Nionavyo mimi tanzania tuliyonayo inapelekwa kihuni na watu wachache wenye uchu wa madaraka na ulafi wa fedha za umma huku wanaotawalwa wakifa kwa kukosa madawa, lishe bora, kukosa elimu bora na lundo la umasikini wa kutupwa kwa kupitia programu za kijinga na vyama vyetu vya siasa ambavyo vinajiita ndio watetezi wetu kupigania maslahi yetu.

  Tangu ccm, ikaja nccr, cuf, alafu chadema hapa utaona kila mmoja anavutia upande wake. Jaribu kuangalia kila mbunge ambae amepata ubunge jana au juzi alikuwaje na leo yuko vipi? majibu utakayokuwanayo yanakuruhusu kusema ni heri nawewe siku moja uwe kiongozi au utawale japo kwa mwaka mmoja.

  Yupi atakuwa sahihi kulinda raslimali ya taifa hili tanzania? mimi au wewe.

  Bora nitawale mimi kwa hali mbaya ya wananchi wangu ambayo viongozi wetu ndo chanzo cha yote haya.


  Ukikubali nitawale nipe comment yako nini nikifanye ktk taifa hili
   
Loading...