Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,856
BORA NIKUPE TALAKA.
1)Ndoa haina furaha,kila siku kugombana.
Ndoa imeja karaha,mara zote twalumbana.
Moyo wapata jeraha,kucha kutwa twazozana.
Bora nikupe talaka,japokuwa nakupenda.
2)kila si najiuliza,kwanini tulioana.
Ndoa imejawa kiza,na mapenzi yamenuna.
Nani wakuniliwaza,wewe mapenzi hauna.
Bora nikupe talaka,japokuwa nakupenda.
3)sina budi sina njia,bora sasa kuachana.
Japokuwa wavutia,mapenzi nikupendana.
Labda nitafurahia,japo hatutoonana
Bora nikupe talaka,japokuwa nakupenda.
4)moyo umekaa chini,siwezi tena na tena.
Itanishika huzuni,usiku hadi mchana.
Wasalimu wa mjini,wambie tumepigana.
Bora nikupe talaka,japokuwa nakupenda.
5)talaka yako chukua,kwa heri ya kuonana.
Japo mbingu zachukia,waty wanapoachana.
Roho yangu yaumia,ila nitakwaza sana.
Bora nikupe talaka,japokuwa nakupenda.
Shairi=BORA NIKUPE TALAKA.
Mtunzi=Idd ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
1)Ndoa haina furaha,kila siku kugombana.
Ndoa imeja karaha,mara zote twalumbana.
Moyo wapata jeraha,kucha kutwa twazozana.
Bora nikupe talaka,japokuwa nakupenda.
2)kila si najiuliza,kwanini tulioana.
Ndoa imejawa kiza,na mapenzi yamenuna.
Nani wakuniliwaza,wewe mapenzi hauna.
Bora nikupe talaka,japokuwa nakupenda.
3)sina budi sina njia,bora sasa kuachana.
Japokuwa wavutia,mapenzi nikupendana.
Labda nitafurahia,japo hatutoonana
Bora nikupe talaka,japokuwa nakupenda.
4)moyo umekaa chini,siwezi tena na tena.
Itanishika huzuni,usiku hadi mchana.
Wasalimu wa mjini,wambie tumepigana.
Bora nikupe talaka,japokuwa nakupenda.
5)talaka yako chukua,kwa heri ya kuonana.
Japo mbingu zachukia,waty wanapoachana.
Roho yangu yaumia,ila nitakwaza sana.
Bora nikupe talaka,japokuwa nakupenda.
Shairi=BORA NIKUPE TALAKA.
Mtunzi=Idd ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.