Umenishinda tabia

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298

1)Penzi ni kama bahati,kama vyema tukipanga
penzi ni kama kabati,kwa ustadi ukijenga
upendo ni mikakati,kwa shabaha ukilenga
umenishinda tabia,nabaki kuvumilia


2)Kimya kimya nakwambia,acha nikupe vidonge
hata ukinikimbia,acha yangu niyalonge
najua utachukia,na mdomo uuchonge
umenishinda tabia,mpaka napatwa hasira


3)Sana umebadilika,umewa maneno mengi
naona hatutofika,na ndo kwanza hatujengi
moyo wangu wafunguka,yakusema yapo mengi
umenishinda tabia,paka napandwa hasira


4)Umeshaanza ulevi,ni kweli siyo uongo
unatoka na wavuvi,bila kutumia bongo
imekufa yako sivi,kwa kupenda sana hongo
Umenishinda tabia,ninahisi ukufunzwa


5)Kisa nakupenda sana,ndiop wanipa machungu
sipendagi kulumbana,nitashitaki kwa mungu
naogopa kuachana,ipotee sifa yangu
Umenishinda tabia,kukuacha naogopa


6)Nahisi rafiki yako,ndie sumu kakupea
ukanyosha kono lako,nawe ukaipokea
subiri talaka yalo,siku nitayo kupea
umeshinda tabia,kwa hiyo tabia yako


7)Ndoa ni majaaliwa,vipi wewe uzembee
usiku wasubiriwa,kuchelewa urejee
ukirudi umelewa,ni nani akupokee
umenishinda tabia,lini wajirekebisha


8)Mke apendae ndoa,sana hufanya bidii
hufuta yake madoa,mabaya hajipambii
mume ajalie ndoa,matatizo hakimbii
umenishinda tabia,nawaza urudi kwenu.


9)Liapa sitokuacha,vipi nikutoe mbio
kitumbua kijachacha,nasema kweli si ndio
yangu macho nafikicha,nalipitisha chujio
umenishinda tabia,nawaza chakukufanya


10)Maneno yangu ya mwisho,utaja vunjika guu
subiria yako kesho,nimeshasema mkuu
ndoa siyo bahatisho,utaenda chini
wewe wazembea ndoa,wenzako waitamani.

SHAIRI -UMENISHINDA TABIA
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160
NB:Anything that you see in this picture and poem is not a reality but it is creativity and picture in an edited picture.

at January 13, 2018
TwitterShare to FacebookShare to Pinterest
 
Back
Top Bottom