Wanabodi;
Nimekuwa nikifuatilia vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi.. Habari kubwa duniani kwa siku za hivi karibuni ni mauaji yanayofanywa na makundi mbalimbali ya kigaidi duniani (AL-QEDA, ISIS, BOKO HARAM, ALSHABAB etc) pamoja na ugonjwa wa Ebola.
Kwa sisi Tanzania tukio linalotugusa zaidi kwa ukaribu ni mauaji yanayofanywa na kundi la Al shabab katika nchi jirani ya Kenya. Sababu kuu ikiwa ni uwepo wa majeshi ya Kenya katika ardhi ya Somalia, pamoja na uvamizi unaofanywa na serikali ya Kenya misikitini katika kutafuta magaidi.
Wanabodi ukiona mwenzako ananyolewa wewe tia maji.. Ni muda tu unaweza sikia na sisi tumevamiwa (siombei) na hao maal shabab, just matter of time tu. So sio busara kuwasema wenzetu vibaya juu ya hilo.. Tujiangalie kwanza kama tupo salama.
Kiukweli hatupo salama hata kidogo, ni heri tunayosikia Kenya juu ya mauaji yanayofanywa na Al shabab na serikali inafanya juhudi kubwa kudhibiti kuliko sisi ambapo serikali imeshindwa kabisa kudhibiti AJALI ZA BARABARANI zinazotokea karibu kila siku sasa, na nyingi zikisababibishwa na uzembe wa madereva. Si ajabu sasa kila ukiwasha TV, Kusikiliza redio au kusoma magazeti ukakumbana na habari ya ajali mbaya imetokea sehemu fulani na kuua watu kadhaa. Serikali imeshindwa kabisa kuzinusuru roho zetu, heri Kenya inajitahidi kwenye al shabab.
Kwa wale madereva wenzangu mnajua tabia za askari wa usalama barabarani pale wanapokukamata na kosa, hicho kinachofanyika ambacho kimekuwa kama utaratibu wa kawaida ndio kinasababisha ajali za kila siku ambazo zinazozuilika. Trafiki anakukamata umezidisha abiria, badala ya kukwambia uwashushe, mkimalizana tu au akikupiga faini, safari inaendelea. Hivyo hivyo kwa spidi kubwa na ukaguzi wa matairi.
Serikali imeshindwa kudhibiti utoaji wa leseni kiholela.
Jiulize wakenya wangapi wanakufa kwa siku kutokana na Alshabab na Watanzania wangapi wanakufa kwa siku kutokana na ajali za kizembe za barabarani.. Mbaya zaidi naona wanatoaga takwimu feki za vifo au siku hizi habari hazitangazwi tena maana ajali ishakuwa kawaida.
TAFAKARI CHUKUA HATUA.