Bora Kenya, Tanzania haipo salama kabisa

sexologist

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
2,276
Reaction score
976
Wanabodi;

Nimekuwa nikifuatilia vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi.. Habari kubwa duniani kwa siku za hivi karibuni ni mauaji yanayofanywa na makundi mbalimbali ya kigaidi duniani (AL-QEDA, ISIS, BOKO HARAM, ALSHABAB etc) pamoja na ugonjwa wa Ebola.

Kwa sisi Tanzania tukio linalotugusa zaidi kwa ukaribu ni mauaji yanayofanywa na kundi la Al shabab katika nchi jirani ya Kenya. Sababu kuu ikiwa ni uwepo wa majeshi ya Kenya katika ardhi ya Somalia, pamoja na uvamizi unaofanywa na serikali ya Kenya misikitini katika kutafuta magaidi.

Wanabodi ukiona mwenzako ananyolewa wewe tia maji.. Ni muda tu unaweza sikia na sisi tumevamiwa (siombei) na hao maal shabab, just matter of time tu. So sio busara kuwasema wenzetu vibaya juu ya hilo.. Tujiangalie kwanza kama tupo salama.

Kiukweli hatupo salama hata kidogo, ni heri tunayosikia Kenya juu ya mauaji yanayofanywa na Al shabab na serikali inafanya juhudi kubwa kudhibiti kuliko sisi ambapo serikali imeshindwa kabisa kudhibiti AJALI ZA BARABARANI zinazotokea karibu kila siku sasa, na nyingi zikisababibishwa na uzembe wa madereva. Si ajabu sasa kila ukiwasha TV, Kusikiliza redio au kusoma magazeti ukakumbana na habari ya ajali mbaya imetokea sehemu fulani na kuua watu kadhaa. Serikali imeshindwa kabisa kuzinusuru roho zetu, heri Kenya inajitahidi kwenye al shabab.

Kwa wale madereva wenzangu mnajua tabia za askari wa usalama barabarani pale wanapokukamata na kosa, hicho kinachofanyika ambacho kimekuwa kama utaratibu wa kawaida ndio kinasababisha ajali za kila siku ambazo zinazozuilika. Trafiki anakukamata umezidisha abiria, badala ya kukwambia uwashushe, mkimalizana tu au akikupiga faini, safari inaendelea. Hivyo hivyo kwa spidi kubwa na ukaguzi wa matairi.

Serikali imeshindwa kudhibiti utoaji wa leseni kiholela.

Jiulize wakenya wangapi wanakufa kwa siku kutokana na Alshabab na Watanzania wangapi wanakufa kwa siku kutokana na ajali za kizembe za barabarani.. Mbaya zaidi naona wanatoaga takwimu feki za vifo au siku hizi habari hazitangazwi tena maana ajali ishakuwa kawaida.

TAFAKARI CHUKUA HATUA.
 
Natamani Wakija Waanze Kutembelea Wizara Zote Nyeti Hapa Town
jigo
 
Umekosea sana ! Kwa geopolitcs za sasa hivi Al Shabab wanahitaji Tanzania kuliko nchi nyingine ye yote ndiyo maana hapa wako kimya. Kenya imewabana somalia, wakiingia ethiopia, ethiopia huwa wanaingia somalia na wanahakikisha wameua al shabab si chini ya 400, hivyo al shabab hawathubutu kuingia ethiopia hivyo nchi salama kwao ni Tanzania na ndiyo maana wapo lakini hawafanyi kitu.
 
Wakenya walijitakia wenyewe waache wavune waliyopanda! Si kila vita lazima ujiingize tu!

Na Siku Tz ikijiingiza ktk migogoro isiyoihusu Tz Basi na Sisi tutakua ktk hatari ya magaidi km Kenya!

Wakenya watoe majeshi Yao Somalia wajenge nchi Yao! Ata hivyo ni bahati tu ya Uganda hawapakani kijiografia na Somalia, haya tunayoyaona kwa Kenya tungeyaona kwa Uganda Siku nyingi sn!
 
ugaidi na ajali za barabarani unaweza kuzicompare?
 
Kweli hatuko salama, unamaanisha FaizaFoy et al?
 
Wanabodi;

Nimekuwa nikifuatilia vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi.. Habari kubwa duniani kwa siku za hivi karibuni ni mauaji yanayofanywa na makundi mbalimbali ya kigaidi duniani (AL-QEDA, ISIS, BOKO HARAM, ALSHABAB etc) pamoja na ugonjwa wa Ebola.

Kwa sisi Tanzania tukio linalotugusa zaidi kwa ukaribu ni mauaji yanayofanywa na kundi la Al shabab katika nchi jirani ya Kenya. Sababu kuu ikiwa ni uwepo wa majeshi ya Kenya katika ardhi ya Somalia, pamoja na uvamizi unaofanywa na serikali ya Kenya misikitini katika kutafuta magaidi.

Wanabodi ukiona mwenzako ananyolewa wewe tia maji.. Ni muda tu unaweza sikia na sisi tumevamiwa (siombei) na hao maal shabab, just matter of time tu. So sio busara kuwasema wenzetu vibaya juu ya hilo.. Tujiangalie kwanza kama tupo salama.

Kiukweli hatupo salama hata kidogo, ni heri tunayosikia Kenya juu ya mauaji yanayofanywa na Al shabab na serikali inafanya juhudi kubwa kudhibiti kuliko sisi ambapo serikali imeshindwa kabisa kudhibiti AJALI ZA BARABARANI zinazotokea karibu kila siku sasa, na nyingi zikisababibishwa na uzembe wa madereva. Si ajabu sasa kila ukiwasha TV, Kusikiliza redio au kusoma magazeti ukakumbana na habari ya ajali mbaya imetokea sehemu fulani na kuua watu kadhaa. Serikali imeshindwa kabisa kuzinusuru roho zetu, heri Kenya inajitahidi kwenye al shabab.

Kwa wale madereva wenzangu mnajua tabia za askari wa usalama barabarani pale wanapokukamata na kosa, hicho kinachofanyika ambacho kimekuwa kama utaratibu wa kawaida ndio kinasababisha ajali za kila siku ambazo zinazozuilika. Trafiki anakukamata umezidisha abiria, badala ya kukwambia uwashushe, mkimalizana tu au akikupiga faini, safari inaendelea. Hivyo hivyo kwa spidi kubwa na ukaguzi wa matairi.

Serikali imeshindwa kudhibiti utoaji wa leseni kiholela.

Jiulize wakenya wangapi wanakufa kwa siku kutokana na Alshabab na Watanzania wangapi wanakufa kwa siku kutokana na ajali za kizembe za barabarani.. Mbaya zaidi naona wanatoaga takwimu feki za vifo au siku hizi habari hazitangazwi tena maana ajali ishakuwa kawaida.

TAFAKARI CHUKUA HATUA.

Ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi..hata urefu wa thread yako hamna cha msingi ...umewahi fanya tafiti kuhusu ajali za Kenya?...au unaropoka tu .
 
Nimeikuta uzi huu humu mtanadaoni leo.....
Ndege ya kivita ya Kenya, yaanguka Somalia
Ndege ya kivita ya KDF aina ya F-5 yaanguka somalia baada ya kufanya mashambulizi kwenye kambi ya Alshabaab. KDF inasema ilianguka kutokana na shida ya mashine.. sexologist bitimkongwe Ntuzu

Last edited by a moderator:
Al-shabab sio wajinga! kamwe hawawezi tia mguu bongo.., wakamuulize PK.
 
Umekosea sana ! Kwa geopolitcs za sasa hivi Al Shabab wanahitaji Tanzania kuliko nchi nyingine ye yote ndiyo maana hapa wako kimya. Kenya imewabana somalia, wakiingia ethiopia, ethiopia huwa wanaingia somalia na wanahakikisha wameua al shabab si chini ya 400, hivyo al shabab hawathubutu kuingia ethiopia hivyo nchi salama kwao ni Tanzania na ndiyo maana wapo lakini hawafanyi kitu.
Ni kweli kabisa...! wapo wengi tu huku wana-enjoy amani na mema ya hii nchi ya asali na maziwa..
 
wewe mleta mada achana kabisa na mauaji ya huko kenyaaa.....ni hatari.
 
Al-shabab sio wajinga! kamwe hawawezi tia mguu bongo.., wakamuulize PK.

usiombeeee.....mkuu hao jamaa waje huku bongo
ndomana tz waligoma kabisa kupeleka jeshi somalia wanajua mziki wake
 
Nimeikuta uzi huu humu mtanadaoni leo.....
Ndege ya kivita ya Kenya, yaanguka Somalia
Ndege ya kivita ya KDF aina ya F-5 yaanguka somalia baada ya kufanya mashambulizi kwenye kambi ya Alshabaab. KDF inasema ilianguka kutokana na shida ya mashine.. sexologist bitimkongwe Ntuzu

jamaaa nomaaa hao wasomali wako hai lakini wamekufaaa....wao hawana sababu ya kuishi duniani
wako tayari kufa wakati wowote
 
Last edited by a moderator:
Tofautisha kupigana na MTU msituni alie na silaha kama wewe vs MTU anaevizia kushambulia either sokoni or elsewhere...mkitaka thibitisha hilo peleka JW somalia uone TZ kama itawadhibiti mnavofikiria
 
Back
Top Bottom