BONGOLALA

TRABSOH

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
339
546
BONGOLALA Taifa la watu waliolala kwenye ulimwengu usio na huruma, wananchi wenye ubongo usio fikirishi ,viongozi wake wanafkiria zaidi matumbo yao kuliko ustawi wa jamii, rushwa ndio nguzo kuu ya huduma , mpaka ngazi ya mtaa na kijiji bila mkono mrefu utoboi kirahisi , vichwa vya wanajamii wake wengi wanauhusudu starehe za muda mfupi kuliko raha za muda mrefu.

Bongolala ni Taifa ambalo limejenga matabaka makubwa mawili moja la wenye uhakika wa maisha na lingine la wabahatishaji, wenye uhakika wa maisha wakifanya kila njia wabahatishaji wasije kuwa kama wao hata kwa theluthi moja kila njia inafanyika kuhakikisha hata wakijikwamua kiasi gani wawe chini yao milele. Bahati mbaya hata wabahitishaji ni kama wameridhika na hali zao na wako kwenye kifungo wasichotaka kutoka .

Wabahatishaji
Hawa jamiii za ya maeneo yake mengi zimechoka kwa uchovu wa maisha, elimu duni, na mateso ya kula kwa kubahatisha , huko Ndiko watoto wanaacha shule wakiwa darasa la tano ,mswalie mswalie mtume hata wakifika la saba hawaendi sekondari na wakienda sekondari wanaambulia sifuri , huko ndiko wezi huzaliwa, vibaka, malaya, mimba za utotoni na mihadarati hupatikana kama pipi , maisha duni yaliopitiliza kiwango hata cha ufukara. Waki cheza kamali na kuhatarisha maisha yao barabarani kwa kuendesha vyombo vya moto bila elimu ya matumizi bora ya barabara na vyombo hivyo, bila Vikinga ajari. Lakini wanapambwa na viongozi wao kwa majina ya kejeri yanayowapa ujasiri wa kuona awako katika njia mbaya atii maafisa usafirishaji.

Huku Ndiko jua hupiga zaidii maana magari na majumba yenye vipoza joto na nyumba zenye nafasi kubwa ya kuruhusu hewa kupita hamna, huku ndiko ugali unaliwa sa kumi na moja mpaka kesho sa kumi na moja. Hawa ndo wale waliofungwa kwenye mzunguko wa umaskini .

Wenye uhakika
Hawa ndio wenye nchi yao wao na vizazi vyao ndio wanashikilia ndoto za kuwa viongozi wakubwa wa Taifa .
Wana uhakika wa maisha watoto wao hawaondoki duniani kwa magonjwa kama malaria wala utapiamlo ,Hawa ndio wale hata watoto wao wakiwa na ubongo wa kuku watasoma walau hata ngazi ya stashahada maana shule wasomazo hata huwe kiazi vipi utafaulu hata kwa goli la mkono , wakati mwingine watakushangaza maarifa yao hayaendani na elimu zao.
Nyumba zao zipo kwenye maeneo yaliyopangiliwa vyema ,mfumuko wa bei sio changamoto kubwa kwao mafuta yakipanda bado utawakuta barabarani wakiendesha ndinga zao. Keki kubwa ya taifa wameificha ndani ya majumba yao bora wakuue lakini sio kugusa keki hiyo.

Huku Ndiko kuna watoto waliondaliwa makao mazuri wakikuua , ukifanya kazi nzito watakwambia mjini akili nguvu umeamua kutumia mwenyew. Huku Ndiko majivuno, dharau na kutokujali vinatamalaki , mali wanazotafuta pamoja na wabahitishaji wanataka ziwanufaishe wao na vizazi vyao tu.

Hawa hawakai gerezani na wakikaa ni muda mchache sana wanatoka, haki wanauziwa na wanamudu kulipia kwa gharama yoyote ile.

Matabaka haya yametengeneza jamii ya watu wa ajabu wasio na utu wala upendo, wabinafsi , wezi na wenye tamaa ndio wamejaa ndani ya jamii yao, wakifikiri ndio njia sahihi ya kila mtu kujali maslahi yake kumbe wamepotoka na ndo wanaliangamiza Taifa lao vizazi vyao vitahangaika kuishi katika Taifa ilo miaka mingi ijayo , linanuka shida na linatoa harufu kali ya umaskini limekosa ubunifu na linaishi kwenye kiza kinene hakuna mwenye maono ya kuwapeleka kwenye mwanga.

BONGOLALA linaweza kukomboka lakini sjui ni lini na nani atakaeweza kulitoa lilipo.
 
Back
Top Bottom