Bongo5.com:wasanii 10 waliojuu zaid mwaka huu,diamond bado namba moja

heaven on desert

JF-Expert Member
Jan 25, 2013
1,025
393
Tupo kwenye robo ya tatu ya mwaka
2013. Mwaka huu muziki wa
Tanzania umeendelea kuonesha
mapinduzi makubwa kuanzia uwepo
wa show nyingi, malipo makubwa
kwa wasanii, wasanii kuwekeza zaidi
kwenye video nzuri na za gharama
na thamani yao kuongezeka zaidi.
Ni wakati huu ambapo show za
Serengeti Fiesta zinaendelea
sambamba na Kili Music Tour. Kwa
kuzingatia idadi ya show
wanazofanya, nyimbo zao
zinavyochezwa redioni, utambuzi wa
kimataifa (international recognition)
na namna wanavyopenya zaidi
kimataifa hii ni list ya wasanii 10
walio hot zaidi mpaka wakati huu wa
robo tatu ya mwaka.
View attachment 111137
Diamond Platnumz
Hakuna ubishi kwamba Diamond
Platnumz ndiye msanii wa Tanzania
aliye hot zaidi muda huu. Mwaka
2013 aliuanza vizuri mno licha ya
kutokuwa na wimbo wowote mpya na
rasmi zaidi ya Muziki Gani
alioshirikishwa tu na Nay wa Mitego,
Kesho uliotoka mwaka jana na
Ukimwona na Mapenzi Basi ambazo
si nyimbo alizoziachia rasmi,
Diamond ameendelea kusikika kila
kona ya nchini na kwingine na
nyimbo zake zikipata rotation ya
kutosha kwenye radio zote, kubwa na
ndogo. Mwaka huu ameongoza kwa
kufanya show nyingi kubwa ndani na
nje ya nchi.
Kwa makadirio ya haraka, show
alizofanya kuanzia Burundi na
Congo, Kenya, Comoro na zile za
Tanzania, tangu mwaka uanze
hakuna shaka msanii huyo ambaye
Bongo5 imempa jina ‘Bongo Flava
Prince' ameshaweka benki si chini ya
shilingi milioni 500.
Siku chache zilizopita, ameongeza
zaidi kasi yake kwa kuachia video kali
ya wimbo wake Number 1, huku
akitambulisha mtindo mpya wa
uchezaji alioupa jina ‘Ngololo'. Kwa
spidi aliyonayo, itachukua muda
mrefu sana, Diamond kupokonywa
kijiti chake cha nafasi ya kwanza
alichokishikilia.
Lady Jaydee
Vuguvugu la Anaconda limemrudisha
rasmi kwenye chart mwanadada
huyu mkongwe. Licha ya kulianzisha
vuguvugu hili kwa matusi,
mashambulizi na madongo mazito
dhidi ya wapinzani wake wakubwa,
Clouds FM, Lady Jaydee alijikuta
akiungwa mkono na watu wengi na
kupandishwa juu kutoka chini
alikokuwa amekaribia kupotea.
Uhai wake ulirejea rasmi baada ya
show yake ya miaka 13 kwenye
muziki kwa kufanya show
iliyomuingiza mpunga wa kutosha.
Mwaka huu amefanikiwa kuwa na
hits mbili namba moja, Joto Hasira
na Yahaya. Kwa wiki sita mfululizo,
Yahaya imeendelea kushika nafasi ya
kwanza kwenye Marimba Music
Chart, MMC na bado haoneshi dalili
za kupunguza kasi.
Hadi sasa, Lady Jaydee ndiye msanii
wa kike anayepata mashavu zaidi
kuliko mwingine yeyote.
Ommy Dimpoz
Wengi hawajui ukweli huu, kwamba
baada ya Diamond, huenda Ommy
Dimpoz akawa msanii anayelipwa
fedha nyingi zaidi kwa sasa. Tangu
mwishoni mwa mwaka jana
alipoachia single yake iliyompa tuzo,
Me and You aliyomshirikisha Vanessa
Mdee, Ommy amekuwa ni mtu wa
show zisizokauka.
Mwaka huu aliongoza kwa kuwa na
nominations nyingi zaidi kwenye
KTMA na kuibuka na tuzo tatu. Kama
ilivyo kwa Diamond, Ommy ni msanii
anayechaji fedha nyingi zaidi kwa
show sasa hivi kiasi kilichomfanya
azikatae shilingi milioni 8
alizoombwa alipwe na kampuni ya
Global Publishers kwenye tamasha la
Matumaini.
Hivi karibuni aliandaa show yake
mwenyewe nchini Burundi
iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa,
ameendelea kuwa mmoja wasanii
kwenye show za Fiesta mwaka huu
na hivi karibuni, akiwa na single
mpya, Tupogo, ataanza ziara yake
nchini Marekani.
AY
Kwa muda mrefu, AY ameendelea
kuimarisha mizizi yake kimataifa na
hadi sasa, hakuna msanii wa
Tanzania mwenye mafanikio
makubwa kimataifa kama yeye. Akiwa
na tuzo ya CHOMVA 2012 mkononi
aliyoipata kutokana na video ya
wimbo wake, I don't Wanna Be
Alone, wiki iliyopita AY alikuwa
msanii pekee wa Tanzania kutaja
tena kuwania tuzo hizo
zinazojulikana sasa hivi kama
CHOAMVA katika vipengele viwili.
Mwaka huu ameachia ngoma mbili
pekee, Jipe Shavu aliyomshirikisha
Fid Q na Bila Kukunja Goti
aliyoifanya na swahiba wake Mwana
FA na kumshirikisha Mnaijeria, J-
Martins. Hivi karibuni yeye na
Mwana FA wameshoot video ya Bila
Kukunja Goti nchini Afrika Kusini na
hakuna shaka kuwa ikitoka itachezwa
kwenye vituo vikubwa vya runinga.
Pamoja na jitihada hizo AY, imekuwa
ngumu kwake kutajwa kwenye tuzo
za KTMA hali iliyomfanya Mwana FA
aandike: "Back to the drawing
board,hii wimbo imeshinda huku,si
‘kill music awards' waliigomea,kuwa
haikuwa inafaa hata kuwa kwenye
nominations zao. Ina maana viwango
vyao ni vya juu hivyo?kuwa unaweza
shinda channel O vya kwao ukawa
hujavifikia?ama kubana kwao kwa
kipuuzi kumeumbuliwa? I'm not
mad..what my boy AYTanzania won
is much much bigger than ‘KILL
music awards'..I'm just concerned…
that was ALL."
Mwana FA
Mwaka huu Hamis Mwinjuma
aliandika historia baada ya kufanya
show ya hip hip kwenye ‘corporate
audience. Ikipewa jina, The Finest,
Mwana FA alisindikizwa na bendi
kongwe ya Kilimanjaro aka Njenje
kuangusha show iliyofanikiwa sana.
Uhusiano wake na Njenje ulizalisha
wimbo wake Kama Zamani ambao
tayari video yake imeendelea kufanya
vizuri na pia kuchezwa Channel O.
Mwaka huu Mwana FA alikuwa
msanii wa tatu miongoni mwa
wasanii wa Tanzania wanaoingiza
fedha nyingi kwenye miito ya simu,
nyuma ya Rose Mhando na Diamond
kwa kuingiza shilingi milioni 18.
Mafanikio yake mengine yana
uhusiano wa moja kwa moja na yale
ya AY kwa ushirikiano wao wa siku
nyingi na hivi karibuni wote
walienda nchini Kenya kutengeneza
nyimbo mbili na producer mkongwe,
Eric Musyoka wa Decimal Records.
Chege na Temba
Ni ngumu kuyasema mafanikio ya
Chege bila kumtaja Temba na vice
versa. Kwa muda mrefu, wakali hawa
wameendelea kuwa pamoja na hivi
karibuni kwenye show za Fiesta
wameendelea kutajwa kuwa wasanii
wanaoshangiliwa zaidi kwa kufanya
show nzuri kuliko wengine.
Nay wa Mitego
Mwaka huu umekuwa mzuri kwa Nay
wa Mitego hasa kwakuwa amekuwa
akipiga show nyingi zinazomuingizia
mkwanja mzuri. Nay wa Mitego
amehit zaidi na Muziki Gani
aliomshirikisha, Diamond Platnumz.
Wimbo huo ulimsaidia kumfungulia
zaidi milango ya neema rapper huyo
controversial. Baada ya kuachia
wimbo wake mpya, Salam Zao, Nay
alirejea tena kwenye midomo ya
watu, blogs, magazeti na kwenye
vituo vya redio na TV kuhusiana na
yale aliyoyasema kwenye wimbo huo.
Lakini kama usemi usemavyo,
promotion yoyote ile ni promotion
nzuri, aina hiyo ya uimbaji
imeendelea kumweka pazuri.
Ben Pol
Ben alijikuta mahali pazuri zaidi
baada ya mwaka huu baada ya
kushinda kipengele cha mtunzi bora
wa mashairi ya Bongo Flava kwenye
KTMA. Na baada ya kuachia video
yake ya Jikubali, Ben Pol ameendelea
kupanda juu kwa spidi huku akiwa
msanii anayetafutwa zaidi kwaajili ya
chorus.
Stamina na Young Killer
Jana na Leo, imewaweka karibu zaidi
rappers hawa japokuwa kila mmoja
ana nyimbo zake zinazofanya vizuri.
Mwaka huu Young Killer aliuingia na
wimbo wake Dear Gambe ambao laiti
kama angekuwa na umri juu ya
miaka 18, angechukua tuzo kibao za
KTMA. Wimbo wake mpya sasa ni Mrs
Superstar ambao umezidi kupigia
mstari uwezo wake kimashairi. Kwake
Stamina naye, Wazo la Leo
aliomshirikisha Fid Q na Mwambie
Mwenzio aliomshirikisha Warda na
Darassa zimemweka pazuri na
kujikuta yeye na Young Killer
wakiwepo kwenye show zote za Fiesta
zinazoendelea.
Madee
Single moja tu, Sio Mimi,
imemuingizia Madee zaidi ya shilingi
milioni 130, na kuthibitisha kuwa,
hit moja tu inaweza kubadilisha
maisha ya msanii. Hadi leo jina la
Madee halikosekani kwenye show
nyingi kubwa na huku akiwa
miongoni mwa wasanii wanaonekana
kupata shavu la kufanya show nyingi
zaidi za Fiesta mwaka huu.
source:bongo5.com
 
naona msemaji wa diamond unataka kujiingiza kwenye joto hasira kwa kutumia bongo five.

Ni wazi huu mtandao una ukaribu na clouds.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom