wanasrmaga ukitaka kuongea kitu na watu wakuamini ongea kwa ushahidi na facts za ukweli, nisikuchoshe msomaji wa mada naenda direct kwenye kukujuza celebrities top 3 ya wasanii wenye pesa utitiri bongoWa
Number 1: Masanja mkandamizaji-
Najua wengi kwa haraka haraka mlidhani hii namba itakuwa ni ya Diamond lakini La hasha, Masanja ni comedian maarufu Tanzania aliyewekeza kwenye miradi ya mpunga huko mbeya na pia anamiliki mgodi wake wa dhahabu, NARUDIA TENA!!! MGODI WA DHAHABU, hii pia imethibitishwa pale ambapo huyu bwana ana bmw ya kisasa na yenye bei kali kuzidi la mpinzani wake diamond platnumz
Number 2: Diamond platnumz-
Bongo tunamuita simba ila Afrika wanamuita king of pop, Hakuna msanii Bongo anayelipwa pesa nyingi kwa show moja kama Diamond, Kumekuwa na wasanii wenzake kama kina Ali kiba, Christian bela, n.k waliofanya mziki muda mrefu kuzidi yeye lakini kumkuta kimafanikio sio leo, Mafanikio hayaongelewi bali yanaonekana kijana ana nyumba yake nzuri madale na pia amewekeza katika kununua nyumba , pia kwa sasa ana label ya WCB ambayo amini usiamini inamuingizia pesa kila kukicha.
Number 3: Lady jay dee:
Miaka nenda rudi wasanii wenzake wanamkuta na wanamuacha, Kipaji anacho nauzuri wake kinamuingizia pesa za kutosha, ukiachana na muziki pia ni mjasiria mali ambae biashara zake zinamuingizia pesa chafu, Dada anamiliki ndinga matata range rover evoque model ya kisasa ambayo ni ndoto za mchana kwa wasanii wa kawaida