Lalo Salamanca
JF-Expert Member
- Dec 9, 2012
- 1,556
- 1,169
Nimeangalia movies na Tv series nyingi japo sio sana ila nimegundua kuwa Africa kuna location nyingi sana za kufanyia movies, hata stories na matukio yanayotokea na yaliyowahi kutokea nchi za Africa yanaweza kubadilishwa na yakawa movies na zikawa nzuri sana. Mfano mauaji ya Kimbari yaliyotokea Rwanda na movies zilizotengenezwa kureflect hilo kama "Hotel rwanda" na zingine, utekaji nyara wa meli Somalia zinazotokea ulaya kuna movie ya "Captain Phillip", hata vita vya wenyewe kwa wenyewe mfano Series ya "Strike Back" season 3 karibu yote imefanyiwa Africa. Lakini sisi na filamu zetu hapa tunang'ang'ania kuigiza maisha yasiyokua ya kwetu ndio maana watu wanatoka mbali huko wanakuja kuigiza kwa niaba yetu. Kuna movie ya "The White Masai" na "Nairobi Half Life" yaani ni mazingira halisi kabisa ya Africa ambayo sisi tunashindwa kuigiza,na ziko katika kiwango cha juu sana.
Tatizo letu ni nini hasa? Je tunaogopa gharama?? hatuyaoni haya??
Come on bongo movies,why not us?
Tatizo letu ni nini hasa? Je tunaogopa gharama?? hatuyaoni haya??
Come on bongo movies,why not us?