Hata ukilinganisha kama za Gana na Naijeria za kiafrika tena za vijijini kabisa hizi za kibongo ni sifuri, hazina hisia ni story tuu za kawaida kama mazungumzo ya kwenye vijiwe vya kahawa. Wasanii wa hapa ni kuchukuana ili utoke, au kama mwanamke kwakua ni mrembo, Hajui kuongea hajui kulia, hajui kusikitika, hajui kuimba wala kucheza hajui kukasirika wala kununa, hawajui kuomba samahani mpk ww unaeangalia ikakuingia, hawajui kuspendi wala hawajui kuact kama ni mwanakiji unamkuta mtu kaweka nywele dawa, wengi wao wakijiona warembo wanachagua sehemu za mapenzi tuu kila siku, hawawezi kuact tofauti na mtu anakua tofauti kweli mpk unaweza kuuliza huyu ndie au sie ukimkuta kwenye mazingira ambayo si ya kawaida.