Bongo movie, Bodi ya filamu washitakiwe

ZE NDINDINDI

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,885
4,012
Kumekuwepo na taarifa kwamba eti wanataka kumshatki DJ Murphy kwa kutafsiri movie za nje kwa kiswahili, aisee hawa wehu tumewalegezea sana embu twende nao samba sasa kama mbwai iwe mbwai tu.

Hawa wasanii wa Bongo movies wanatumia sound effects za movie za Hollywood, yaani maigizo yao tu yakianza utasikia sound za 300, terminator hadi movie za Nigeria zinatumika.

Wanatumia nyimbo za wasanii kama P Square na hata za wasanii wa America kwenye maigizo yao bila ruhusa
wanaiga movie za watu na kuzicheza kwa kiswahili haswa bwana JB.

Hayo yanatosha kuwafikisha mahakamani na kuwasiliana na wahusika ambao soundtracks zao zimetumika kwenye maigizo ya kibongo bila ruhusa yao au kama Makonda alivyosema watuonyeshe mikataba inayowaruhusu kufanya hivyo.

Bodi ya filamu huwa inakagua maigizo ya hawa wapuuzi ila inapitisha bila hata kuuliza ruhusa ya kutumia soundtracks za watu, nao washtakiwe.
 
Majingasana hayo,memarayamwisho kuangalia bongo movie ni mwakajana wakati nasafiri
 
Wanatapatapa tu..wanajikombakomba ili waonekane na kwa taarifa yao Hela yangu hawatoipata kwenye kununua filamu zao..Nadownload zangu series za nje inatosha

Huu uzalendo wa kulazimishana umenishinda
 
Back
Top Bottom