Bongo land

Okol36

JF-Expert Member
Jan 10, 2015
1,524
716
Hii ndio Bongo

Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya. MZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi....kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic . BINTI: Mi naitaka hii MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe. Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako... Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee. MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano. MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.
 
Asante mjomba hiyo ndio dawa ya vidafa vinavyopenda vinavyoonekana kwa nje ila ukweli wa mambo anaujua muhusika
 
Back
Top Bottom