Bongo kila mtu daktari na mwanasheria

GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
5,902
10,503
Huko Tanganyika kila mtu mjuzi. Kwenye uandishi wa habari wamo, kwenye udaktari wamo, kwenye sheria wamo. Mradi tu kujitia ujuvi.

Kipindi cha Covid-19 Kila mtu aligeuka kuwa mwanasayansi na mchambuzi mahiri wa conspiracy theories na international propaganda!

Juzi kuna makanjanja wamekamatwa muhimbili pale wakijifanya madaktari. Kasoma soma tu videsa vya Google kajitunuku na cheti cha udaktari yeye mwenyewe!

Ndio sampuli ya watu waliomo mitandaoni wakipotosha na kutoa ushauri batili watu wakiwaamini kuwa ni madaktari. Ndio hawa wa "Kunywa juisi ya mchaichai, meza karafuu, fanya vile na vile...." tafrani tu.

Kipindi fulani palizuka vishoka mahakamani lakini wakadhibitiwa ipasavyo. Kukopi kopi tu gugo na yeye kashakuwa wakili.

Ndio sampuli ya watu humu wanatoa ushauri batili wa kisheria mitandaoni kisha watu wakaamini ni ushauri sahihi.

Majukwaa ya sheria na majukwaa ya madaktari yadhibitiwe, na ushauri wowote unaotolewa humo uchukuliwe kwa tahadhari kubwa.

Kama una shida ya kitabibu ama kisheria tembelea hospitali na ofisi za mawakili.

BE SO WARNED!
 
Siyo Bongo peke yake bali ni duniani kote. Misinformation ni tatizo la dunia nzima ndiyo maana platforms nyingi kama IG, FB na Twitter imebidi kuja na mikakati ya kupambana nayo. Kuna conspiracies za kila aina na maelezo ya karibu kila kitu - mazuri na mabaya. Ni wajibu wetu kuchambua mbivu na mbichi kama tulivyoonywa na Mkwere:

Akili za kuambiwa ALWAYS changanya na zako

Ila Wabongo sijui kidogo tumezidi maana dah!
 
Wabongo wamezidi asee
 
Back
Top Bottom