Bongo Hiyooooo, Njia Panda ya Mkoa

Hii ni Stendi ya mabasi ya kwenda ndani na nje ya dar.Ni ya pale karibu na Jengo la Tanesco Ubungo.Hako kajengo kenye paa jekundu ndio choo cha kulipia...shilingi 200 kwa haja kubwa na ndogo na kuoga. Baada ya hapo yanaanza magari ya Mbagala na Mnazi Mmoja.Yetu ya Mlandizi hayana rangi ya kuchorwa iliyoasisiswa na Mwaibula
 
Camera gani ulitumia na ulikuwa upande gani? Umepiga eneo kubwa!
 
Camera gani ulitumia na ulikuwa upande gani? Umepiga eneo kubwa!

Picha hiyo itakuwa imepigwa kwa juu hasa nadhani jengo la Tanesco na imepigwa mchana. Kuhusu camera itakuwa ni digital ya kawaida tu.
 
Kaka Mlandizi tena..kumbe wewe wanyumbani kabisaa aisee..!!
Unakaa pande zipi pale? Tena mimi nimebukua Ruvu Sekondari pale wakati ule ikiwa ni ya mchanganyiko. Mitaa ya Mlandizi naijua vyema sana:upande wa Kilangalanga na ule wa Mlandizi bondeni hadi Ruvu JKT
 
mbona sioni magari ya gongolamboto au wanageuza nayo river side!!!
 

Kuhusu foleni msihofu baada ya CDM kuingia madarakani hali itakuwa kama hivi.
 
Nashangaa bado wanaoingia ni wengi kuliko wanaotoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…