Boxer wa zamani Larry Homes adai heavy weight champions wa sasa wasingetoka salama enzi zake.

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,459
17,266
Mwana masumbwi wa uzito wa juu Duniani Larry Homes amesema wapiganaji wa sasa wa ngumi wasingetoka salama enzi wake akiwa ulingoni.

Homes amasema ni kweli kua hawa wana masumbwi wa uzito wa juu wa sasa kina Joshua, Tyson, Wilder na wengine kina kibonge wasingetoa upinzani ila wasingechukua roud ulingoni.

Mimi binafsi nakubaliana nae, hawa heavy weight wa sasa hakuna kitu, ngumi zimepoteza mvuto, hakuna hard punchers kama kina Lyle, Earnie Shavers, Jimmy Young, Leo Spinks, George Formen, Ken Norton, Jerry Quarry, Ali, Smoking Joe, na kadhalika.

Mkongwe Bob Foster aliwahi kusema boxing now days is like wrestling.

Mimi binafsi baada ya kizazi cha kina Riddick Bowe, The Real Deal, Tyson nilipoteza hamu ya kufuatilia ngumi.

Larry Holmes: Current Heavyweights "Couldn't Stand A Chance" In My Era
 
Uko sahihi na uzuri hajajizungumzia yeye peke yake (watu wanaweza hisi anajifagilia tu) kasema kwa hawa watoto walaini wa saa hz wasingetia mguu kwenye zama zao akawa taja na wakongwe wenzie anaoamini yeye walikuwa nuksi sana!
 
Maisha katika ubondia yamebadilika. Wazia kwamba tumetoka enzi za pambano kua na mpaka raundi 50 hadi leo kuna raundi 12.

Zamani iliwezekana kwa bondia kupigana hata ndani ya miezi 3 na watu hata wanne tofauti ila siku hizi hayo yamepunguzwa ili kupunguza chansi za injury na vifo...

Pia boxers wengi wanarely kwenye tekniki kuliko power, usiniquote vibaya hapa ukadhani nimemaanisha hakukua na skilled boxers enzi za akina Holmes ila siku hizi ni mabondia wachache wanaweza amua kwenda toe to toe bila kua na uhakika wa ushindi.
 
Laini sana aisee. Sioni ngumi nzito kabisa.
 
Ila mkuu unajua kabisa boxing is about power and strength, kubadili ngumi kua tekniki ni sawa na kufanya mchezo wa ngumi uwe wa pata potea kama kamari.

Ndio maana Bob Foster alisema ngumi sasa zimekua kama mieleka. Mieleka ndio unatumia tekniki, unaona Ray Mysterio mwenye kilogram 70 anapigana na Big show mwenye kilogram 220 na Ray anashinda kwa sababu ametumia tekniki.

Leo baada ya pambano moja mchezaji anahitaji mezi zaidi 12 kujiandaa kwa pambano lingine, utafikiri anasoma shule ambapo inahitaji mwaka mmoja kumaliza darasa moja kwenda lingine.

Nakumbuka Tyson alipigana na Razor Ruddock mwaka 1991 March refa akasitisha pambano kimakosa, likaandaliwa lingine ndani ya miezi 3, Jume 1991 zikapigwa round 12 hadi Tyson akavunjwa ngoma ya sikio na ngumi ya Razor maarufu kama The Smash.
Razor Ruddock: Would His “Smash” Have Taken Out Joshua, Wilder – Fury? — Boxing News

Mimi binafsi nakosa flavor kabisa kwenye ngumi, ndio maana ni bora niangalie mieleka(ingawa ya sasa pia sio mitamu kama ya kina Stone Cold Steve Austin, The Rocky Maivia-The Rock, ) kuliko boxing.
 
Ila mkuu unajua kabisa boxing is about power and strength, kubadili ngumi kua tekniki ni sawa na kufanya mchezo wa ngumi uwe wa pata potea kama kamari.

Ndio maana Bob Foster alisema ngumi sasa zimekua kama mieleka. Mieleka ndio unatumia tekniki, unaona Ray Mysterio mwenye kilogram 70 anapigana na Big show mwenye kilogram 220 na Ray anashinda kwa sababu ametumia tekniki.

Leo baada ya pambano moja mcezaji anahitaji mezi zaidi 12 kujiandaa kwa pambano lingine, utafikiri anasoma shule ambapo inahitaji mwaka mmoja kumaliza darasa moja kwenda lingine.

Nakumbuka Tyson alipigana na Razor Ruddock mwaka 1991 March refa akasitisha pambano kimakosa, likaandaliwa lingine ndani ya miezi 3.

Mimi binafsi nakosa flavor kabisa kwenye ngumi, ndio maana ni bora niangalie mieleka(ingawa ya sasa pia sio mitamu) kuliko boxing.
Chief tragedies ndiyo zimeubadilisha mchezo wa ngumi.

Cheki hapa

Benny 'Kid' Paret vs Emile Griffith: The Maricón Fight

Pia tafiti zinaonyesha kwa zamani mara nyingi bondia huweza hata kufa kwa kushiriki mapambano mfululizo bila kupumzika. Mfano Benny alipigana na Fullmer kisha akapigana na Emile miezi 3 mbele. Wakati Fullmer alisubiri miezi kumi ndiyo akarudi tena ulingoni.

Mabadiliko yanalenga kumkinga bondia na majeraha, magonjwa na kifo.
 
Mkuu ina maana ndani ya miaka 15, 20 ndio kumekua na vifo, magonjwa, injury nyingi kwa maboxer kuliko wenzao wa miaka 20 iliyopita? Kwamba hao kina Tyson walikua wagumu zaidi kuliko hawa wa sasa?
 
Mkuu ina maana ndani ya miaka 15, 20 ndio kumekua na vifo, magonjwa, injury nyingi kwa maboxer kuliko wenzao wa miaka 20 iliyopita? Kwamba hao kina Tyson walikua wagumu zaidi kuliko hawa wa sasa?
Ona hii kitu boss.

Kabla ya Mike Tyson kulikua na wakina Joe Luis kabla yake kulikua na Rocky Marciano kabla yake walikuwepo wakina Max Baer kabla ya Max Baer walikuwepo wakina Dempsey.

Max Baer alipelekea vifo vya watu wawili ulingoni na ni hardest puncher ever. Je mtu wa enzi za Max Baer akisema wakina Mike Tyson hamna kitu utamuaminishaje kama kuna kitu?

My point is idadi ya vifo na injuries haitupi picha ya era gani ilikua na hard punchers ila inatupa picha ni era gani ubondia haukua ukiconsider taratibu za kiafya. Ila hard punchers wapo katika kila generation.

Mike Tyson na Larry Holmes walikuta ubondia upo watered down kiasi chake hivyo the process is ongoing haikua mwisho kwao tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom