Bomu latibua futari Mbagala! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomu latibua futari Mbagala!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 3, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Wakati wahanga wa mabomu ya Mbagala wakiwa bado hawajasau vizuri yaliyowakumba siku za nyuma....mlipuko mwingine wa bomu ulitokea juzi na kusababisha tafrani ya aina yake kwa wakazi hao ambao baadhi yao walikuwa wakijipatia futari.

  Mlipuko huo ulitokea saa moja usiku mtaa wa Mbagala Kuu baada ya msimamizi wa nyumba namba MA/1/2835, aliyefahamika kwa jina la Emmanuel kumaliza kukusanya taka na kuzichoma kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi.

  Emmanuel ambaye hakumtaja mmiliki wa nyumba hiyo, alisema alikuwa anafanya usafi saa 11 jioni na baada ya kufanya usafi huo aliondoka kwa muda lakini ilipofika saa moja usiku wakati taka hizo zikiungua, ghafla kulisikika mlio mkubwa eneo alilokuwa amekusanya taka hizo. Alisema baada ya mlio huo majirani wa eneo hilo ambao walikuwa wanamalizia kufuturu walilazimika kukimbia ili kunusuru maisha yao.

  Kwa mujibu wa Emmanuel, mlipuko huo uliwakumbusha yale yaliyotokea Aprili 26 mwaka huu na kusababisha watu 26 kupoteza maisha. “Tunaiomba Serikali itume wataalamu wa mabomu ili kuchunguza zaidi kwani tumelipwa fidia na wengine tumeanza ujenzi, tuna wasiwasi hali inaweza kubadilika.

  “Inaonekana kuna baadhi ya mabomu yamejifukia chini sasa tunapoanza ujenzi yanaweza kulipuka, tutaishi kwa hofu hadi lini? Mtu kachoma moto tu hapa kishindo kilichotokea kila mmoja alikimbia sehemu yake, tunaomba waje kuangalia kama mabomu yapo au hayapo ndipo tuanze kujenga,” alimalizia.

  Source: http://www.darhotwire.com/home/news/2009/09/01/bomu_latibua_futari_mbagala.html
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mwezi mtukufu jamani.

  Allah atawalinda, inshaahlaah mashaalah
   
 3. kikaango

  kikaango Member

  #3
  Sep 3, 2009
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni ndugu zangu mungu yupo atawaokoa. Serikali wasaidieni hao kusafisha kabisa maeneo au kuwahamisha
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Allah atawalinda na mabalaa hayo
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mungu hubariki hatua unazo chukua, ukikaa kwenye mkeka na kusubiri allah.....umeliwa.
   
Loading...