meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,828
Tunaposema huu upuuzi wa vyuo vya kata hautakiwi watu wanasema tuna dharau bora jamii inajionea yenyewe.
Ati mtu alifeli kidato cha nne leo hii anapewa cheti cha kuwa daktari...ukiuliza nini eti ooh tunapunguza uhaba wa madaktari...pambaff sana.
MY TAKE
Ati mtu alifeli kidato cha nne leo hii anapewa cheti cha kuwa daktari...ukiuliza nini eti ooh tunapunguza uhaba wa madaktari...pambaff sana.
MY TAKE
- SERIKALI INATAFUTA KURA
- G.ABACHORI ANASAKA NOTI
- MLALAHOI ANASAKA AJIRA YA URAHISI
by JackbauerSerikali ingewekeza katika vyuo vya utabibu kama vile KILOSA,KIBAHA,MVUMI na MACHAME tungeweza kuwa na vyuo bora sana kuliko IMTU lakini kwa kuwa serikali na jamii yetu inaamini mafanikio yanakuja kwa kukurupuka na bahati bahati haya ndio matokeo yake.
Roma haikujengwa kwa siku moja,vile vile taasisi kama MUHAS,UDSM,SUA,MUCCOBS hazikujengwa siku moja.
Leo hii unashuhudia chuo kama KAM MEDICS kinafundisha matabibu usishangae mwakani kinatoa degree ya udaktari,udaktari wa meno,pharmacy,na kozi nyingine lukuki bila kujipanga halafu unategemea ilinganishwe na MUHAS...huu ni uhuni.
Nasikia sikia kuwa UDSM ilianza kama kitivo cha sheria cha chuo kikuu cha EAST AFRICA leo hii ni university yenye courses lukuki sasa linganisha na UDOM na mikozi yake lukuki iliyoanza juzi juzi halafu uniambie itakuwa sawa na UDSM...what a joke?go to ARUSHA UNIVERSITY,MAKUMIRA UNIVERSITY n.k ujionee idadi ya course zilizopo kulinganisha na resources.
Mbona taasisi kama DIT imebakia kuwa tech college na inatoa wahitimu wazuri tu bila hata kujipachika u-UNIVERSITY?
Tuache utani wa elimu hasa hasa elimu inayohusu afya.
Miaka takribani 15 tumeshuhudia wanafunzi wa sekondari wakifeli masomo ya sayansi vibaya sana PCB ikiwemo halafu linganisha na idadi ya wanafunzi wa udaktari katika kipindi hicho(waweza kuta zinalingana au hata kuwa kubwa kwa wahitimu wa elimu za afya) sasa utajiuliza wametokea wapi?
Muhimbili ilikuwa inadahili wanafunzi kati ya 70-150 kipindi kile cha watoto wakifaulu vizuri na nusu au robo tatu kati yao walikuwa wanadisco sasa leo hii Muhimbili anatoa 200,KCMC 100,Bugando 70,IMTU 90 n.k hii akili ya ukubwani au vyuoni imetokea wapi ghaflaghafla?....Tunaendekeza siasa ee?tunajidanganya wenyewe!
Siamini kama ni number ya watumishi wa afya waliopikwa nusu ndio imetuletea matokeo mazuri tunayoyaona kwenye afya kwa sasa bali ni juhudi za USA na wenzake.
Matokeo ya elimu hii ya kata ni uwepo wa semina nyiingi zinazoenda kwa jina la 'ON JOB TRAINING" hii inadhihirisha kuwa mabomu yaliyotegwa na vyuo vyetu inabidi yateguliwe..swali ni kwamba tutaweza kuyategua yote kwa wakati kabla hayajalipuka?...jibu ni hapana na mengine ndio hayoo yanalipuka!
Last edited by a moderator: