BOMU LA ARUSHA: Serikali imeanza kucheza mchezo wa kisiasa?

BOMU LA ARUSHA: Serikali imeanza kucheza mchezo wa kisiasa?

Sijaelewa, kwanini jina la mtu 1 tu ndio linatajwa wakati walioshikiliwa na polisi ni watu 6? Nahisi kuna kamchezo kanataka kuchezwa hapa.

Kwa akili ya kawaida tumeanza kuelewa.
Nina hakika unaweza kuwa mchezo wa serikali hii. Kuna ukweli kwamba huyo boda boda anayetajwa alijitokeza kueleza tukio hilo kwamba alikodiwa na mtu ambaye alizunguka naye na mwisho akamuelekeza ampeleke pale kanisani. Wakati tukio la bomu linalipuka yule bodaboda alikimbia kama watu wengine kujinusuru na alikuwambia wenzie tukio hilo na kuwa tayari kutoa ushirikiano na polisi na sasa inasadikika au stori za Nchimbi zinamtaja kama mtupa bomu. Huu ni upotoshaji namba moja unaoniaminisha kuwa serikali imehusika na tukio hili kwa sababu wanazojua wao kama walivyojihusisha na Dr
Ulimboka na pia Kibanda huku wakisingizia watu wasiohusika.
Kuomba tuwe na utulivu si hoja lakini kama usalama wetu unaweka rehani maisha yetu kwa manufaa ya ccm inatusaidia nini?? Hata hivyo sie watanzania tumekuwa wavumilivu na wenye subira pamoja na vituko vyote hivi vya ccm.
Mbona hawatutajii majina ya wahusika wengine wengine?? Hapa pia bado wanaendeleza siasa za kidini kwa kutaja raia mmoja mkristo ili ionekane mhusika ni mkristo. Wenye akili zetu tunaelewa mchezogani wanafanya watu hawa wakina Nchimbi. Waache kucheza na akili za watanzania. Tunaelewa wanachofanya na mchezo wao ni mauti kwetu!
 
SERIKALI KUCHUA HATUA KALI MLIPUKO ARUSHA
Monday, 06 May 2013 Written by Mjengwa Blog Email Tuma Maoni

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Dkt.Emmanuel Nchimbi

Na Immaculate Makilika-Maelezo
SERIKALI imesema kuwa itachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi nafasi yake katika jamii kufuatia kuwepo kwa watu wachache wasiyoitakia mema nchi yetu kutaka kupandikiza chuki za kidini miongoni mwa Watanzania na kuleta mapigano, mauaji nchini
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu mlipuko wa uliotokea katika kanisa la katoliki la Mtakatifu Joseph Parokia ya Olasiti Arusha mjini Mei 5, mwaka huu saa 4:30 asubuhi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi 59, kati ya hao watatu ni mahututi.

Aliwataja watu waliofariki dunia kuwa ni Regina Kurusei mwenye wa miaka 45 mkazi wa Olasiti ambaye alifariki siku ya tukio wakati alipokuwa kipatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru na James Gabriel(16) aliyefariki usiku wa kuamkia leo.
“Tutachukua hatua kali bila huruma kuzigandamiza njama hizi mbaya dhidi ya taifa letu. Tutachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa letu kwanza,” alisema Waziri Nchimbi.
Alisema tayari kikosi kazi maalumu kimeundwa ili kuchunguza tukio hilo.
Waziri Nchimbi alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mlipuko huo ni bomu. Hivyo uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania .
“ Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na jeshi la polisi. Miongoni mwao ni Victor Ambroce mwenye umri wa miaka 20, dereva wa bodaboda,mkazi wa Mrombo, Arusha,ambaye anatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo. Watuhumiwa wengine watano waliokamatwa ni raia wane wa kigeni na Mtanzania mmoja ambao wanashikiliwa kwa maahojiano,” alisema.
Aidha Waziri Nchimbi alisema Serikali inamewataka wanasiasa na viongozi wote wajiepushe na kauli zinazochochea ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki miongoni mwa Watanzania.
”Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za kisheria itakazozichukua dhidi ya viongozi wa aina hii ambao maslahi yao ni muhimu kuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania,” alisisitiza huku akisema Serikali kwa nguvu zake zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wote waliohusika na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hilo wanasakwa popote walipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria..
Aliongeza kuwa kwa niaba ya Serikali anaungana na Watanzania kulaani wahusika wote wa tukio hilo walioshiriki kwa njia yoyote. Pia inawataka viongozi wa kisiasa, kidini,na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu.
Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya kuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia, mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Baba Mtakatifu, Askofu Fransisco Mantecillo Padilla. Aidha alikuwepo mwenyeji wake Askofu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu la Arusha.
Inakadriw a kuwa katika uzinduzi huo kulikuwa na watu zaidi 2000. Hivyo wakati mgeni rasmi akiwa ametoka nje akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi mtu aalirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu na baada ya kutua kulitokea kishindo na mlipuko mkubwa.
Katika tukio hilo viongozi wa Serikali na dini waliohudhuria ibada hiyo hawakupata madhara.

Machezo ya CCM:

Nategemea juhudi zinafanywa kuwachomoa wasaudi na kesi atasukumiwa Dereva wa Bodaboda. Rusubiri tuu.
 
Kwa akili ya kawaida tumeanza kuelewa.
Nina hakika unaweza kuwa mchezo wa serikali hii. Kuna ukweli kwamba huyo boda boda anayetajwa alijitokeza kueleza tukio hilo kwamba alikodiwa na mtu ambaye alizunguka naye na mwisho akamuelekeza ampeleke pale kanisani. Wakati tukio la bomu linalipuka yule bodaboda alikimbia kama watu wengine kujinusuru na alikuwambia wenzie tukio hilo na kuwa tayari kutoa ushirikiano na polisi na sasa inasadikika au stori za Nchimbi zinamtaja kama mtupa bomu. Huu ni upotoshaji namba moja unaoniaminisha kuwa serikali imehusika na tukio hili kwa sababu wanazojua wao kama walivyojihusisha na Dr
Ulimboka na pia Kibanda huku wakisingizia watu wasiohusika.
Kuomba tuwe na utulivu si hoja lakini kama usalama wetu unaweka rehani maisha yetu kwa manufaa ya ccm inatusaidia nini?? Hata hivyo sie watanzania tumekuwa wavumilivu na wenye subira pamoja na vituko vyote hivi vya ccm.
Mbona hawatutajii majina ya wahusika wengine wengine?? Hapa pia bado wanaendeleza siasa za kidini kwa kutaja raia mmoja mkristo ili ionekane mhusika ni mkristo. Wenye akili zetu tunaelewa mchezogani wanafanya watu hawa wakina Nchimbi. Waache kucheza na akili za watanzania. Tunaelewa wanachofanya na mchezo wao ni mauti kwetu!

Kwani ulikuwa hujui, watalamu wa ku-analyze mambo tulisha sema parterns zinajirudia kama mwaka 2005 - 2010 walipisingizia CUF. Kwanza ilikuwa Udini, Ukabila baadaye Ukaja Ujambazi na Ugaidi. Sasa hayo hayo yajirudia kwa CHADEMA. Tatizo CHADEMA akili kubwa haiwezi kuangukia kwenye mtego uliommaliza CUF, wamekinukisha hawana ujanja, Vatican sio mchezo, watajulikana wote.
 
Kikwte anataka kuprove kuwa yy si mdinI na haya mashambuliz yanayotokea si waislam..ss ili kutuprovia kuwa si waislam akaamua aweke zengwe la kumpachika mkristu kuwa ndo mtuhumiwa ambaye n victor..swali je wanashikiliwa 6 kwann tutajiwe jina la mmoja tu..hili ni zengwe tu na tumewashtukia...ukizingatia lema alimtuhum kuwa n mdini..kinda rubbish
 
Kwa akili ya kawaida tumeanza kuelewa.
Nina hakika unaweza kuwa mchezo wa serikali hii. Kuna ukweli kwamba huyo boda boda anayetajwa alijitokeza kueleza tukio hilo kwamba alikodiwa na mtu ambaye alizunguka naye na mwisho akamuelekeza ampeleke pale kanisani. Wakati tukio la bomu linalipuka yule bodaboda alikimbia kama watu wengine kujinusuru na alikuwambia wenzie tukio hilo na kuwa tayari kutoa ushirikiano na polisi na sasa inasadikika au stori za Nchimbi zinamtaja kama mtupa bomu. Huu ni upotoshaji namba moja unaoniaminisha kuwa serikali imehusika na tukio hili kwa sababu wanazojua wao kama walivyojihusisha na Dr
Ulimboka na pia Kibanda huku wakisingizia watu wasiohusika.
Kuomba tuwe na utulivu si hoja lakini kama usalama wetu unaweka rehani maisha yetu kwa manufaa ya ccm inatusaidia nini?? Hata hivyo sie watanzania tumekuwa wavumilivu na wenye subira pamoja na vituko vyote hivi vya ccm.
Mbona hawatutajii majina ya wahusika wengine wengine?? Hapa pia bado wanaendeleza siasa za kidini kwa kutaja raia mmoja mkristo ili ionekane mhusika ni mkristo. Wenye akili zetu tunaelewa mchezogani wanafanya watu hawa wakina Nchimbi. Waache kucheza na akili za watanzania. Tunaelewa wanachofanya na mchezo wao ni mauti kwetu!

Sio Mapolisi wote au wana TISS wanaimba wimbo wa CCM. Tunaomba mtujuze juu ya huyu Dereva wa boda boda anayebebeshwa zigo hili, kitakacho fuata ni kumuhusisha na Chadema na Lema.
 
Tukio hili ni tofauti kabisa na matukio mengine, hakuna ujanja ujanja wowote utakaofanyika, ili ni shambulio dhidi ya Balozi halali anayewakilisha Vatican hapa Tanzania na target namba two ilikuwa ni Askofu.Sasa basi licha ya kuwa JK alishamaliza ziara yake huko kwa Waarabu lakini kinachomfanya arudi haraka ni kuogopa reaction ya Vatican maana balozi wa Vatican ni mwakilishi wa papa, FBI, CIA, M16 wote wana taarifa hizi, is not easy kama wafu wa CCM wanavyodhani.War against crusaders will never succeed in this country, kwanza nashangaa mpaka dakika hii JK hajaomba msaada wa FBI wakati aliyetaka kuuwawa ni Balozi wa nchi jambo ambalo lingeleta chaos kwenye International Community.
Kwa nini watu wana wadiwasi? Hawa waliokamatwa si mmoja wao alikamatwa na waumini wenyewe. Polisi walimwokoa tu kutoka kwenye kipigo. Hii ni kwa mujibu wa habari kwenye vyombo vya habari na watu waliokuwepo kwenye tukio. Sasa wasiwasi wa nini au ni kwa sababu jina lililotajwa siyo watu walilotarajiwa kulisikia. Ikiwa ni hivyo basi tunatembea na bomu vichwani mwetu. Inashangaza watu kumhukumu mtu kwa jina lake! Kumbuka unaweza kukuta mtu Mussa ni mkristu au mwislamu. Je na hakina Kingunge utawaweka wapi? Kwa ufupi jina la mtu halionyeshi dini yake su itikadi iliyo kicvhwani mwake.
 
Tumia akili yako ( kama unayo ) japo kidogo.....

Watuhumiwa waliokamatwa jumla ni 8 ni kwa nini jina linatajwa la mtuhumiwa mmoja!!?? Stuka.
 
mkuu mbona unalazimisha mambo wewe ukweli wako unaoujua basi wasaidie polisi vinginevyo wewe ni mhusika na kuna namna ulivyohusika kwa sababu utakuwa na kitu chako unachokijua na ulivyohusika.

Hoja yake namba 2 ina mashiko usibeze bure. Watu wanaoshikiliwa ni 6 kwanini jina la mmoja ndo litajwe? Na watano waliobaki wawe described tu? Kuna justification gani kwa kufanya hivi?
 
Kimkwete ana mikono ya damu. Hii damu itamtesa maisha yake. Asidhani ataishi kwa amani
 
Tumia akili yako ( kama unayo ) japo kidogo.....Watuhumiwa waliokamatwa jumla ni 8 ni kwa nini jina linatajwa la mtuhumiwa mmoja!!?? Stuka.
Sawa Mheshimiwa akili yangu niliyonayo inanielekeza kuwa jina si mwelekeo wa itikadi aliyo nayo mtu kichwani. Pia inanielekeza kuwa mtu anayetaka kutuchafua kwa swala la udini hawezi kutumia njia nyepesi za kututambulidha moja kwa moja.
 
Hivi mnajua kuna uwezekano wa raia wa kigeni kutupa bomu ili kutuchonganisha...hasa...wa upande ule..eastern
 
hao wengine majina yao ni nyaraka za sirikali hayarusiwi kuanikwa hadharani.

ni siri za taifa mkuu
wenyeakili tumemuelewa saaaana nchimbi
kuna dogo amelazwa yeye alimshuhudia.....mtuhumiwa ....sasa anachokisema nchimbi nadhani anamaanisha...........wakina pengo wegeuze shavu la pili.....inatia huruma saana...kwanini werekali ikurupuke??????ukiangalia bbc. Al jazera.....mkuu wa mkoa, rpc...nchimbi kauli zinapishana

tumuamini nani sasa?????
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa nini watu wana wadiwasi? Hawa waliokamatwa si mmoja wao alikamatwa na waumini wenyewe. Polisi walimwokoa tu kutoka kwenye kipigo. Hii ni kwa mujibu wa habari kwenye vyombo vya habari na watu waliokuwepo kwenye tukio. Sasa wasiwasi wa nini au ni kwa sababu jina lililotajwa siyo watu walilotarajiwa kulisikia. Ikiwa ni hivyo basi tunatembea na bomu vichwani mwetu. Inashangaza watu kumhukumu mtu kwa jina lake! Kumbuka unaweza kukuta mtu Mussa ni mkristu au mwislamu. Je na hakina Kingunge utawaweka wapi? Kwa ufupi jina la mtu halionyeshi dini yake su itikadi iliyo kicvhwani mwake.
UPUUZI kama huu wako unatia kichefuchefu!! Ni tukio gani ambalo serikali imelifanyia kazi watu waache kuwa na wasiwasi na hili!! I hate whitewashers!!!!!!!!
 
Nchimbi!! Nchimbi!! Sikia neno langu la kinabii kwako, ' ya kwamba nalikusikia ktk tamko lako juu ya mauaji ya Mwangosi na serikali yako kuiacha damu isiyo na hatia kumwagwa pasipo hata sheria kuchukuliwa dhidi ya waarifu. Nikakusikia tena, ktk hali ya ujasiri sana ukimdhalilisha mtumishi wa Mungu Mh. Mch Msigwa juu ya wizi wanyara za taifa.

Na leo pasipo woga unatoa tena tamko la utata ukionesha mtuhumiwa mkuu ni mkristo dhidi ya wakristo wenzie. Sasa utawala wako umefitinika na utawala uliofitinika hauwezi kudumu. Si muda mlefu, utaulizwa damu zinazomwagwa pasipo hatia-kwa kuwa Bwana ajua wewe ndo mwenye dhamana.
 
Hivi hili agizo liliondolewa kwenye Quran ? ''Fight those who do not believe in Allah, nor in the latter day, nor do they prohibit what Allah and His Apostle have prohibited, nor follow the religion of truth, out of those who have been given the Book, until they pay the tax in acknowledgment of superiority and they are in a state of subjection (Quran 9:29)''

Kama bado lipo ndani ya Quran basi hiyo ni sehemu ya Ibada kwa Muislam, kama hujui Uislam ni nini basi endelea kujifunza iko siku utajua lakini... ''Multiple Personality Disorder'' ni ugonjwa unaosababishwa na mafundisho ya kishenzi sana kwa upande mmoja na mafundisho ya busara kwa upande mwingine huku waumini wakitakiwa kuyafuata yote wakati wote
Idadi kubwa ya Waislam wale wabobezi kwenye dini wanaugua ugonjwa huu,hivyo kwao kitu chochote kinachofundisha chochote kilicho kinyume na Uislam wana haki ya kukiadhibu hata kwa kuua kizazi chote.
 
Baadhi ya wakazi mbalimbali mkoani Arusha wameanza kuingiwa na mashaka kama kweli serikali ina nia ya dhati na uwezo wa kushughulikia suala la mlipuko wa Bomu kanisani ambalo kwao wanaamini lina uhusiano mkubwa sana na chokochoko za kidini(Kwa sababu lililenga viongozi wakuu wa dini moja, waamini wa dini moja, limetokea kanisani, limeibuka kipindi hichi ambacho kuna fukuto la mivutano ya kidini hapa Tanzania).

Hii inatokana na juhudi mbali mbali za viongozi wa serikali na CCM kwa makusudi kuanza kukwepesha sehemu ya ukweli kuhusu hili ili llionekane ni tukio lenye msukumo wa kisiasa au kijamii(Uhalifu wa kawaida) na wala sio tukio lenye msukumo wa kiimani(Kidini), kwa mfano;

1/Kauli za harakaharaka za mfuatano zinazoshahabiana kutoka kwa viongozi wa juu wa serikali na CCM (RC wa Arusha Magessa Mulongo hapo jana na ambayo ilirudiwa pia na Nchimbi, Gharib Bilali nk) ya kuwa ''Suala hili ni uhalifu wa kigaidi tu na hatutegemei kama lina uhusiano wowote na mivutano ya Imani za kidini hapa Tanzania na wala tusijaribu kulihusianisha na mambo ya kidini''.

2/Kauli rasmi ya serikali kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani Emanueli Nchimbi ya kuwa jeshi la polisi limewakamata washukiwa Sita, na kumtaja mmoja tu kwa majina(Victor karist Ambrose) na kuacha kutaja washukiwa wengine.
Swali ni Kwanini huyo tu kawahi kutajwa kwa majina?

3/Juhudi za makusudi na lazima zinazofanywa sasa na WanaCCM mitandaoni(Zilianza saa chache sana toka tukio kutokea baada ya Kigogo mmoja wa CCM kuwapa amri hiyo) kutaka kuonyesha tukio hili lina msukumo wa kisiasa na limepangwa na chama fulani cha upinzani.

Hili ni kosa kubwa la kwanza kwa serikali katika kushughulikia uhalifu huu wa Arusha. Hakukuwa wala haikuwa BUSARA wala HEKIMA kutaja mtu mmoja na kuwaacha wengine waliokamatwa na wakati huohuo akihusisha tukio hilo na chokochoko za kisiasa na kidini!!. Ni bora angeishia kusema wamekamata watu kadhaa na polisi inaendelea kuwahoji.

Jioni hii nibehatika kufuatilia mjadala bungeni wa wizara ya mambo ya ndani.Moja ya michango iliyoni-touch ni wa Wabunge Zitto Kabwe(CHADEMA) na David Kafulila(NCCR-MAGEUZI).Hakika walitoa ushauri murua sana kwa serikali na akina Nchimbi juu ya migogoro ya kisiasa na ya kidini inayoendelea nchini kwa sasa ambayo pengine ndo inazaa matatizo kama hili la Arusha.Kama wanataka kutatua migogoro hii ya kijamii inayoendelea sasa ktk nchi yetu na kuepusha maafa zaidi,no bora wakauchukua na kuutumia ushauri wa hawa jamaa!!
 
Upuuzi wa kuleta masikhara katika vitu critical unatugharimu sana!
Sijui wanataka watu wafanye self defence?
 
I expected that. Hatuna viongozi ambao wako tayari kutatua matatizo ya aina hii. Inawezekana hawana uwezo au hawana nia au pengine wao wenyewe ni sehemu ya hizi hujuma. Ukitaka kulielewa hili tazama walivyoshughulikia matukio yaliyotangulia (padri huko Zanzibar, Daudi Mwangosi, Dr Ulimboka, Kibanda, kuchomwa makanisa n.k.)
 
Back
Top Bottom