BOMU LA ARUSHA: Serikali imeanza kucheza mchezo wa kisiasa?

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
552
Baadhi ya wakazi mbalimbali mkoani Arusha wameanza kuingiwa na mashaka kama kweli serikali ina nia ya dhati na uwezo wa kushughulikia suala la mlipuko wa Bomu kanisani ambalo kwao wanaamini lina uhusiano mkubwa sana na chokochoko za kidini(Kwa sababu lililenga viongozi wakuu wa dini moja, waamini wa dini moja, limetokea kanisani, limeibuka kipindi hichi ambacho kuna fukuto la mivutano ya kidini hapa Tanzania).

Hii inatokana na juhudi mbali mbali za viongozi wa serikali na CCM kwa makusudi kuanza kukwepesha sehemu ya ukweli kuhusu hili ili llionekane ni tukio lenye msukumo wa kisiasa au kijamii(Uhalifu wa kawaida) na wala sio tukio lenye msukumo wa kiimani(Kidini), kwa mfano;

1/Kauli za harakaharaka za mfuatano zinazoshahabiana kutoka kwa viongozi wa juu wa serikali na CCM (RC wa Arusha Magessa Mulongo hapo jana na ambayo ilirudiwa pia na Nchimbi, Gharib Bilali nk) ya kuwa ''Suala hili ni uhalifu wa kigaidi tu na hatutegemei kama lina uhusiano wowote na mivutano ya Imani za kidini hapa Tanzania na wala tusijaribu kulihusianisha na mambo ya kidini''.

2/Kauli rasmi ya serikali kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani Emanueli Nchimbi ya kuwa jeshi la polisi limewakamata washukiwa Sita, na kumtaja mmoja tu kwa majina(Victor karist Ambrose) na kuacha kutaja washukiwa wengine.
Swali ni Kwanini huyo tu kawahi kutajwa kwa majina?

3/Juhudi za makusudi na lazima zinazofanywa sasa na WanaCCM mitandaoni(Zilianza saa chache sana toka tukio kutokea baada ya Kigogo mmoja wa CCM kuwapa amri hiyo) kutaka kuonyesha tukio hili lina msukumo wa kisiasa na limepangwa na chama fulani cha upinzani.
 
Hilo si jambo geni kwa serikali hii ya ccm, hata marehemu Daudi Mwangosi waliudanganya umma wa watanzania kuwa ametupiwa bomu na wanachama wa Chadema, na wengine wakaenda mbali na kudai yeye (Mwangosi) alikuwa amejivika bomu alitaka kuwaua polisi.

Ni bahati nzuri tu kwamba zilitolewa picha zikiwaonyesha policcm wakimsulubu na hatimaye mmoja akaamua kumsambaratisha kwa bomu. Kwahiyo kwa hili tukio la Arusha hatuwezi kushangaa kuona ukweli unafichwa na propaganda zinatengenezwwa na kulishwa wananchi.
 
KAMA KUNA MTU BADO ANAKUMBUKA OMAR MAHITA NA 'TOROLI YA VISU VYENYE TOMATO SAUCE', KILE KINACHOITWA 'UGAIDI' JIJINI ARUSHA UNA MALENGO YA KISIASA KUGAWA JIJI HILO KIDINI KUNAKOELEKEA UCHAGUZI WA MADIWA. WaTanzania wala tusipumbazwe kama mazezeta hivi; hakuna cha(1) Sheikh Ilunga, (2) Al-Shabaab, (3) Al-Qaeda wala nani anayewadhuru wananchi kwa malengo ya kuleta hofu na hali ya kutokuaminiana kati ya Wakristo kwa Waislamu nchini. Kwa kufuatilia matukio ya 'Ugaidi wa Kuchonga' na matukio ya hivi karibuni jijini Arusha lazima ujiulize kwamba kati ya watajwa watatu hapo juu na (4) Serikali ya CCM, ni yupi kati ya wote mwenye kuweza KUNUFAIKA kisiasa na ulipuaji ovyo wa mabomu A-Tauni??????? Na kwa mtindo huo ndio maana kati ya michango yote juu ya tukio hili la kusikitisha sana, hakika nimeweza kumtambua mwenzetu huyu, Mkuu Lyamunda, kuwa kweli ni great thinker mwenye uwezo mkubwa kuona ujumbe ilioko nyuma ya ujumbe unaoonekana wazi kwa kila mtu. Ni masikitiko yalioje kuona jinsi gani serikali ya CCM inavyotumia dhana ya 'Ugaidi' kwa maslahi kisiasa kwa mtindo ambao sio kabisa. Wakristo kwa Waislamu kote nchini, tafadhalini kaeni mbali sana na hizi mbinu chafu za CCM na serikali yake kutumia hizi mbinu za ki-Nazi kutafuta kutugawa kwa misingi ya kidini kwa kutumia silaha yao mpya ya 'Ugaidi unaosimamiwa na vijana wake'. 'Gaidi wetu wa kuchonga' yuko ndani ya serikali hata kesho. Tena mbinu hizi zikiendelea zaidi basi huenda tukalizimika kutaja kwa majina baadhi ya vijana wa serikali ya CCM walipata kutumwaa Zanzibar miaka ya Mahita dhidi ya CUF kwa matukio kama haya haya.
Tokea mlipuko wa Arusha ulipotokea, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana habari hii, nimepelkea kuamini kuwa kwa sasa kuna dini mpya mbili amabazo ni hatari sana CHADEMA NA CCM!! haswa humu katika JF. anyway yana mwisho haya lkn kumbukeni kuwa tunaiuza nchi kwa bei rahisi sana!! Angalau nimefarijika kidogo kukutana na hii!! source ikiwa ni ZITO kabwe! #Nyufa........ Maadui hupita kwenye nyufa. #CUF ilipoitwa chama cha Waislam, hata watu wenye heshima nchini waliamini. Nyufa...... #CHADEMA ilipoitwa chama cha wakristo hata watu wenye akili wakaamini. Nyufa..... #Udini upo, #Udini haupo ni kauli za kupanua nyufa. Kama Taifa tuzibe nyufa hizi. Tukae tukiri makosa, tukatae kugawanywa. Maadui wanatumia nyufa hizi kuingia kubomoa Taifa hili. Tusome alama ukutani. Epuka kauli za chuki. Hate speeches must be made illegal. There is so much hate in our society now, in communities, within communities, against communities. We are a Nation- United Republic of Tanzania na kama huamini uhatari wa dini hizo mpya, basi endelea kufuatilia response ya wanajumuia hapa!! watu wanaabudu vyama kuliko UKWELI? yaani bila kujua wanauza kwa bei rahisi sana iwe kwa kauli au matendo yao, adui mkubwa hawamjui... Mola atuepushe na balaa...
 
Hilo si jambo geni kwa serikali hii ya ccm, hata marehemu Daudi Mwangosi waliudanganya umma wa watanzania kuwa ametupiwa bomu na wanachama wa Chadema, na wengine wakaenda mbali na kudai yeye (Mwangosi) alikuwa amejivika bomu alitaka kuwaua polisi.

Ni bahati nzuri tu kwamba zilitolewa picha zikiwaonyesha policcm wakimsulubu na hatimaye mmoja akaamua kumsambaratisha kwa bomu. Kwahiyo kwa hili tukio la Arusha hatuwezi kushangaa kuona ukweli unafichwa na propaganda zinatengenezwwa na kulishwa wananchi.
Tukio hili ni tofauti kabisa na matukio mengine, hakuna ujanja ujanja wowote utakaofanyika, ili ni shambulio dhidi ya Balozi halali anayewakilisha Vatican hapa Tanzania na target namba two ilikuwa ni Askofu.

Sasa basi licha ya kuwa JK alishamaliza ziara yake huko kwa Waarabu lakini kinachomfanya arudi haraka ni kuogopa reaction ya Vatican maana balozi wa Vatican ni mwakilishi wa papa, FBI, CIA, M16 wote wana taarifa hizi, is not easy kama wafu wa CCM wanavyodhani.

War against crusaders will never succeed in this country, kwanza nashangaa mpaka dakika hii JK hajaomba msaada wa FBI wakati aliyetaka kuuwawa ni Balozi wa nchi jambo ambalo lingeleta chaos kwenye International Community.
 
SERIKALI KUCHUA HATUA KALI MLIPUKO ARUSHA
Monday, 06 May 2013 Written by Mjengwa Blog Email Tuma Maoni

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Dkt.Emmanuel Nchimbi

Na Immaculate Makilika-Maelezo
SERIKALI imesema kuwa itachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi nafasi yake katika jamii kufuatia kuwepo kwa watu wachache wasiyoitakia mema nchi yetu kutaka kupandikiza chuki za kidini miongoni mwa Watanzania na kuleta mapigano, mauaji nchini
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu mlipuko wa uliotokea katika kanisa la katoliki la Mtakatifu Joseph Parokia ya Olasiti Arusha mjini Mei 5, mwaka huu saa 4:30 asubuhi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi 59, kati ya hao watatu ni mahututi.

Aliwataja watu waliofariki dunia kuwa ni Regina Kurusei mwenye wa miaka 45 mkazi wa Olasiti ambaye alifariki siku ya tukio wakati alipokuwa kipatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru na James Gabriel(16) aliyefariki usiku wa kuamkia leo.
"Tutachukua hatua kali bila huruma kuzigandamiza njama hizi mbaya dhidi ya taifa letu. Tutachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa letu kwanza," alisema Waziri Nchimbi.
Alisema tayari kikosi kazi maalumu kimeundwa ili kuchunguza tukio hilo.
Waziri Nchimbi alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mlipuko huo ni bomu. Hivyo uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania .
" Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na jeshi la polisi. Miongoni mwao ni Victor Ambroce mwenye umri wa miaka 20, dereva wa bodaboda,mkazi wa Mrombo, Arusha,ambaye anatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo. Watuhumiwa wengine watano waliokamatwa ni raia wane wa kigeni na Mtanzania mmoja ambao wanashikiliwa kwa maahojiano," alisema.
Aidha Waziri Nchimbi alisema Serikali inamewataka wanasiasa na viongozi wote wajiepushe na kauli zinazochochea ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki miongoni mwa Watanzania.
"Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za kisheria itakazozichukua dhidi ya viongozi wa aina hii ambao maslahi yao ni muhimu kuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania," alisisitiza huku akisema Serikali kwa nguvu zake zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wote waliohusika na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hilo wanasakwa popote walipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria..
Aliongeza kuwa kwa niaba ya Serikali anaungana na Watanzania kulaani wahusika wote wa tukio hilo walioshiriki kwa njia yoyote. Pia inawataka viongozi wa kisiasa, kidini,na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu.
Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya kuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia, mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Baba Mtakatifu, Askofu Fransisco Mantecillo Padilla. Aidha alikuwepo mwenyeji wake Askofu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu la Arusha.
Inakadriw a kuwa katika uzinduzi huo kulikuwa na watu zaidi 2000. Hivyo wakati mgeni rasmi akiwa ametoka nje akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi mtu aalirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu na baada ya kutua kulitokea kishindo na mlipuko mkubwa.
Katika tukio hilo viongozi wa Serikali na dini waliohudhuria ibada hiyo hawakupata madhara.
 
Chama fulani cha Siasa viongozi wake ndio wawe wa kwanza kuhijiwa
 
Hii sasa inavuka mipaka, ilikuwa makanisa sasa hivi inaenda hadi kwa waumini na viongozi wao.
 
Hii yote ni sababu ya woga wa chama cha magamba kuelekea uchaguzi wa madiwani hapo Arusha!!!Wanatafuta kisingizio cha kuvuruga uchaguzi ambao wanajua wazi watashindwa; hivyo kuficha aibu yao sasa wanawatumia watu wao walipue mabomu ili Arusha kuonekane hakufai kufanya uchaguzi!!!
 
Ni vyema wakalifahamu hili mapema, watanzania wa leo siyo wale wa miaka 47, wanajua kuchambua kati ya ukweli na propaganda. Endapo wamefanya hivyo kwa kuhofia uchaguzi wa madiwani, je watatumia hizo trick hata ifikapo 2015 ?

Kweli nimeamini hakuna awaye yeyote mwenye akili timamu ni mfuasi wa CCM.
 
Naungana na wanaosema hakuna propaganda za Ofisi ndogo Lumumba wala za Nchimbi , hii ni habari ya kimataifa , aliyelengwa ni Balozi wa Vatican hilo halina Ubishi , hawa wazee wa vitu vyenye ncha kali kwenye hili hawawezi , tuwaite FBI tujue mbivu na mbichi .
 
KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEA KATIKA KANISA KATOLIKI LA YOSEFU MFANYAKAZI PAROKIA TEULE YA OLASITI, ARUSHA MJINI, TAREHE 5 MEI, 2013.

Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, naomba kuwasilisha Taarifa yaawali kuhusu tukio la mlipuko uliotokea katika Kanisa Katoliki la MtakatifuJoseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013 saa4:30 asubuhi.

Mheshimiwa Spika,
mnamo tarehe 5 Mei, 2013 saa 4:30 asubuhikulitokea mlipuko katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Parokia ya Olasiti, jijini Arusha. Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada yakuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia. Mgeni Rasmi katika uzinduzialikuwa ni Balozi wa Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, AskofuFransisco Mantecillo Padilla. Aidha, alikuwapo mwenyeji wake AskofuJosephati Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha. Katika uzinduzi huoinakadiriwa kuwa kulikuwa na zaidi ya watu 2000. Wakati Mgeni Rasmiakiwa ametoka nje ya Kanisa akijiandaa kukata utepe kama ishara yauzinduzi mtu alirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu ambapo baada ya kutua kulitokeakishindo na mlipuko mkubwa. Mlipuko huo ulisababisha taharuki miongonimwa waumini na kusababisha watu kukimbia ovyo.

Mheshimiwa Spika,
katika tukio hilo watu wawili wamefariki duniaambapo REGINA LONGINO KURUSEI, Mwarusha, umri wa miaka 45, mkaziwa Olasiti alifariki dunia siku ya tukio wakati akipatiwa matibabu katikaHospitali ya Mount Meru na majeruhi mwingine JAMES GABRIEL umri wamiaka 16 amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 6 Mei, 2013. Aidha, watu 59 wamejeruhiwa na watatu kati yao ni mahututi. Majeruhi 38walikimbizwa hospitali ya Mount Meru kupatiwa matibabu. Majeruhi 16walikimbizwa hospitali ya St. Elizabeth kwa Father Babu, majeruhi mmojaalipelekwa hospitali ya Selian na majeruhi mwingine alipelekwa katikahospitali ya Dkt. Wanjara, Mianzini. Natumia fursa hii kutoa pole kwawafiwa, uongozi wa kanisa Katoliki, wakazi wa Arusha na Watanzania wotekwa tukio hili la kinyama. Aidha, nawaombea majeruhi wote wa tukio hilowapone haraka.

Mheshimiwa Spika,
Viongozi wa dini na Serikali waliohudhuria ibada hiyohawakupata madhara yeyote kufuatia mlipuko huo. Baada ya Jeshi la PolisiMkoa wa Arusha kupokea taarifa ya tukio hilo waliimarisha ulinzi kwakuongeza idadi ya askari katika eneo hilo. Aidha, Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha MheshimiwaMagesa Mulongo walifika eneo la tukio na kufanya tathimini ya hali ilivyona kuelekeza hatua za kuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika,
kutokana na uzito wa tukio hilo, kitaifa na kimataifa,Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Naibu Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Pereira A. Silima, na InspektaJenerali wa Polisi, Said A. Mwema walikwenda Arusha na walitembeleaeneo la tukio, waliwatembelea majeruhi na kuelekeza hatua za ziada zakuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika,
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mlipuko huoni bomu. Uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika unaendeleakufanywa na Jeshi la Polisi na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi waTanzania. Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi. Miongoni mwao ni Victor Calisti Ambrose mwenye umri wa miaka 20, dereva wa bodaboda, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha ambayeanatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo. Watuhumiwa wengine watanowaliokamatwa ni raia wanne wa kigeni na Mtanzania mmoja ambaowanashikiliwa kwa mahojiano.

Mheshimiwa Spika,
siku za karibuni kumekuwepo jitihada kubwa sana zawatu wachache wasiyoitakia mema nchi yetu kutaka kupandikiza chuki zakidini miongoni mwa watanzania na kuleta mapigano na mauaji miongonimwa watanzania, sina shaka kuwa shambulio la Arusha ni sehemu yamikakati hiyo miovu. Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa Serikalihaitavumilia hata kidogo mbegu za chuki za kidini miongoni mwawatanzania na tutachukua hatua kali bila huruma kuzigandamiza njama hizimbaya dhidi ya taifa letu. Tutachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujalihadhi na nafasi yake katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa letu kwanza.

Mheshimiwa Spika,
Pamoja na kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifawametoa maelekezo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo tayariInspekta Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Wakuu wa Vyombo vinginevya Ulinzi na Usalama wameunda Kikosi Kazi maalumu ili kuchunguza tukiohilo.

Mheshimiwa Spika,
kokote duniani, tukio la kushtukiza, linalosikitisha nakuhuzunisha kama hili linapotokea, wananchi wote huungana na kuwawamoja kama taifa na kulaani wahusika na kuwafariji waathirika wa tukiohilo. Nchini Marekani, Mgombea mmoja wa Urais wakati wa uchaguzi mkuuwa Mwaka 2012 aliishutumu Serikali kutokana na tukio la kulipuliwa kwaUbalozi wa Marekani nchini Libya. Ni wazi kuwa mgombea huyu alichukuatatizo lile kama ajenda ya kisiasa. Hata hivyo, alishutumiwa vikali naWamarekani wenzake kwa kuelezwa kuwa ni mtu mwenye kukosa kabisamisingi ya uaminifu na uzalendo kwa taifa lake (Fundamental dishonest).

Serikali inasikitishwa sana wanasiasa wa aina hii ambao wanajitokezanchini na kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa gharama za maisha yaWatanzania. Wanasiasa na viongozi wote wajiepushe na kaulizinazochochea ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki miongonimwa Watanzania. Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za kisheriaitakazochukua dhidi ya viongozi wa aina hii ambao maslahi yao ni muhimukuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu kuliko utulivu waWatanzania na maslahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania.

Mheshimiwa Spika,
kwa niaba ya Serikali naungana na Watanzaniawenzangu kulaani wahusika wote wa tukio hilo walioshiriki kwa njia yoyote.

Aidha, Serikali kwa nguvu zake zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wotewaliohusika na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hili wanasakwapopote walipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Tunawatakaviongozi wa kisiasa, kidini na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwanafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwakisiwa cha amani na utulivu.

Mheshimiwa Spika,
mwisho nawasihi Watanzania wawe watulivu wakativyombo vya dola vikiwasaka waliohusika na shambulio hilo, kila mwenyetaarifa za kuwezesha kukamatwa wahalifu hao atoe taarifa hizo kwa Jeshila Polisi. Aidha, ninawaomba Watanzania tuendelee kukataa vitendo vyauvunjifu wa amani katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

Source: wavuti.com - wavuti
 
There are times i feel ashamed kuwa MTANZANIA and ths is one of them moments!
 
SERIKALI KUCHUA HATUA KALI MLIPUKO ARUSHA
Monday, 06 May 2013 Written by Mjengwa Blog Email Tuma Maoni

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Dkt.Emmanuel Nchimbi

Na Immaculate Makilika-Maelezo
SERIKALI imesema kuwa itachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi nafasi yake katika jamii kufuatia kuwepo kwa watu wachache wasiyoitakia mema nchi yetu kutaka kupandikiza chuki za kidini miongoni mwa Watanzania na kuleta mapigano, mauaji nchini
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu mlipuko wa uliotokea katika kanisa la katoliki la Mtakatifu Joseph Parokia ya Olasiti Arusha mjini Mei 5, mwaka huu saa 4:30 asubuhi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi 59, kati ya hao watatu ni mahututi.

Aliwataja watu waliofariki dunia kuwa ni Regina Kurusei mwenye wa miaka 45 mkazi wa Olasiti ambaye alifariki siku ya tukio wakati alipokuwa kipatiwa matibabu katika hospitali ya Mount Meru na James Gabriel(16) aliyefariki usiku wa kuamkia leo.
"Tutachukua hatua kali bila huruma kuzigandamiza njama hizi mbaya dhidi ya taifa letu. Tutachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujali hadhi na nafasi yake katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa letu kwanza," alisema Waziri Nchimbi.
Alisema tayari kikosi kazi maalumu kimeundwa ili kuchunguza tukio hilo.
Waziri Nchimbi alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mlipuko huo ni bomu. Hivyo uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania .
" Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na jeshi la polisi. Miongoni mwao ni Victor Ambroce mwenye umri wa miaka 20, dereva wa bodaboda,mkazi wa Mrombo, Arusha,ambaye anatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo. Watuhumiwa wengine watano waliokamatwa ni raia wane wa kigeni na Mtanzania mmoja ambao wanashikiliwa kwa maahojiano," alisema.
Aidha Waziri Nchimbi alisema Serikali inamewataka wanasiasa na viongozi wote wajiepushe na kauli zinazochochea ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki miongoni mwa Watanzania.
"Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za kisheria itakazozichukua dhidi ya viongozi wa aina hii ambao maslahi yao ni muhimu kuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania," alisisitiza huku akisema Serikali kwa nguvu zake zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wote waliohusika na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hilo wanasakwa popote walipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria..
Aliongeza kuwa kwa niaba ya Serikali anaungana na Watanzania kulaani wahusika wote wa tukio hilo walioshiriki kwa njia yoyote. Pia inawataka viongozi wa kisiasa, kidini,na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa kisiwa cha amani na utulivu.
Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya kuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia, mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Baba Mtakatifu, Askofu Fransisco Mantecillo Padilla. Aidha alikuwepo mwenyeji wake Askofu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu la Arusha.
Inakadriw a kuwa katika uzinduzi huo kulikuwa na watu zaidi 2000. Hivyo wakati mgeni rasmi akiwa ametoka nje akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi mtu aalirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu na baada ya kutua kulitokea kishindo na mlipuko mkubwa.
Katika tukio hilo viongozi wa Serikali na dini waliohudhuria ibada hiyo hawakupata madhara.

Sijaelewa, kwanini jina la mtu 1 tu ndio linatajwa wakati walioshikiliwa na polisi ni watu 6? Nahisi kuna kamchezo kanataka kuchezwa hapa.
 
Baadhi ya wakazi mbalimbali mkoani Arusha wameanza kuingiwa na mashaka kama kweli serikali ina nia ya dhati na uwezo wa kushughulikia suala la mlipuko wa Bomu kanisani ambalo kwao wanaamini lina uhusiano mkubwa sana na chokochoko za kidini(Kwa sababu lililenga viongozi wakuu wa dini moja, waamini wa dini moja, limetokea kanisani, limeibuka kipindi hichi ambacho kuna fukuto la mivutano ya kidini hapa Tanzania).

Hii inatokana na juhudi mbali mbali za viongozi wa serikali na CCM kwa makusudi kuanza kukwepesha sehemu ya ukweli kuhusu hili ili llionekane ni tukio lenye msukumo wa kisiasa au kijamii(Uhalifu wa kawaida) na wala sio tukio lenye msukumo wa kiimani(Kidini), kwa mfano;

1/Kauli za harakaharaka za mfuatano zinazoshahabiana kutoka kwa viongozi wa juu wa serikali na CCM (RC wa Arusha Magessa Mulongo hapo jana na ambayo ilirudiwa pia na Nchimbi, Gharib Bilali nk) ya kuwa ''Suala hili ni uhalifu wa kigaidi tu na hatutegemei kama lina uhusiano wowote na mivutano ya Imani za kidini hapa Tanzania na wala tusijaribu kulihusianisha na mambo ya kidini''.

2/Kauli rasmi ya serikali kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani Emanueli Nchimbi ya kuwa jeshi la polisi limewakamata washukiwa Sita, na kumtaja mmoja tu kwa majina(Victor karist Ambrose) na kuacha kutaja washukiwa wengine.
Swali ni Kwanini huyo tu kawahi kutajwa kwa majina?

3/Juhudi za makusudi na lazima zinazofanywa sasa na WanaCCM mitandaoni(Zilianza saa chache sana toka tukio kutokea baada ya Kigogo mmoja wa CCM kuwapa amri hiyo) kutaka kuonyesha tukio hili lina msukumo wa kisiasa na limepangwa na chama fulani cha upinzani.

mkuu mbona unalazimisha mambo wewe ukweli wako unaoujua basi wasaidie polisi vinginevyo wewe ni mhusika na kuna namna ulivyohusika kwa sababu utakuwa na kitu chako unachokijua na ulivyohusika.
 
Tukio hili ni tofauti kabisa na matukio mengine, hakuna ujanja ujanja wowote utakaofanyika, ili ni shambulio dhidi ya Balozi halali anayewakilisha Vatican hapa Tanzania na target namba two ilikuwa ni Askofu.

Sasa basi licha ya kuwa JK alishamaliza ziara yake huko kwa Waarabu lakini kinachomfanya arudi haraka ni kuogopa reaction ya Vatican maana balozi wa Vatican ni mwakilishi wa papa, FBI, CIA, M16 wote wana taarifa hizi, is not easy kama wafu wa CCM wanavyodhani.

War against crusaders will never succeed in this country, kwanza nashangaa mpaka dakika hii JK hajaomba msaada wa FBI wakati aliyetaka kuuwawa ni Balozi wa nchi jambo ambalo lingeleta chaos kwenye International Community.
Je LUKUVI hawa ws tukio la Arusha nao ni wahuni kams ulivyo ongea hivi karibunu??
 
baadhi ya watu wanachochea vurugu halafu wao ndiyo wa kwanza kuanza kulaumu na kujijenga kisiasa kitu ambacho ni kibaya sana.
 
Baadhi ya wakazi mbalimbali mkoani Arusha wameanza kuingiwa na mashaka kama kweli serikali ina nia ya dhati na uwezo wa kushughulikia suala la mlipuko wa Bomu kanisani ambalo kwao wanaamini lina uhusiano mkubwa sana na chokochoko za kidini(Kwa sababu lililenga viongozi wakuu wa dini moja, waamini wa dini moja, limetokea kanisani, limeibuka kipindi hichi ambacho kuna fukuto la mivutano ya kidini hapa Tanzania).

Hii inatokana na juhudi mbali mbali za viongozi wa serikali na CCM kwa makusudi kuanza kukwepesha sehemu ya ukweli kuhusu hili ili llionekane ni tukio lenye msukumo wa kisiasa au kijamii(Uhalifu wa kawaida) na wala sio tukio lenye msukumo wa kiimani(Kidini), kwa mfano;

1/Kauli za harakaharaka za mfuatano zinazoshahabiana kutoka kwa viongozi wa juu wa serikali na CCM (RC wa Arusha Magessa Mulongo hapo jana na ambayo ilirudiwa pia na Nchimbi, Gharib Bilali nk) ya kuwa ''Suala hili ni uhalifu wa kigaidi tu na hatutegemei kama lina uhusiano wowote na mivutano ya Imani za kidini hapa Tanzania na wala tusijaribu kulihusianisha na mambo ya kidini''.

2/Kauli rasmi ya serikali kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani Emanueli Nchimbi ya kuwa jeshi la polisi limewakamata washukiwa Sita, na kumtaja mmoja tu kwa majina(Victor karist Ambrose) na kuacha kutaja washukiwa wengine.
Swali ni Kwanini huyo tu kawahi kutajwa kwa majina?

3/Juhudi za makusudi na lazima zinazofanywa sasa na WanaCCM mitandaoni(Zilianza saa chache sana toka tukio kutokea baada ya Kigogo mmoja wa CCM kuwapa amri hiyo) kutaka kuonyesha tukio hili lina msukumo wa kisiasa na limepangwa na chama fulani cha upinzani.

shida ya ccm na serikali yao ni hii, matukio yanatokea tayari wana majibu hata kabla ya upelelezi. Na tayari wameshajipanga mitandaoni kutetea na kuanza kuhusiha na siasa za chama hasa cdm.kwanini waziri na serikali yote inawahi kutuelekeza kuwa lile ni tukio la kawaida la kigaidi halihusiani na dini bila hata upelelezi? Au walijua kinachoendelea?
 
Kama ni mchezo wa kisiasa basi ccm Ndio wanaucheza na hakuna kitu kinaumiza Kama watu mnamsiba na majonzi mtu analeta Kauli za kebehi tumuombe Mungu atuepushe na haya majanga
 
Back
Top Bottom