Bomu la ajira

Unataka kusema nini? Yaani kama hakuna kuajiriwa watoto wasisomeshwe?

Ndugu “education is liberation of your mind and information is opportunity “

Usingojee serikali ikusomeshe au kukupa kazi!
 
Tuweke record hao walimu 91elfu ni walio tuma maombi tu kwa kozi za Sanaa, hiyo haimaanishi kwamba MTAANI Kuna walimu 91elfu tu ambao hawana ajira
 
Pambaneni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ifike kipindi tuache porojo na kiki za kijinga mtaani hali ni mbaya sana degree holder za fani hiyo ni kama wamepoteza dira kabisa na mtukufu haonyeshi kabisa kujari hii sio sawa kabisa kama ni hivyo TCU wafute bas hiyo kozi.
 
Wanajenga stigler goji na standard geji.....wakati kule Madimba kuna shule ina mwalimu 1.

John Stone ni chizi sana.

Sent using my Nokia Torch
 
Enzii za Mwalimu woteee.mnapata shule,ajira na tiba....na wote mmepitia JKT....akukuwa na Udini wala Ukabila🤣🤣.Leo hii Rwanda wanafuata Hazimio la Arusha...sisi tunabaguana kivyama.....kama chama chako kinakubalika na Watanganyika nini tatizo...mpaka utumie vijana waliopita CCP🤣🤣🤣
 
Unataka kusema nini? Yaani kama hakuna kuajiriwa watoto wasisomeshwe?

Ndugu “education is liberation of your mind and information is opportunity “

Usingojee serikali ikusomeshe au kukupa kazi!
Education is not matter b'se we have already, what is matter is kind of education we give them and conducive environment for our graduates to be employed or to employ themselves.
 
About 90% ya tuliopata elimu ya chuo kikuu tunafikiria kuajiriwa tu kwasababu elimu ya chuo kikuu, ukiondoa ualimu, ni kumuandaa mtu kuja kuwa afisa ambaye kazi yake ni ya ofisini sana pamoja na kupanga mipango na kisimamia/ kuwapangia kazi watu wa chini.
Kwahiyo tunapokosa ajira inakuwa tatizo kubwa sana.
Kwa mfano mtu aliyesoma finance, food science, microbiology, chemistry, geology n.k hawezi kujiajiri kutokana na zile opportunity zinazopatikana kwenye hizo areas kuhitaji mitaji mikubwa sana na hivyo anajikuta akishindwa kujiajiri katika fani aliyosomea.
Na kuna wengine wanadai kwamba tujiajiri kwenye shughuli kama kilimo, ufugaji na biashara, lakini mimi naona si sawa. Moja ya sababu ni kwamba ,watu wengi wanaofanya hizo shuguli ni watu ambao wana elimu ya form four, std 7 au hawana elimu kabisa. Sasa kulikuwa na ulazima gani wa mm kusoma hadi chuo kikuu na wakati kazi nitakayofanya haihitaji elimu yoyote. Pia lazima kuwe na mgawanyo wa kazi katika jamii, sasa kama mm niliwaacha wenzangu( walioishia lasaba na form four) wanachoma chips au wanafanya kazi yoyote, na mm baada ya kutoka chuo nakuja kufanya kazi ileile. Hapo nakuja kuwapunguzia kipato kwa kugombania wateja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuweke record hao walimu 91elfu ni walio tuma maombi tu kwa kozi za Sanaa, hiyo haimaanishi kwamba MTAANI Kuna walimu 91elfu tu ambao hawana ajira
Na bomu linakuja wanaomaliza mwaka ujao maana ni wengi sana. Kama udsm mwaka 2017 walichukua wanafunzi 14000 kwa mwaka wa kwanza, wakati mwaka 2015 walichukuliwa 5000+ .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipaumbele chețu ni kunuñua ndege cash
Basi jiwe weka mazingira mazuri ya PPP mbona hutaki sekta binafsi itamalaki hatimaye kuwe na ajira?umeumbwa na roho ya uharibifu he hujioni kama wewe ndo tatizo?ukimaliza miaka kumi bila kubadilika hakika wananchi wengi watakua wamerudi nyuma zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka kusema nini? Yaani kama hakuna kuajiriwa watoto wasisomeshwe?

Ndugu “education is liberation of your mind and information is opportunity “

Usingojee serikali ikusomeshe au kukupa kazi!
Serikali inatakiwa iweke mazingira mazuri ya watu kujitegemea. Hii ya sasa yenyewe ndo inawekea vikwazo watu wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukiwa serious kwenda kwenye uchumi wa kati KILIMO cha KIBIASHARA ni inevitable.
Tatizo liko wizara ya fedha kuna watu wanawaza kodi tu bila kujua kodi ni outcome ya uzalishaji, procurement of goods & services spending.
Mathalani, tukiwa na serious industrial farming ya pamba, (maana yake) value chain ya kupata vitambaa au nyuzi na mafuta kama end products,
hapo kati kati chemists wataingia kutengeneza madawa ya pamba
watu wa masoko watauza products, wahasibu wataingia ku-manage finances, storage nao wamo. Legal wanaingia kwa ajiri ya mikataa ya mauziano au namna gani mikopo ipatikane kiwanda ku-expand.Food science wanaingia kwenye kutengeneza mafuta ya kula.
Watu wakipata fedha, wataingia uwanjani kuangalia soka.
Agribusiness iko very inclusive. Wanasiasa wetu wana advocate kwa kilimo cha kujikimu.

Naomba niwe mkweli, Wizara ya fedha ina watu hawajui mipango ya kimkakati kukuza uchumi kwa haraka. Wanadhania uchumi ni kuwekeza kwenye miradi ya mikubwa pekee ambayo Return on investment takes forever.
 
Ujasiriamali hausomewi mkuu, haimake sense mwalimu wa ujasiriamali kufundisha hilo somo wakati anastruggle na maisha magumu.
Marekani hata China ukisema entrepreneurs ni watu kama akina Steve Jobs, Bill Gates, Mark Zuckerberg, Jack Ma hata Jeff Bezoz... they used their brain to create or and innovate new business. Kwetu hapa wauza mitumba ndio barabarani tunadhania hao ndio.
Na mara nyingi mambo haya ya kuja na tafsiri za kukoteleza hufanywa na watu ambao sijui huwa wanawaza nini.

Tunge-breed hao watu nchi ingepata hela in return. Mpaka sasa TRA haina imani na biashara inayoweza kuanzia sebuleni kwa mtu. Wao ili wakupe TIN lazima walambe na hela ya pango.
Jeff Bezoz kaanzisha Amazon kwenye sehemu ya kuengeshea gari katika nyumba ya mtu na laptop yake yenye internet.

Mungu tusaidie Watanzania
 
Jiwe hana maono ya wapi nchi anataka kuipeleka, sasa ukimwambia afanye kama watangulizi ni sawa na kumchoma kwenye kidonda.

Unafikiri atakuwa anazungumzia nini ikiwa uchumi umemshinda, tatizo la ajira kalitengeneza kubwa zaidi baada tu ya kuingia madarakani.

Jiwe hata kama akifanya hivyo atakuwa hana lolote jipya la kuwaeleza Watanzania zaidi ya stori zile zile za kila siku ndege, sgr, tuibiwa sana, nchi tajiri hii, wapo watu wanakwamisha serikali yangu (Tundu Lissu) n.k hapo amekuwa amemaliza hotuba, na akiendelea zaidi ya hapo ni kutukana Watanzania.
 
Hi
Tuweke record hao walimu 91elfu ni walio tuma maombi tu kwa kozi za Sanaa, hiyo haimaanishi kwamba MTAANI Kuna walimu 91elfu tu ambao hawana ajira
Hili la walimu 91000 ni kama robo tu ya walio mtaani. Kuna waalimu wengi sana mtaani mpaka huruma.
Bora hata hao walimu kuna watu kama sociology,business admn, banking na chungu mzima wako kitaa.
Kuna watu walioachishwa kazi kwenye makampuni yaliyofungwa wengi wao nao ajira hakuna.
Kwa mara ya kwanza nimeona kwa macho yangu mtu mwenye cpa akilazimika fanya kazi ya 400k.
Kadri siku zinavyozid na private sectors zinaamua kupunguza mishahara sabab ya competition ya ajira. Najiuliza baada ya 2020 tutaishije?
 
Kwa kweli aisee
 
Hivi kama mishahara inapungua what about their pension plan?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…