Tanzania ni nchi tajiri lakini watu wake ni masikini tena wengi wetu ni masikini wa mali na akili. Hata huyo mtawala aliyetangulia na kuleta kinachoitwa 'ukuaji wa uchumi' ni kuwa ameshusha idadi ya waliokuwa na uwezo kiuchumi na kuiongezea idadi ndogo sana isiyozidi 2% utajiri wa kupindukia!
Sasa ninachoangalia hapa ni kuwa zoezi hili litaongeza sio masikini bali mafukara, maana hapa tunakuja kuwa na mtu asiye na huakika wa mlo mmoja tofauti na awali ambapo huyu huyu alishinda na njaa lakini alikuwa na pa kulaza ubavu wake lakini leo hatakuwa hata na makazi.
Swal ni je, kama Mh. JPM katika siku zake 100 ataweza kutengeneza idadi hii ya mafukara itamchukua muda gani kutengeneza utajiri/matajiri na kufanya replacement ya hawa. Najikumbusha juu ya 'maisha bora kwa kila Mtz'.