VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Tarehe 5/1/2016 imepiga hodi. Imefika. Bomoabomoa kurudi tena kuanzia kesho. Usiku wa leo, wakaazi wenye nyumba zenye alama ya 'X' hawatalala usingizi. Utakuwa usiku mfupi na usio na ladha ya pipi. Usiku wa kusubiri kubomolewa makazi.
Leo, usiku utakuwa wa kujiulizauliza na kujiandaa kujiliza hapo kesho na kuendelea. Usiku wa kukumbukwa. Usiku wa kuwaza kilichotokea hadi kitakachotokea kuanzia kesho. Usiku wa leo, watailaumu na kuilaani Serikali na watendaji wake wote bila mafanikio.
Utakuwa usiku wa kujiapiza na kupania kutochagua tena hawa mwaka 2020. Lakini, usiku utasahaulisha kuwa watanzania ni wepesi wa kusamehe na kusahau. Waungwana. Kesi kujaribu kusimamisha ubomoaji huo inaunguruma muda huu Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi. Jaji Kente amebaki mwokozi pekee.
Usiku mfupi na wa kuweka kwenye diary!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Last edited: