Bomoabomoa Dodoma imenihuzunisha sana.

Magombelema

Member
Oct 11, 2011
15
4
Nimeumizwa na kitendo cha serikali kuwabomolea wananchi jumbazao huko dodoma eti kumpisha mwekezaji.Nimemsikia mama mmoja kwenye taarifa ya habari ya ITV akilia baada ya nyumba yake kuvunjwa huku akisema amani Tanzania haipo.Hii inamaana gani?
 
Safi sana, wanachi waache kuvamia maeneo kwa kisingizio cha serikali itawalinda.
 
mkuu Magombelema, unashangaa kusikia mwananchi akihoji amani tulio nayo hapa tanganyika..je ni swali geni kwako kulisikia, je wewe uko kisiwa gani,tanganyika hakuna amani kuna utulizu na uoga wa kijinga...
 
sinana interprises VS WANANCHI WA NJEDENGWA.
Mahakama ilitoa Notisi ya siku 14,wabomoe waondoke.
Mfupa huo Mh lukuvi aligonga mwamba,Msekela aligonga mwamba,Dr nchimbi kakurupuka.

Ua mtu mmoja wengi wakae kwa amani,na si ua wengi mmoja akae kwa amani.
TBC Hawajawataja Marehemu au wamefufuka,
 
Habari wana jamvi,
Wakazi hawa kupata haki yao ilikuwa ndoto ya mchana.kuna mtu anaitwa MAIMU. Huyu ndiye kivuli cha kazi yote ya jana.

Ukiwa unatoka dsm kuja dodoma mkono wa kushoto kuna yard kubwa ya matreka ya power tila.hili eneo kwa nyuma yake ndo zahama hii ilipotoke.
Huyu MAIMU ndo anatumika lakini nyuma yake yupo AGREY MWANRI,anayemtumia huyu bwana kufanikisha mambo yake ili yeye asijulikane.

Kumbuka hata matreka yaliyopo hapo yard ni dili la mwanri kwa best yake maimu.
Raia waliofukuzwa na kuvunjiwa ili kupisha ujenzi wa shule ya bwana MAIMU unabaraka za n.waziri AGREY MWANRI.

Kwaiyo hapa kuwa tunalalamika haiwezi saidia.
 
Safi sana, wanachi waache kuvamia maeneo kwa kisingizio cha serikali itawalinda.

Watu wanapojenga ovyo serikali inawajibika, lazima iseme ilikuwa wapi wakati wakati watu wanajenga bila kibali katika maeneo yasiyoruhusiwa, kwanini isiwazuie kujenga na kuona kubomoa ni vizuri zaidi. Lazima ikubali responsibilty, si haki kuwaumiza wananchi kwa makosa ya pande mbili.
 
Hao watu hawakuanza leo huo Ujenzi,
Tuseme hizo nyumba hazikuibuka tu kama uyoga watu wakazikuta asubuhi zishajengwa!!
Zimeanza kujengwa taratibu mpaka zikafikia hapo Serikali ya Chama "Twawala" ikiangalia tu.
Tena kuna mdada mmoja alidai alikwenda mpaka Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kuomba kibali cha ujenzi na akaelekezwa mpaka wapi Mlango uelekee.
Leo wabakuja kuwavunjia kinyama namna hii, hakika ni u-Ghaddaf wa hali juu.
Wale wananchi ukiwaangalia ni maskini tu hata kabla hawajabomolewa.
Serikali inayotakiwa kuwasaidia kuondokana na umaskini ndio inazidi kuwatia kwenye umaskini uliokithiri.
Hivi kwa mnaoijua Dododma ni ndogo kiasi gani mpaka iwe imejaa kiasi cha huyo mwekezaji kukosa eneo jingine mpaka iwe lazima apewe hapo kwenye makazi ya wananchi?
Si angetafutiwa eneo jingine tu??!!!
Ghaddaf aliewaua Raia wake walioandamana kwa kwa kuwakanyaga na tingatinga,
Na hawa waliotumia tingatinga kuwabomolea wananchi waliokua wakijiendeshea maisha yao kwa shida hivyohivyo, nani katili?
Kama sikosei Dodoma ni mkoa ambao hakuna hata mbunge mmoja wa upinzani,
Hayo ndio malipo yenu kwa wananchi hao?!!
Iko siku tu!!!
 
Habari wana jamvi,
Wakazi hawa kupata haki yao ilikuwa ndoto ya mchana.kuna mtu anaitwa MAIMU. Huyu ndiye kivuli cha kazi yote ya jana.

Ukiwa unatoka dsm kuja dodoma mkono wa kushoto kuna yard kubwa ya matreka ya power tila.hili eneo kwa nyuma yake ndo zahama hii ilipotoke.
Huyu MAIMU ndo anatumika lakini nyuma yake yupo AGREY MWANRI,anayemtumia huyu bwana kufanikisha mambo yake ili yeye asijulikane.

Kumbuka hata matreka yaliyopo hapo yard ni dili la mwanri kwa best yake maimu.
Raia waliofukuzwa na kuvunjiwa ili kupisha ujenzi wa shule ya bwana MAIMU unabaraka za n.waziri AGREY MWANRI.

Kwaiyo hapa kuwa tunalalamika haiwezi saidia.
KAKA NIMEKUELEWA TENA YARD ILE IPO ROAD LISEVU....LKN HANA X YA MAGUFULI,nilikwa najiuliza MAIMU katoa wapi ubavu huo...kmbe ypo huyo mwizi wa kaskzn.....
RPC hajui alikuwa KUPOKEA KIBATARI CHA UHURU CHAMWINNO
 
sinana interprises VS WANANCHI WA NJEDENGWA.
Mahakama ilitoa Notisi ya siku 14,wabomoe waondoke.
Mfupa huo Mh lukuvi aligonga mwamba,Msekela aligonga mwamba,Dr nchimbi kakurupuka.

Ua mtu mmoja wengi wakae kwa amani,na si ua wengi mmoja akae kwa amani.
TBC Hawajawataja Marehemu au wamefufuka,

dr nchimbi angeendelea kufundisha tu!hapo udsm!
 
anaharibu personality,alitutelekeza darasani,akaufuata ukuu wa wilaya!leo hii wakaz wali0vunjiwa nyumba wanamzungumziaje?so sad

Duh mdau umenikumbusha huyu mama dept.ya HI. Mbona alikuwa anaeleweka sana ila tamaa sijui au kutoelewana na akina Tambila,George,Kaizirege etc
 
Back
Top Bottom