Bomoa bomoa Morogoro road, ni kweli wananchi wameonewa?

Bomoa bomoa Morogoro road, ni kweli wananchi wameonewa?

Umenena jambo jema nami ni muhanga ila nimeshidwa cha kuchangia maana wewe umemaliza yote.mimi miaka mi tatu iliyopia walipita watu wa tanroads na bahati nzuli walinikuta mwenyewe Dukani na wakaniuliza baazi ya maswali na nilipowajibu wakachukua no ya mwenye flemu maana mimi nilikua mpangaji,kaukweli niliwahoji watu wale walinieleza ukweli nami nilikua nalipa kodi kimachalemachale na niliachana napo mwaka huu .wale watu wa tanroads walinielekeza jiwe lilipo na kweli lipo mita 121 na sijui kwanini hizi kesi hazikua muda huo wote maana nijuavyo kesi nyingi wananchi walishindwa .na sio kimara mpaka kibamba tu ni mpaka kiluvya nazani si mmeona kilichotokea kibaha maili moja?hadi kituo cha police kimebomolewa je ni uonevu?
Well said mkuu.
Taifa linahitaji watu kama wewe ambao wanasimamia Ukweli na Uwazi.
Kuna watu wanapotosha umma na kumwaga sumu ya Chuki,ukabila na uzandiki sijui kwa manufaa gani!
Nashukuru sana mkuu kwa kuuweka ukweli wa suala husika upenuni.
 
Kama hawajaonewa nilitegemea jengo LA TANESCO pale Ubungo liwe la kwanza kuvunjwa maana lipo ndani ya hifadhi ya barabara kuliko hizo nyumba za walalahoi zinazobomolewa na TANROADS
 
Well said mkuu.
Taifa linahitaji watu kama wewe ambao wanasimamia Ukweli na Uwazi.
Kuna watu wanapotosha umma na kumwaga sumu ya Chuki,ukabila na uzandiki sijui kwa manufaa gani!
Nashukuru sana mkuu kwa kuuweka ukweli wa suala husika upenuni.
Fanya uchunguzi utaona watu wengi wanaobomolewa hawakupewa hati na hawakua wanalipa kodi ya majengo na hata wenye hati walipita kiujanja ujanja na Mzee wangu alihangaika kupata hati alinyimwa coz eneo sio rasmi.na watu wanasema niwanyonge wengi wenye maeneo ni mchanganyiko wengine wanauwezo mkubwa.
 
Umeandika na kuwasilisha vyema sana mkuu.
Watanzania tumejaa na kuongoza kwa UNAFIKI.
Hatutaki kuishi maisha yetu kwa kufuata taratibu,kanuni na sheria. Kinachoshangaza zaidi kwani hili suala la BOMOA BOMOA hapa nchini limeanza katika hilo eneo la Kimara tu!?
Mbona kuna watu walibomolewa nyumba zao awamu zilizopita na mpaka mwanzo wa awamu hii ya tano!
Watu wa Buguruni mbona wameendelea na maisha yao. Kunduchi mtongani mbona lilipita greda!?
Kwa nini baadhi ya wakazi wa Kimara wanajiona wao hawagusiki (untouchables). Miaka ya nyuma baba yangu mzazi na familia yangu tulivunjiwa nyumba msasani kipindi kileee. Nafikiri unakumbuka hili mkuu ilitokea miaka ya themanini. Watu walivunjiwa nyumba maeneo ya msasani. Lakini maisha yaliendelea.

Leo hii watu kila kitu wanataka kuingiza siasa tu. Sumu ya chuki na ukabila ni mbaya sana.
Ndio maana moja ya sheria za ardhi zinasema ardhi yote ya Tanzania iko chini ya uangalizi wa Rais.
Hata kama umenunua kiwanja chako na kujenga, Mh. Rais ana mamlaka ya kufuta umiliki wa ardhi husika.
Kiwanja ni chako lakini madini yakigunduliwa chini ya ardhi si mali yako.
Kama kuna mradi wa Maendeleo unahitajika kupita hapo kwa manufaa ya Taifa na Watanzania kwa ujumla serikali kupitia vyombo vya mamlaka wana haki kisheria ya kukuondoa hapo iwe kwa hiyari au kwa nguvu.

Safi sana Mkuu. Nimependa pia uwasilishaji wako. Mimi nimeshazoea ' Kunyoosha ' tu maelezo na sipendi ' Unafiki ' hivyo watakaoguswa na mitazamo yetu watusamehe tu.
 
Umenena jambo jema nami ni muhanga ila nimeshidwa cha kuchangia maana wewe umemaliza yote.mimi miaka mi tatu iliyopia walipita watu wa tanroads na bahati nzuli walinikuta mwenyewe Dukani na wakaniuliza baazi ya maswali na nilipowajibu wakachukua no ya mwenye flemu maana mimi nilikua mpangaji,kaukweli niliwahoji watu wale walinieleza ukweli nami nilikua nalipa kodi kimachalemachale na niliachana napo mwaka huu .wale watu wa tanroads walinielekeza jiwe lilipo na kweli lipo mita 121 na sijui kwanini hizi kesi hazikua muda huo wote maana nijuavyo kesi nyingi wananchi walishindwa .na sio kimara mpaka kibamba tu ni mpaka kiluvya nazani si mmeona kilichotokea kibaha maili moja?hadi kituo cha police kimebomolewa je ni uonevu?

Safi sana Mkuu ngoja tuendelee tu Kuwanyoosha kwa kuwapa ukweli na wengine bahati mbaya sana mishipa yetu ya Unafiki ilikatwa pale pale Wodi ya Uzazi wakati tunazaliwa miongo mitatu na nusu iliyopita.
 
Mimi nilinunua kibanda changu 2007, madalali wakaonyesha dalili ya kudhulumiana mmoja aliyekosa Dili akasema kwa sauti "kwanza mnamuuzia barabarani" mimi sikuipuuza Ile sauti wale wengine wakaanza kujitetea kwa kueleza mpaka halisi utakapopita.
Nikaenda serikali za mtaa Pamoja na Kwa mjumbe kujiridhisha ni kweli wakanionyesha nyumba itakayokuwa ya mwisho na walishaambiwa wasiendeleze Huko.
Miaka 10 baadae (Yaani juzi) bomoabomoa imepita na watu wanapaza sauti.
 
Nilibahatika kumsikiliza msemaji wa TANROADS alisema road reserve inavary kulingana na sehemu,akataja kuanzia clock tower mpaka 4km umbali ni 15m pande zote,kuanzia 4km mpaka 10km umbali ni 30m,10km mpaka 20km umbali ni 121m,kuanzia 20km mpaka 30km umbali ni 90m,then 60m then 30m mpaka morogoro.

[emoji115]Hiyo ni morogoro road tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu zuri pekee ilitakiwa tulipate kupitia mahakama...kinachoonekana TANROADS wanavizia hawataki hata kusubiri maamuzi ya mahakama chombo pekee ambacho kingetafsiri hizo sheria
 
Mimi nilinunua kibanda changu 2007, madalali wakaonyesha dalili ya kudhulumiana mmoja aliyekosa Dili akasema kwa sauti "kwanza mnamuuzia barabarani" mimi sikuipuuza Ile sauti wale wengine wakaanza kujitetea kwa kueleza mpaka halisi utakapopita.
Nikaenda serikali za mtaa Pamoja na Kwa mjumbe kujiridhisha ni kweli wakanionyesha nyumba itakayokuwa ya mwisho na walishaambiwa wasiendeleze Huko.
Miaka 10 baadae (Yaani juzi) bomoabomoa imepita na watu wanapaza sauti.
Una Bahati sana wewe, kuna jamaa kanunua kajenga ghorofa akamshawishi mwenzake anunue jamaa akakataa akajenga nyuma sana, sasa ghorofa linabomolewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
upload_2017-8-27_9-16-0.png

upload_2017-8-27_9-12-49.png

upload_2017-8-27_9-14-13.png
 
Back
Top Bottom