Habari wadau wote wa jamii forum, nipende kutoa pole kwa wale wote ama ndugu ama jamaa waliokumbwa na kadhia hii ya bomoa bomoa.
Binafsi sielewi chochote kuhusu sheria, hasa hizi za barabara, naomba niulize, ni kweli wananchi wameonewa na hii bomoa bomoa ama ni haki ya serikali?
kwa maana serikali(TANROADS) inatumia sheria ipi kubomoa hizi nyumba.
kwa maana nijuavyo barabara ya Morogoro ni barabara ya mkoa, sasa iweje tu wabomoe Kimara hadi Kibamba?
kama huo upanuzi unahusu tu Kimara na Kibamba, inamaana na watu wa mikoa mingine walio hizo mita za barabara kuu kama wakazi wa kimara na kibamba nao wana makosa na watabomolewa siku yeyote ile?
mwisho napenda kuwaomba, mwanaJF yeyote yule anayejua sheria zinazohusu barabara aziweke hapa jukwaani(vielelezo, attachment, file, pdf etc) hasa hiyo sheria ya mita sijui 121 iliyotumika kuwabomolea wakazi wa kimara, kibamba?
Sababu tunaweza kuwa mstari wa mbele kuwaonea huruma wakazi waliobomolewa ilhali walivunja sheria, au tukawa mstari wa mbele kuiunga serikali ya awamu ya tano kumbe nao hawana sheria yeyote ile wanatumia tu ubabe.
NOTE:HUU UZI UTAKUWA MZURI SANA KAMA WACHANGIAJI WATAKUWA WANABANDIKA NA SHERIA ZA BARABARA ZOTE ZA MTAA, KUU, KUHUSU MWANANCHI AJENGE MITA NGAPI........... HII ITAEPUSHA USUMBUFU KATI YETU SISI,VIZAZI VILIVYOPO NA VIJAVYO, NA MAMLAKA ZISIZOZINGATIA SHERIA NA UTU KWA RAIA WAKE.
Sent using Jamii Forums mobile app