Bomoa Bomoa Awamu ya 2: Eneo la Jangwani - Dar es salaam

Bomoa Bomoa Awamu ya 2: Eneo la Jangwani - Dar es salaam

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,096
ZOEZI la Bomoa bomoa limeanza kwa kasi kwa awamu ya pili Jiijini Dar. Awamu ya kwanza ilianza mwezi mmoja uliopita (Novemba) na kufyeka majumba katika maeneo ya Mwenge, Kinondoni, Mbezi, Bunju n.k.

Sasa leo hii wakazi waliojenga maeneo ya Jangwani/Mkwajuni wamefikiwa na Tingatinga na ubomoaji unaendelea muda huu.

Wakazi wa maeneo haya waliokumbwa na zoezi hili wanalalamikia utartibu wa kustukiza unaotumika na kusema serikali iwe inawapa taarifa wananchi mapema ili wajiandae na sio kuvamiwa ghafla kama inavyofanyika hivi sasa!

Taarifa zaidi zaja..
 
Hao walishapewa viwanja mabwe pande Kitambi kwahiyo hawalutakiwa kuonekana hapo
 
Hao ndo wanasababisha jua liwe kali town, waache waende to
 
Wasilaum sana maana kubomolewa makazi wachukulie kama wamekumbwa na mafuriko,vyombo vmekwnda na maji,waanze upya,BOMOA
 
Utpiepo na kapicha ili tuone kama ndio wenye viwanja Mabwepande wameuza wakruidi ili mvua ikinyesha wapewe vingine maana nasikia biashara ya viwanja vya majanga ndio habari ya mjini
 
Kwa kweli ktk kundi la binadamu wanaoniudhi ni hao waliojenga mabondeni na walishapewa hadi viwanja lakini hawakuhama na waliendelea kuishi humo,sasa wasidhani hii ni awamu ya 4 (wadhani kesho watarudi wajenge tena) hii ni awamu ya 5 na rais ni Dr John Pombe Joseph Magufuli yaani hapa kazi tu.
 
Nawashukuru manispaa kwa kuwabomolea hawa watu wanao sababisha mafuriko....!
 
Masikini wakazi wa bondeni mkwajuni muda huu nyumba zao zinavunjwa na tingatinga,,,,source mi mwenyewe,,,,nimeshindwa kupiga picha nilikuwa kwenye daladala,,,
 
Mnaoshabikia ubomoaji wa nyumba za watu mjipange yakiwatokea ninyi. Haki za binadamu zizingatiwe ktk kutekeleza maagizo ya serikali. Mbona wakwepa kodi walipewa siku saba? Kwani sheria si ilishakuwepo wangewekwa rupango direct? Mnaonea dagaa, kumbe papa mnawagwaya. Mngeanzia zile za mikocheni na ufukweni kama mko kiuhalisia. Acheni usanii
 
Binafsi hawa siwezi kuwasikitikia kwani walipewa viwanja miaka mingi tu lakini walikataa kuhamia. Na kila maa ikinyesha mvua wanasababisha usumbufu kwa sababu ya mafuriko.
 
wabomoe na za masaki na osterbay,,,fear game /play na pale mesina mbezi kuna watu wamejenga juu ya mitaro ya maji maji hayana pa kwenda
 
Mnaoshabikia ubomoaji wa nyumba za watu mjipange yakiwatokea ninyi. Haki za binadamu zizingatiwe ktk kutekeleza maagizo ya serikali. Mbona wakwepa kodi walipewa siku saba? Kwani sheria si ilishakuwepo wangewekwa rupango direct? Mnaonea dagaa, kumbe papa mnawagwaya. Mngeanzia zile za mikocheni na ufukweni kama mko kiuhalisia. Acheni usanii

kweli mkuu,pale msasani bonde limezibwa na nyumba za vigogo kwa nini wasianze na hizo?
 
Pia kuna jamaa kanipigia simu kuwa leo Tazara nao wameweka nyumba X zilizo mita30 kutoka kwenye Reli yao kuanzia Tazara Station,wenye nyumba wamepewa siku3 kuanzia leo mpaka tarehe 20 Mwezi huu wawe washahama na kubomoa nyumba zao.
 
Back
Top Bottom