Bomba la gesi kutoka Kusini mpaka Dar lina manufaa gani?

Mzee2000

JF-Expert Member
Aug 7, 2009
527
221
Bomba la gesi kutoka Kusini mpaka Dar limeanza kujengwa leo. Thamani yake ni $bilioni1.

Kwa pesa hiyo litakuwa na manufaa gani?
 
ujenzi umeanza maeneo gani!? Nalile tangazo la vyama vya wafanyakazi wa mtwara kwamba huo mpango hawajawashirikisha wananchi ndio kusema limepuuziwa na serikali ama?
 
Halafu ni. watu wangapi wanauwezo wa kuvuta gesi majumbani mwao?Kama maji Dar ni shida sembuse gesi?
Huu ni mpango tu wa wakubwa.
 
bombagasdartolindi.jpg


914mm x 16.0-cubic-metre pipes at the construction site of the Kinyerezi gas receiving station and control room in Dar es Salaam yesterday. Laying of the gas pipeline, which is being undertaken by Chinese Petroleum and Technology Development Company (CPTDC) and is wholly owned by the government of Tanzania, will last for 18 months. On completion, the 700-kilometre-long pipeline will be able to transport 784 million cubic feet of gas a day from Mtwara

Picha kwa hisani ya Khalfan Saidi IPPMEDIA

Kikwete kuzindua mradi gesi kesho
Na Mwandishi wetu
7th November 2012

Rais Jakaya Kikwete kesho anatarajiwa kuzindua mradi wa ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi asilia kutoka Mtwara na Songosongo na bomba la mafuta la kusafirisha gesi hiyo hadi jijini Dar es Salaam.


Uzinduzi huo utafanyika katika eneo la Kinyerezi Ulongoni, Manispaa ya Kinondoni, mahali ambapo mitambo na bomba hilo vinatarajiwa kujengwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika eneo hilo ikiwa ni ziara yake kwa ajili ya kuweka sawa mazingira ya uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, akiambatana na menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, alisema ameridhika na maandalizi hayo na kwamba hakuna sababu ya kufanya uzinduzi huo usifanyike.

Sadiki pia aliwataka wananchi na wakazi wanaoishi kuzunguka eneo hilo kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya uzinduzi huo baada ya Rais kuwasili eneo hilo saa 3: 00 asubuhi.

Kamishna wa Nishati na Petroli, Mhandisi Hosea Mbise, alisema kuwa jumla ya mitambo minne yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 840 inatarajiwa kujengwa katika eneo hilo kwa mgawanyiko wa maeneo manne ikitokea Mnazi Bay, Somanga Funga na kukutana Songosongo hadi Kinyerezi na kusafirishwa hadi Tegeta kupitia Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mbese aliitaja migawanyiko ya maeneo hayo kuwa ni Kinyerezi ambako mitambo yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150 inatarajiwa kujengwa, Kinyerezi II mitambo ya Megawati 240, Kinyerezi III mitambo ya Megawati 300 wakati mitambo ya Megawati 150 itajengwa katika eneo la Kinyerezi 1V.

Kwa mujibu wa Joyce Kisemo, Mkurugenzi Masoko na Vitega Uchumi TPDC, Joyce Kisemo, mradi huo ulianza mwaka mmoja na nusu uliopita na kutarajiwa kukamilika Januari mwakani kwa gharama za Dola za Kimarekani bilioni 1.225 ambazo ni mkopo nafuu kutoka Serikali ya Watu wa China.

Source: NIPASHE
 
Halafu ni. watu wangapi wanauwezo wa kuvuta gesi majumbani mwao?Kama maji Dar ni shida sembuse gesi?
Huu ni mpango tu wa wakubwa.

Hiyo siyo gesi ya kuvuta nyumbani kwako. Ni tunatumia kuzalisha umeme itasaidia kupunguza gharama za umeme nchini tutaweka umeme hadi vijijini kwakuwa bei itapungua.
 
Ujenzi unaendelea, haya mambo kuna majirani zetu yanawarusha roho hadi wanatuvuruga ndani ya EAC.

IMG_0657.jpg


IMG_0661.jpg


IMG_0666.jpg


IMG_0746.JPG


01.JPG


[h=3]Serikali yaridhishwa na kasi ya ujenzi wa bomba la gesi[/h]Serikali imeridhishwa na kasi ya kazi inayofanywa ya mradi wa kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

Hayo yalibainika wakati Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Balozi wa China nchini, Lu-Youging walipofanya ziara ya pamoja kukagua ujenzi wa bomba hilo. Katika ziara hiyo walitembelea kambi tano za mradi za Somangafungu, Nyamwage, Ikwiriri, Mkuranga na Kongowe katika Mto Mzinga.


Waziri Muhongo alisema ameridhishwa na kasi ya kazi inayofanywa ya mradi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam huku akiwataka watanzania kuwa na imani na kazi hiyo.


Alisema awali zoezi hilo lilitakiwa kukamilika mwezi Januari, 2015, lakini huenda likawahi kumalizika kutokana na kuwepo kwa vifaa vya kisasa na imara kutoka Kampuni ya China Petroleum Pipeline (CPP) watakao fanya kazi ya kulitandaza.


Alisema mabomba hayo ni imara na yanaweza kudumu kwa zaidi ya miaka 70 iwapo yatatunzwa vizuri na kwamba serikali itahakikisha inayafuatilia vizuri na kuhakikisha hayachafuki


Waziri Muhongo alisema kazi ya kuunganisha vipande vya bomba inaanza rasmi tarehe 26 Agosti na wakati huo uchimbaji ukiendelea kwa ajili ya kuweka mabomba hayo ambayo yatakuwa tayari yameunganishwa.


"Uunganishwaji unafanywa na mitambo ya kisasa kabisa na hapo bomba linapochimbiwa ndio hapohapo uunganishaji unafanyika na bomba zitakazolazwa baharini zitaunganishwa hukohuko" alisema.


Alisema kwa bomba zitakazoenda baharini uzito wake ni mkubwa zaidi ikilinganishwa na bomba zitazotumika nchi kavu kwakuwa zitakazolazwa baharini zitawekewa zege maalumu.


"Bomba zitakazoenda baharini zitakuwa na uzito wa zaidi ya tani 10 baada ya kuwekewa zege ambapo kwa sasa zina uzito wa tani tatu" alisema.


Alisema kazi ya kutandaza mabomba baharini itaanza Septemba 16, mwaka huu kwa kuwa kazi hiyo inahitaji umakini mkubwa.


Profesa muhongo alisema pindi bomba hilo litapokamilika uzalishaji wa umeme utaongezeka kutoka megawati 1500 zilizopo hadi kufikia megawati 3000 mwaka 2015 na kuanza kuuza umeme utakaokuwa wa ziada kwa nchi jirani.


Kuhusu suala la ajira, Waziri alisema mradi huo tayari umezalisha ajira. Alisema magari ya watanzania yapatayo 45 yamepewa kazi ya kusafirisha mabomba huku watanzania wengine wakiajiriwa katika kazi zinazoendelea.


Balozi wa China nchini, Lu Youging alisema mradi huo ni wa kipekee na una umuhimu mkubwa sana kwa uchumi wa Tanzania kwani kupitia mradi huo, Tanzania itaweza kuwa na viwanda vingi na kupelekea kuongezeka kwa ajira nchini.


Aliongeza kuwa mradi huo utasaidia katika utunzaji wa mazingira kwakuwa badala ya kuendelea kukata miti kwa ajili ya mkaa na kuni, watanzania watatumia gesi asilia kwa matumizi ya kupikia.


SOURCE: MICHUZI
 
Chinese are saying the speed is impressive, look at the map and see the updates of laying the pipe can be done by 2014 :banana:



























 
Back
Top Bottom